Yanga SC sasa kucheza nane bora Africa; CAF yaifuta Lupopo

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,735
20,484
CAF yaifuta Lupopo; Yanga SC sasa kucheza nane bora Africa

Na mwandishi wetu

Timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam nchini, pengine inaweza kuwa ni timu yenye bahati kubwa mwaka huu baada ya kupangwa katika hatua ya makundi ya nane bora katika hatua ya robo fainali ya kombe la Klabu Bingwa Afrika. Uamuzi huo umefikiwa na Shirikisho la Soka barani Africa (CAF) baada ya kuiondoa timu ya St. Eloi FC Lupopo ya DRC kutokana na timu hiyo kumchezesha mshambuliaji wa kimataifa kutoka Zambia, Felix Mumba Sunzu pamoja na Félicien Tshamalenga Kabundi ambaye hakusajiliwa katika mashindano ya CAF, ila Lupopo walimuingiza katika orodha ya wachezaji wake kinyemela kuziba nafasi ya aliyekuwa mshambuliaji wao hatari, Ndume Wa Ndume aliyekwenda kufanya majaribio nchini Ubelgiji katika klabu ya Vassalund anayochezea mtanzania Mohamed Rajabu maarufu kama Athuman Machupa.
Katika kikao hicho iligundulika kuwa mshambuliaji mzambia Felix Mumba Sunzu alicheza huku akiwa na adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata msimu uliopita wa 2009 katika mechi ya fainali kati ya TP Mazembe ya DRC na Heartland ya Nigeria ambapo Mazembe waliibuka mabingwa wa Afrika baada ya kuwashinda wapinzani wao kwa bao 1-0 licha ya kufungwa 2-1 nchini Nigeria, na waliibuka washindi wa ujumla kwa faida ya bao la ugenini. Mzambia huyo aliichezea Mazembe msimu uliopita kabla ya kujiunga na Lupopo kwa mkopo.
Kwa mtaji huo Tanzania inakuwa na wawakilishi wawili katika michuano ya kimataifa, kwani wapinzani wa Yanga, Simba SC ndio waliokuwa wamebaki pekee kwani wao hawakucheza raundi ya awali kutokana na kile kilichoelezwa na CAF kwamba Simba iko katika kiwango cha juu Afrika, hivyo haiwezi kupangwa raundi ya awali kama zilivyokuwa Yanga na Lupopo.
Mwandishi wetu alijaribu kuwasiliana na viongozi wa Lupopo ili kupata maoni yao kuhusu uamuzi huo wa CAF, lakini juhudi zake ziligonga mwamba kwani kila aliyepigiwa simu alidai hawawezi kulizungumza kwa sasa kwani kwa siku ya leo ni sikukuu huko kwao DRC na hawapo ofisini, na waliahidi kuzungumzia baadaye saa nne kwani kwa sasa wamechanganyikiwa habari za ‘kijinga’ kutoka CAF .
Kama ni kweli waanze maandalizi mapema
 
Hivi leo ni tarehe ngapi vile. Naona kama kuna watu fulani ambao kinyume chao ni werevu wanasherekea siku yao!
 
Back
Top Bottom