Yanga yatanguliza mashushu Sudan, mmoja kati ya walioenda ni Mwakalebela

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
4,084
8,664
Yanga SC ni timu kubwa sana wakati timu nyingine hubabaika sana na kutanguliza mashushushu wiki 2 kabla wao wanapeleka baada ya mechi ya kwanza, huo ndiyo ukubwa wa timu inayojiamini. Yaani kiwango cha Mamelodi, Raja, Wydad.

Sasa zikiwa zimebaki siku 5 ndipo Yanga wamepeleka mashushushu wawili Khartoum kuweka mambo sawa kabla ya kwenda kupindua meza kwa kuwachapa timu ndogo ya Al Hilal mabao 2-0.

Anayebisha abishe tu lakini Al Hilal kazidiwa kifedha na Yanga, kazidiwa ubora wa wachezaji, kazidiwa ubora wa benchi la ufundi.

Mwakalebela na shushushu mwenzake wanatarajiwa kufanya kazi nzuri tofauti na iliyofanywa na shushushu Senzo aliyetangulizwa kule Rivers State
Nigeria akiambatana na mpishi wakafanikisha kuweka sawa mambo ya ugali na dagaa wakisahau mambo mengine hadi Jenerali Bugatti alipoingilia kati pale uwanjani na kuwaambia wachezaji "ZIS IS WAR ZIS WAR, WAR IS ZEA".

***Hii picha haihusiani na mashushu bali ni kikosi kazi cha kushughulika na kesi za Yanga huko CAS na FIFA na huwa kinashindwa kesi kila siku! Hapa kilikuwa mubashara mtandaoni kikipambana na wakili msomi Bm3 wakaangukia pua

mashushu.JPG
 
Shushushu ana mwili mkubwa vile si atashtukiwa hata kabla hajaanza kazi.
Thats the idea, huyo ana divert attention wakati wa sudan wameweka macho yote kwake, shushushu namba 2 anatengeneza mazingira ya kuwapa raha wananchi jumapili
 
Hata wangeenda mashushu kumi, kufungwa ni pale pale, ukishindwa kufunga uwanja wa nyumbani kwenda kufunga ugenini huwa ni bahati ambayo huwa haiji mara 2 mlipata ya kwanza kwa Township Roles, Round hii mtapigwa kama ngoma.
 
Uwanjani mnacheza 22 home advantage ipo lakini sio guarantee ya ushindi De Agosto kwafungwa kwao na Simba hata Simba kasha fungwa hapo kwa Mkapa na Juaneng Galaxy hio mechi bado mbichi tuwe na akiba ya maneno
 
sasa makolo team mbovu ni ya kuitolea mfano? toa mifano ya teams nyingine kubwa level ya yanga kama mamelodi, raja, waydad, berkane,mazembe
 
Back
Top Bottom