SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,149
- 7,913
Jana nilisikia kuwa Yanga baada ya mechi yao na Medeama, walizungumza na mshambuliaji wao hatari aliyewasumbua sana Jonathan Sowah kwa nia ya kumsajili.
Nakumbuka msimu uliopita katika mashindano ya shirikisho, karibia kila timu iliyokuwa inacheza na Yanga, baada ya mechi ya kwanza na timu hiyo, kabla hata ya kurudiana walikuwa wanaonyesha waziwazi interest na wachezaji walioonekana hatari wa timu pinzani na kuwaahidi kuwasajili. Nakumbuka walifanya hivyo kwa TP Mazembe, walifanya hivyo kwa AS Bamako. Walipokutana na Monastir, ghafla tawi lao Singida Big Stars wakaingia ushirikiano na Monastir. Tulio na jicho la tatu tulihoji haya mambo toka kipindi kile. Baada ya mission katika shirikisho kufanikiwa hakuna mchezaji wa TP Mazembe wala Bamako aliyesajiliwa Yanga msimu huu wala ule ushirikiano na SBS hatujausikia tena.
Kwa mtazamo wangu hizi ni mbinu chafu zisizo za kiungwana na kimichezo za kurubuni wachezaji ili kuwapunguza makali kabla ya mechi ya marudiano, ili mchezaji asicheze kwa kiwango chake akidhani atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga baada ya muda mfupi. Mbinu hii pia siyo fair kwa timu yake ya sasa inayomlipa mshahara wake. Mara nyingine unakuta timu inaamua hata kutompanga huyo mchezaji katika mechi ya marudiano wakiwa na wasiwasi hatacheza kwa bidii.
Embu waza Yanga wangefanyiwa kitu kama hicho kwa timu pinzani kuonyesha interest waziwazi kwa kuongea direct na mchezaji wa Yanga katikati ya mashindano bila kwanza kwenda kwa uongozi wa timu. Naamini wote tunajua jinsi malalamiko yao yangekuwa maana tuliyaona wakati wa sakata la Feisal na Azam. Hizi ni janja janja za muda mfupi na mwisho wa siku zinagonga mwamba maana sitegemei kama wataweza kufanya hivyo kwa wachezaji wanaojitambua wa CRB au wa Al Ahly.
Nawasilisha.