Yanayojiri Bungeni Dodoma: Ijumaa Tarehe 11 Aprili 2014 - Uwasilishaji wa Taarifa za Kamati

Weston Songoro

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
2,793
1,083
UKAWA leo wamechanganyikiwa baada ya Ummy Mwalimu, Mwenyekiti wa Kamati Namba Moja kumwaga nondo za kutetea muundo wa serikali Mbili na kuuponda muundo wa Serikali tatu.

- Juma Duni Haji, Akiwasilisha maoni ya wachache kutoka kwenye kamati namba 11 ambapo alianza kwa kusema,

1. Hoja za wengi ni muundo serikali ya shirikisho kuua udugu, kwani kabla ya muungano hatukua na udugu.

2. Kuna wajumbe wanasema kuirudisha serikali ya Tanganyika ni kufufua makaburi, kwani imezikwa? ninachofahamu mimi Tanganyika imekufa kwa kubadilisha jina tu.

3. Wengine eti serikali3 zitarudisha usultani Zanzibar, Loooooh! Mashaaalah, baada ya miaka 50 tunayazungumza haya? katiba ya sasa kifungu 98b kimetoa ruhusa Watanganyika na Wazanzibar wakikubaliana muungano utavunjika sio lazima serikali 3.

4. Mabunge ya sasa yana wajumbe wasiopungua 438 ya serikali 3 yatakua na 314 sasa mtu anaibuka tu na kusema serikali 3 gharama.

5. Ikaelezwa Zanzibar kuruhusiwa kutafuta misaada nje kwa nini mliizuia sasa baada ya serikali 3 mmerejesha? Ikaelezwa pia mafuta kuondolewa ktk orodha ya mambo ya muungano, ni miaka7 hii lilipitishwa, kisa serikali 3 ndio mnaliondoa?

6. Katika dharau tunayofanyiwa kwa udogo wetu Znz tunaambiwa hatuna uwezo kuchangia muungano, pato la Mznz na Mtanganyika halina tofauti, Tanganyika ni kubwa lakini kwa mmojammoja umasikini wetu ni sawasawa.

7. Makusanyo ya muungano yanayotumika kwa muungano hayajazidi 35% ambapo si chini ya 60% yaliyobaki yanatumika Tanganyika, hizi tume ambazo haziundwi na account kutofunguliwa ni kwa sababu mapato haya Znz haitakiwi kupata.

8. Sifa ya Zanzibar kwa miaka 50 kama serikali hizi mbili kweli zilikua na nia njema, Zanzibar ingekua sasa Hongkong ya Afrika.

9. Znz haina benki kuu wala sarafu yake na sera zote za uchumi ziko chini ya Muungano, Zanzibar mmeifunga miguu na mikono, leo kutatua matatizo ya Muungano kwa mfumo wa serikali 3 linatangulizwa swala la gharama, kwani lini zilikua ndogo?

10. Nilisoma kwenye magazeti miaka 50 uhuru wa Tanganyika si chini ya Bilioni 70 zimetumika katika sherehe, sherehe zenyewe za uwanja wa taifa kutazama gwaride watu wanavyorusha viatu, hayo hayo miaka yote.

11. Mikoa ya Tanganyika wakati wa 64 ilikua 17 tu ila sasa haipungui 26, Wilaya zilikua 60 mpaka 70 lakini sasa hazipungui 150, kila ukipanua madudu haya unaongeza gharama za utawala, yanatuhusu nini sisi Wazanzibari magharama haya?

12. Alichofanya Warioba ni kujaribu kusahihisha haya ya miaka 50, baada ya kutusaidia wengi mnataka hali hii iendelee?
 
Kumbe ummy mwalimu naye ni kiboko kwenye kuwasilisha ameiva kweli.
 
Kwanini hasomi? Yaani jamani mbona wanajidhalilisha? Unaweza kutoa ushindi kwa wapinzani wako kwa ujinga wako!
 
Wakuu. kama ilivyo kawaida yetu huwa tunakuwa na Uzi hapa kwaajili ya yale yanayotokea bungeni ili kutoa msaada kwa wale wasio fuatilia kupitia Tv na kubadilishana mawazo kulingana na kile kinachotokea bungeni sasa naona uzi rasmi hapa haupo so niwaombe wale wanaofuatilia na wale walioko bungeni watupie updates hapa

cc Skype
Kb 10
Chabruma
na wengine wote

BACK TANGANYIKA
 
Sijaona mtu bogust kama huyu Mama... Hopeless kabisa.... Ni zeroooo ... Anamwaga pumba za kufa mtuuuuuu.....
 
Back
Top Bottom