Uchaguzi 2020 Yanayojiri Mapokezi ya Tundu Lissu jimboni Mkalama na Singida Mjini

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mcheza kwao hutunzwa.Ndivyo tunavyoweza kuelezea mapokezi ya Tundu Lissu hapo Jana alipokanyaga Ardhi aliyozaliwa.

Leo Mgombea huyo anayepewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda atafanya kampeni zake katika Jimbo la Mkalama na baadaye Singida Mjini.

Tundu Lissu ameandika historia mpya ya Mgombea anayependwa na maarufu zaidi kati ya wagombea wote ingawa hajaweka bango hata moja katika nchi nzima huku mshindani wake wa Karibu akiwa ametapaza mabango kila mahali mpaka kwenye miti ya watu mashambani na vichochoroni.

Katika hali inayochekesha na kushangaza vigenge vya wanaCCM vinavyofadhiliwa na chama hicho vimekuwa vikiandaa tafiti feki za kuonyesha mgombea wao atashinda ili kuhadaa watu na labda kuhalalisha wizi wa kura.

Tunatarajia kuwaletea kila kinachojiri katika kampeni za Leo za mgombea huyu ambaye anaonekana wazi ana kibali duniani na mbinguni

---------- ------------- ---------
Yaliyotokea saa 7 Mchana

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu akizungumza na wananchi wa Iguguno waliosimama barabarani kuzuia msafara wake uliokuwa njiani kuelekea Kata ya Nduguti viwanja vya gulio jimboni Mkalama Mkoa wa Singida.

‘’Maandiko matakatifu yameandika haki huinua taifa, taifa letu litainuka kukiwa na haki na tukiwa huru na tunataka maendeleo yenye maana kwetu‘’ - @TunduALissu

‘’Mtoto wako akienda shuleni au hospitali atendewe haki na sio kununua haki, mama lishe atendewe haki na bodaboda atendewe haki’’ - @TunduALissu

"Nawambia wakazi wa Singida, kama unataka kuwa huru kuuza biashara zako ukiwa huru, uuze chochote unachozalisha ukiwa huru chagua Tundu Lissu’’ - @TunduALissu

Mhe. Rais amemnadi Mgombea Ubunge Jimboni hapo Oscar Alex Kapalale.
 

Attachments

  • IMG-20201011-WA0015.jpg
    IMG-20201011-WA0015.jpg
    66.6 KB · Views: 1
  • VID-20201011-WA0049.mp4
    9.5 MB
Sawa TL anaweza akashinda kwa % zaidi ya 60 ila, je watanzania wako tayari kupokonya kuulinda nakuchukua huo ushindi kwa wababe ambao waka tayari kwa lolote ilahali wasipoteze uraisi? ...... ....wako wapi ambao wako tayari kufa kwaajiri ya maabadiliko?
 
Kuna watu tunatoa sifa na matumaini kwa wagombea wetu mpaka wagombea wenyewe wanashangaa jinsi wanavyotumainishwa! All in all yote kheri, 28 Oct hiyoooo! Hii si kama show ya simba na yanga, Mara ratiba kubadilishwa, hii ni no matter what could happen, ratiba haibadilishwi! Na kakinglish nimetumia , hahahah!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom