Yanga VS Simba 13.08.2022

CARDLESS

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
7,786
15,732
Wadau habari za usiku, ni matumaini yangu mko poa kabisa, na kwa wale wenye matatizo ya basi M/Mungu wafanyie shufaa warudi kwenye hali zao za awali.

Mara baada ya salamu na dua zangu kwenu basi niende moja kwa moja kwenye mada husika. Na kabla ya kuzama ndani MIMI NI MPENZI WA YANGA hapa TZ, MAN UTD kwa ULAYA, na BRAZIL kwa level za MATAIFA.

Tunatarajia kuwa na mtanange wa kukata na shoka baina ya SIMBA na YANGA weekend inayofuata yaani 13.08.2022.

Kutokana na michuano mbalimbali ambayo itafuata kwa msimu mpya basi kila timu imefanya usajili ikiamini inaweza kuponya matatizo yaliyowasibu msimu ulipita.

Tukianza na Yanga wao, wameleta wachezaji hawa hapa.

1. Morrison - Winga
2. Ki Aziz - Winga/Mshambuliaji
3. Lomalisa - Left back
4. Kambole - Mshambuliaji
5. Bigirimana - DFM Kiungo

Kwa upande wa Simba wao, wameshusha nondo hizi hapa.

1. Okrah - Winga
2. Okwa - Winga/Kiungo
3. Oattara - Center Back
4. Phiri - Winga
5. Georgonovic - Mshambuliaji
6. Akpan - Kiungo DFM
7. Kyombo - Mshambuliaji
8. Kapama - Beki/Kiraka

Hapa lazima kwanza tujue kuna maboresho ya kikosi na Ufumuaji wa kikosi.

Tukubali au tukatae YANGA wao wameboresha kikosi wakati SIMBA amefumua Kikosi.

Timu zote hizi mbili zimepata mchezo wa kujipima uwezo wa kimataifa. Mimi nimeona nini kwenye hizi timu zote mbili kuelekea msimu ujao.

YANGA nilichokiona, kwa nafasi walizosajili katika kuziba mapungufu yao ya msimu ulipita hasa Wings, Kiungo wa Chini, na beki wa kushoto. Wao kwa kuangalia mchezaji mmoja mmoja wamefanikiwa kwa 80%, yes sio 100% kwa sababu mpira una mambo mengi sana, majeraha, kutofit kwenye mfumo nk.

SIMBA nilichokiona, kwa nafasi zao zenye shida hasa Kiungo wa chini, Beki wa kati, mshambuliaji wa kati, wings zao. Kwa wao nawapa alama 60% hadi 70% yes ni hizo alama na sio 100% kwanini, Simba ilihitaji wachezaji wachache tu lkn wameenda kuchukua wachezaji wengi zaidi ya kilichotakiwa.

MIFUMO NA NAMNA TIMU ZINACHEZA NA MATARAJIO YA WENGI.

SIMBA kwa muonekano ni mchanganyiko wa watu wa Speed na Slow, ndio, iko hivyo, Ukiwa na kiungo kama CHAMA, KANOUTE/MZAMIRU na MKUDE tegemea timu kucheza mpira wa taratibu sana. Hapa CHAMA ni namba 10. Ukiwa na SAKHO, OKWA, na AKPAN hapa utakuwa timu yenye speed.

Wapenzi na mashabiki wa Simba wanafaa watambue wazi kuwa timu yao ina maingizo mapya mengi mno, na uchezaji wao sio kitimu ni ile individual performance, ndio unaona mchezaji anakokota mpira bila hata kuangalia mwenzake yuko wapi au apasie kwa wakati gani au upande upi.

Viungo wa Simba wanapoteza mipira hovyo, back pass ni nyingi mno huku wakitengeneza nafasi finyu za kupenyeza mpira kwa namba 9 wao.

Bado tatizo la Ushambuliaji halijakaa sawa na hii itafanya upotevu wa nafasi muhimu sana.

Sina shaka na back line ya SIMBA hata kidogo, ingawa nimemuona sana INONGA akiturn hovyo na bila tahadhari zozote, sijui ni uchezaji mpya au ni ile kuona anaweza kufanya vyovyote as wanasimba wanamuamini na kumwelewa sana.

Kwa upande mwingine YANGA wao wameboresha tu kikosi chao lkn hii haifanyi kuwa wao ni bora kwa msimu ujao HAPANA, HAPANA, HAPANA.

Yanga lazima waingie SOKONI kumalizia kitu, ndio lazima warudi SOKONI kununua Beki mmoja wa kati, Mwepesi na mwenye accuracy nzuri kwenye passing, blocking na awe mwenye speed. Pamoja na ubora wa YANGA ila MWAMNYETO sio beki wa kumtegemea na ni njia nyepesi mno kwa zile foward hatari. Beki zingine kama KUSHOTO na KULIA kuko salama kabisa chini ya DJUMA (Apunguze uzito kidogo) LOMALISA kushoto kule.

Eneo la kati ya uwanja Yanga wao wana wachezaji angalau wanaoendana kiasi, Speed. Aina yao ya viungo ni wale twende mbele na tukirudi basi tumebanwa mno. Eneo hili ili Yanga iwe salama zaidi inahitaji iwe na BIGIRIMANA, AUCHO/SURE BOY na FEISAL hapa watapata NGUVU, SPEED na Accuracy kubwa ya pasi zao.

Pamoja na hayo yote lkn pia hii timu lazima itambue kuwa ni ngumu mno kwa FEISAL kucheza sambamba na KI AZIZ, Yes ni ngumu, kwa sababu Feisal ni mzito kidogo wakati Ki Aziz ni mwepesi mno hivyo kufanya idadi kubwa ya pasi kupotea kwa kupisha speed zao. Feisal anatakiwa kujiimarisha kwa speed na balance nzuri kuendana na mwenzake.

Kwa ujumla hizi timu zikikutana itakuwaje??

Binafsi kwa kuangalia hizi timu mechi ijayo ukiondoa mambo ya misumari nk game haitokuwa nzuri sana, ndio haitokuwa nzuri sana kwa sababu Yanga wana beki mbovu za kati, wakati Simba wana washambuliaji na Viungo wabovu. Mechi hii itaamuliwa zaidi na mipira iliyokufa. Direct freekicks zinaenda kuamua hii game, kwa maana wachezaji hawana tahadhari juu ya hayo maeneo.

Kama Simba wataenda kurekebisha tatizo lao la VIUNGO kucheza kila mtu kivyake basi hii game YANGA anaenda kufa 2-0 au Zaidi.

Kwann nimetabiri hivi??
Uimara wa beki za Simba na ukijumlisha na marekebisho kwenye eneo la kiungo basi YANGA hawatoweza pata goli lolote huku Simba wakijaribu kupata zaidi ya Goli moja.

Lakini pia kama watacheza kama nilivyoona leo hii aina ile ya ukabaji SIMBA anaenda Kufa 2-1. Simba nimewapa goli kutokana na uzembe wa beki za kati za Yanga lkn kama Yanga watalifanyia kazi tatizo lao na Simba yule INONGA akicheza kwa namna amecheza leo hii SIMBA anaenda KUFA 3-0.

Kwann nimetabiri magoli hayo?? UBORA WA WASHAMBULIAJI WA YANGA ni MKUBWA kulinganisha ni Simba, chemistry ya Timu yenyewe na aina ya Udhibiti kwenye eneo la kiungo.

TUSUBIRI 13.08.22.
 
Kumamake nyie wakuda Uto, round hii mtatwambia ilikuwaje mkawa unbeaten msimu ulioisha?

Tutawapiga katerero moja tajatifu mpaka mrushe maji.

*****

cocastic
 
Kumamake nyie wakuda Uto, round hii mtatwambia ilikuwaje mkawa unbeaten msimu ulioisha?
...
Mkuu mpira sio tu umeshinda ndio timu yako imekuwa bora, hatufangalii hivyo mkuu.

Yanga wanacheza as a team, Simba wanacheza kila mmoja kivyake, huwezi kujua pasi itahama hapa kwenda kule au kiungo fulana ataenda kuiomba pale ili apige pale.

Simba bado hawana kiungo mkabaji wa maana. Akpan ni mzito na anapoteza mipira hovyo, kitu ambacho ni hatari na game nyingi tutendelea kumuona sana MKUDE au MZAMIRU akishuka chini.

Nimemwangalia OKRAH sijui lkn kwa nilivyomuona ana safari ndefu mno kwenye ligi yetu, Simba imeongeza wachezaji wa aina ile ile (Machachari) OKWA, PHIRI, OKRAH timu yoyote ile inahitaji balance ya hizo namba. Huwezi na Wings zote wafupi tupu, kuna game utahitaji watu warefu wakapambane nk.

Yanga wao nilichokiona kwao ni wapate beki mmoja wa Kati mbadala wa MWAMNYETO basi, timu yao ni nzuri kwenye eneo, kuanzia Nyuma hadi Mbele.

Ni ngumu sana kwa timu za Ligi ya Bongo kuchukua Point mbele ya Yanga, ni Ngumu mno.

Subiri Ligi ianze utaelewa hiki. Nakumbuka mwaka jana kwenye Simba day, tulisema hivihivi kuwa Simba ni Mbovu ila watu hawakukubali.
 
Kumamake nyie wakuda Uto, round hii mtatwambia ilikuwaje mkawa unbeaten msimu ulioisha?

Tutawapiga katerero moja tajatifu mpaka mrushe maji...
Kwa nini mnapenda sana kutukana tukana matusi hovyo! Kama mada haikufurahishi, kwa nini usipite tu kimya kimya!

Katika maisha tukikosa kitu kinachoitwa ustaarabu, hakika tutakuwa ni watu wa hovyo sana.
 
Twende mbele turudi nyuma mechi za simba na yanga huwa hazitabiriki....japo simba amekuwa mnyonge kwa yanga misimu kadhaa, binafsi naenda kuiona Derby bora kutokea misimu yote maana kila timu imefanya usajili wa kibabe binafsi natabiri matokeo yatakuwa sare ya 2-2.
 
Mkuu unafundisha timu gani hapa Tanzania? Tuanzie hapo kwanza! Siyo unaleta ndoto zako kabla hatujakufaham.
 
Utopolo watakufa za kutosha.
Ila Mimi nalia na Simba hawapo serious na biashara ya jezi.
Kama wametoa jezi 4,000 na zimetoka zote na Kama wameuza kwa 35,000 watakuwa wamepata milion 140.
Biashara ya jezi inaonekana ni nzuri na inalipa wawekeze huko.na wawe na vituo maalum vya kuuzia jezi MIKOA YOTE.zisiuzwe tu kiholela
 
Mkuu unafundisha timu gani hapa Tanzania? Tuanzie hapo kwanza! Siyo unaleta ndoto zako kabla hatujakufaham.
Kwa sasa niko COPENHAGEN, DENMARK. Vp unataka kusemaje?? Najua mpira na sijaongea kishabiki hapo ni vile nimeona hayo matamasha.
 
Back
Top Bottom