Yaliyojiri Mkutano wa CCM na waandishi wa habari Peacock Hotel

breaking newzz!
yule mgombea aliepigwa na mh ndugai afariki dunia mda mfupi uliopita. akizunguzia tukio hilo mganga mfawidhi wa hospital ya mkoa dodoma Dr.kyeche amesema marehem amepata tatizo LA brain concasion baada ya kupigwa na kitu kizito hivyo kusababisha dam kuvilia kwenye ubongo.
Mkuu hebu kua serious hili jambo ni kweli au?
 
sasa si wangetoa press release tu kwa nini kusumbua watu, laana ya CCM kwa JK haitokaa ifutike chama kinatoa machozi kwa kuendekeza hila za JK na Nappe
Gobachev aliiua USSR na anadunda na maisha itakuwa kuliuua li CCM!
 
CCM wanapitia kipindi kigumu sana,maana hakuna mwenye ujasiri wa kumshambulia Lowasa kwa sasa maana wanajua jamaa yuko nje ya chama kwahiyo anaweza kusema lolote kwasasa. Sio @Nape wala makonda anaeweza kufungua domo na kuropoka kama awali, mwenyekiti wao ndio kabisa kitu kinagonga chu.pi. Sasa hivi ndio uadui umedhihirika kati Lowasa na JK, na kwenye Press Lowasa wala hakutoa shukrani kwa mwenyekiti wa chama alichotoka.

Wameyataka wenyewe, acha wakione chamoto.
 
Last edited by a moderator:
Inabidi jamaa nayeye tumwalike ajiunge na kundi kubwa la Safari ya matumaini maana hata yeye inaelekea ameichoka CCM ndomaana kathubutu hata kutimua mbio........ huenda anakwenda kuchukua kadi ya CDM
 
Mrema na Dr Slaa waliondoka CCM mwaka 1995 ilikuwa ni miaka mitatu baada ya siasa ya vyama vingi kuanza. Television zilikuwa mbili tu; ITV na TVZ redio zilikuwa tatu tu. Leo ni miaka ishirini badae, kuna vituo vingi vya TV, Radio na mitandao ya kijamii, watanzania wa sasa wanaelimu na exposure kubwa. Na kipindi hicho Nyerere alikuwa hai na alikuwa ana aminiwa na wa tz. Leo miaka 20 baadae huwezi kufananisha impact ya kujiondoa CCM kwa Mrema na Dr Slaa na IMPACT ya Lowassa kujiondoa CCM.
 
Sasa mbwembwe zilikuwa za nini kumbe mkutano wenyewe ulikuwa wa kakatibu ka mkoa, aha acheni hizo na muwe wakweli, hapa hakuna visingizio kwani siasa ni ushabiki, bila ushabiki hakuna siasa. Siasa ni uchaguzi pasipo ushabiki hakuna uchaguzi.

Kwenye red: Mi siko huko unakofiriki, nimeandika kile kilichotokea.
 
hawana jipya ccm maana kikubwa kilicho wapeleka pale ni kusema juu ya Kamanda Lowasa kuamia mjengoni hawana lolote CCM ha ha ha ha ha haaaaaaa! nasikia raha sana
 
Mkuu usiandike kishabiki, walisema wanamkutano na Waandishi wa habari hakuna sehemu waliyosema watamjibu Lowassa. Hicho walichoongea ndio kilichopangwa, usiwaze kushabiki twende haki tu kwa hoja, mimi nilikuwepo hapo.

Kwa hiyo wamewaita ili kuwashukuru
 
Lowassa ni Heavy Weight Politician, Master. Sikilizieni bado kitambo kidogo tu watu wataona mziki, maana sasa amekutana na vichwa vikali vya upinzani, timu imekamilika. Mikakati itakayosukwa hapo, sioni uwezekano wa CCM kushinda uchaguzi wa mwaka huu.

Tusubiri tuone.
 
kuweweseka nako ameshindwa huyu sio mda atatangaza kuhamia chadema
:laser::bathbaby:
 
Mkuu usiandike kishabiki, walisema wanamkutano na Waandishi wa habari hakuna sehemu waliyosema watamjibu Lowassa. Hicho walichoongea ndio kilichopangwa, usiwaze kushabiki twende haki tu kwa hoja, mimi nilikuwepo hapo.

Kwi kwi Kwi Kwi kwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom