MUSHEKY
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 2,812
- 2,754
Wakuu kwa kuwa nchi yetu inafuata utawala wa sheria ningependa niwasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano.
Nijikite kwenye mada,
Mnamo tarehe 24 Juni, 2010 mshambuliaji na nahodha wa Timu ya Taifa ya Ufaransa Thiery Henry aliitwa na kuwekwa kikaangoni na Rais wa Ufaransa wa wakati huo Nicolas Sarkozy aandike insha isiyopungua maneno 2000 juu ya kwa nini walivurunda kwenye fainali ya Kombe la Dunia kwa mwaka huo.
Kana kwamba haitoshi Serikali ilionyesha karipio lao kwa timu kwa kuisafirisha timu yote na benchi la ufundi kwa tiketi za "Economy class" ili iwe fundisho kwa vizazi vijavyo.
Ili kuonyesha kwamba mambo hayo siyo mageni, tukirudi nyuma kidogo mnamo mwaka 1994 na 1998 kwenye Makombe ya Dunia (la Marekani na Ufaransa), nchini Iraq nako mambo yalikua si shwari kwa timu ya nchi hiyo iliyokua inapambania kufuzu fainali hizo, ambapo mtoto wa kiume wa Saddam Hussein bwana Uday yeye alianzisha Guantanamo ya kimichezo kwenye floo ya chini katika jengo la Kamati ya Olimpiki ya nchi hiyo.
Bwana Uday aliwasweka wachezaji kwenye chemba hizo za mateso mara kwa mara na kuwatishia kuwakata miguu na kuitupa kwa mbwa wakali waliozunguka chemba hiyo ya mateso.
Sambamba na hilo mwaka 2000 nchini Ivory Coast kwenye harakati za kufuzu AFCON mtawala wa kijeshi wa wakati huo ambaye sasa ndiye Rais wa nchi hiyo, aliisweka timu yote pamoja na viongozi wake kwenye kambi ya kijeshi, wakapewa msoto mkali baada tu ya kutolewa kwenye raundi ya kwanza ya michuano hiyo ya Mataifa ya Afrika.
Sambamba na hilo, hivi majuzi waziri wa nchi mwenye dhamana ya michezo Mohamed Mchengerwa alitoa agizo zito kutoka Serikalini kwenda kwa Klabu ya Yanga, kwamba Serikali inaiagiza Yanga kwamba ni lazima ikashinde mechi yake ya marudiano dhidi ya Wasudan.
Na kwa kuSa Dar es salaam Young Africans ilienda Sudan kuliwakilisha taifa, pengine ndiyo hasa msingi wa kauli ya kiongozi huyu mkubwa wa nchi kuipa agizo hili Yanga ambalo kiukweli limegeuka kuwa mzigo mzito kwa timu pamoja na uongozi.
Sasa kwa kuwa Rais wa Yanga alisikika akipokea maagizo hayo ya Serikali na kuahidi kuyatekeleza, ni wakati muafaka sasa kwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuipa adhabu nzito timu ya Jangwani kwa kushindwa kutekeleza au kupuuzia maagizo ya nchi.
Mchengerwa kuwaacha Yanga hivi hivi ni kutengeneza "Double standards" na kukufanya upuuzwe hata wakati mwingine ukitoa maagizo kwa wengine yatapuuzwa tu!
Napendekeza uongozi wa Yanga wakiwemo Injinia na Profesa na wachezaji wote akiwemo Mwamnyeto na Mayele, wapelekwe Kambi ya Lugalo kwa walau wiki moja wakapigwe "Rolling" na kata tumbo ya kufa mtu ili iwe fundisho kwa timu za nchi hii kuliletea taifa aibu.
Ikumbukwe pia Yanga imeshindwa kuakisi harakati za Rais Samia za Royal Tour za kuitangaza nchi yetu kimataifa kwa mara ya pili mfululizo. Sasa jambo ambalo halivumiliki hata kidogo, kwani hali hii inachangia kudidimiza sekta ya utalii nchini.
Nawasilisha.
Sent from my M100 using JamiiForums mobile app