Yamenikuta ukweni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
YAMENIKUTA UKWENI

Shangazi'enu aliniomba nimpeleke hom kwetu akaonane na bi mkubwa, nikakataa KUTOKANA na sababu BINAFSI lakini baadaye alipokaza uzi, nikaona acha nimpeleke.

Ile tumefika, nikachukua parachichi nikalipondaponda kwenye maharage, akakataa kula akidai nimemfanyia kusudi ili aone KINYAA ashindwe kula. Nikaomba radhi, yakaisha.

Baada ya mwezi kanipeleka kwao, kimbembe kwenye msosi
Siku ya kwanza, kifungua kinywa mabibo na togwa, nikaona duuu!
Siku ya pili, kufungua kinywa embe na uji, dah!
Siku ya tatu, mahindi ya kuchoma na maji ya kunywa ya kisimani,

Nikamchek mwanangu na kumpanga anipigie na aniambie kuwa bosi anataka nirudi kazini haraka.
Mwana akanipigia, nikaweka loud speaker, wote wakawa wanasikia na kusikitika kuwa nitawaachia ukiwa
Wote walilalamika kuwa sikukaa sana

Hivi, shangazi'enu alifanya kunilipia kisasi au ndo ULIKUWA UHALISIA wa maisha yao
Si unajua tena mapenzi upofu!!

ILA SIMWACHI.
KWANZA BIBO NA TOGWA VINAENDA KULIKO MICHAI YENU NA MICHAPATI YENYE HAMIRA.
 
Usimwache alikurudisha paradiso kwenye asili. Wengi wetu tunapenda vyakula vya mchongo
 
Wakwe wapo Nachingwea?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom