Yametimia-Mhyao keshamtia mimba mpwa wangu...........!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Wana JF,Niliwahi kuja na uzi huu hapa chini:
https://www.jamiiforums.com/mahusia...myao-kwa-mpwa-wangu%85%85%85%85%85%85%85.html

Siku za hivi karibuni, nilianza kuona mabadiliko kutoka kwa mpwa wangu, malaria haziishi na kutapika hakuishi. Jana mama Ngina kanijuza kwamba mpwa ni mjamzito na mtuhumiwa ni Mhyao.
Kwanza huyu mpwa keshafanya mtihani wa kidato cha nne na kapata Division four. Nilikuwa nafikiria kumpeleka kozi ya Secretarial lakini ndio hivyo tena, mjukuu mwingine huyo yu aja.

Kweli ng'ombe wa masikini hazai.
 
Khaaa mtambuzi, mbona dunia haina urafiki na wewe? Naona kila siku unakuja na visa vipya, pole sana na jiandae kwa kulea mjukuu. Ndo ukubwa huo.
 
Khaaa mtambuzi, mbona dunia haina urafiki na wewe? Naona kila siku unakuja na visa vipya, pole sana na jiandae kwa kulea mjukuu. Ndo ukubwa huo.


Kaka sikio la kufa halisikii dawa...........!
 
Mkuu pole sana. Ukiona hivyo ujue utu uzima umekamilika. Kuitwa babu ni heshima, lakini inapendeza zaidi hiyo heshima ikija kiheshima heshima. ndo ukubwa huo tumia busara zako kulitatua tatizo hilo.
 
mpeleke kwa shangazi yake.....si alishikilia mkwanja?
la mpeleke kwa huyo mwanaume.....
au mrudishe kijijini....
ila unahuruma sana mlee ila funzo watakalojifunza kina Ngina usilie na mtu
 
Pole mkuu gust,

Unabahati hajasema mtuhumiwa ni wewe!
Maana hawachelewi hawa ukionyesha hutaki wanalolitaka basi so linakudondokea
Na raia wananza oh ndio maana hakutaka.
Mwache aende naye atakalishwa kama mwenzie
 
Daah! sasa anakuwa mke wa pili ama wa kwanza anaondolewa au mhyao keshapata alichotaka atasepa mtambuzi alee mjukuu? ama sikio la kufa halisikii dawa! pole mtambuzi!
 
Honengera nyingi kwako kwa kuongeza wajukuu baba,

Na km hali ya hewa itaendelea hivi jiandae kupata mjukuu mwingine maana sijui km msimu huu nitanusurika lol!
 
Honengera nyingi kwako kwa kuongeza wajukuu baba,

Na km hali ya hewa itaendelea hivi jiandae kupata mjukuu mwingine maana sijui km msimu huu nitanusurika lol!
Ninyi mtaniuwa kwa Presha mwaka huu..................Hebu nipeni BREAK kwanza.
 
Back
Top Bottom