Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe na Wenzake leo 20/01/2022. Shahidi 10 amaliza, shahidi wa 11 mwingine kuanza ushahidi kesho 21/01/2022

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 20/01/2022 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea.

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

Kujua kesi ilipoishia soma:
Jaji ameingia Mahakamani

- Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili wa Serikali
  • Pius Hilla
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Tulimanywa Majige
  • Ignasi Mwinuka
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili
  • Nashon Nkungu
  • Faraji Mangula
  • Fredrick Kihwelo
  • Seleman Matauka
  • Maria Mushi
  • Khadija Aron
  • Alex Massaba
- Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tupo tayari Kuendelea

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea Jaji Shahidi Nakukumbusha Bado upo Chini ya Kiapo.

Wakili wa Serikali: Jana Uliulizwa Kama Ulidukua Taarifa za Mtu Mwingine, Ukasema Jibu haiwezi Kuwa Ndiyo au Hapana, Ulikuwa Unamaanisha Nini?

Shahidi: Ukisema Hacking Inategemea Nia ya Yule anaye fanya Kile Kitendo, Kuna Wakati Inaweza Kuwa Nia Ovu au Hapana, Ndiyo Maana Nikasema Inategemea.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali pia Kuhusiana na Zoezi la Extraction, Kama zoezi ulilofanya Ungeweza Kubaini namba Ya Mtu anaitwa Bwire, Ukasema huwezi, Fafanua.

Shahidi: Katika Extraction tunafanya Zoezi la Identification la ICCID namba, na Ilikuja Ni namba gani lazima Urudi Kwa Mtoa huduma, ndiye atathibitisha ni Namba gani

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Pia Kuhusiana na Wakati Wa Kufanya Uchunguzi, Kama Kifaa kikiwa Kina Kina Internet Connection, Inaweza Kisababisha Kifaa Kuingiliwa, Ukasema Siyo Kila Wakati ila ni wakati fulani fulani.

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Wakili alikuwa ananiuliza Kifaa Cha Maabara Ndiyo Maana Nikasema Kama Kitaunganishwa Kina weza.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kama Kifaa Cha Maabara Wakati Wa Uchunguzi Hakitakiwi Kuwa na Internet Connection, Kinatakiwa Kuwa Off, Waka uliza Kama Kinaweza Kuwa Connected na Infrared au Bluetooth.

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Hayo ni Mambo tunazingatia Maabara Kwamba Wakati wa zoezi Tuna hakikisha Hakuna Connection either ya Bluetooth au Infrared.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusu zoezi la Analysis Ukasema Wakili Kakunukuu Vibaya Ulikuwa Unamaanisha nini Shahidi: Wakati wa zoezi la Analysis Una tafuta Content ulizopewa against zile content Zote, Ndiyo analysis.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Pia akama Kwa Uchunguzi Uliofanya kama Ukiweza Kubaini Majina ya Mmoja baada Ya Mwingine, Kama Wana husika na Ugaidi Ukasema Mpelelezi Ndiyo anaweza Kubaini hilo.

Shahidi: Role Yangu Kama Mchunguzi, Ni Kumpa Mpelelezi Yale aliyo yaomba, Mimi kama Mchunguzi sihusiki Kabila na Hilo.

Wakili wa Serikali: Ulikuwa Unaulizwa Kuhusiana na Data ambazo Ulizo Access Katika zile Simu, Kama Ukiweza Kupata Simu za Kuongea Ukasema Wewe Ulicho access ni Call Logs

Shahidi: Wakati Watu wawili Wanaongea Kwenye Mawasiliano Kuna Mtu anaunganisha hapo, ambaye ni Mtoa Huduma, Mimi siwezi.

Mangula: OBJECTION Mheshimiwa Jaji, jana Wakati namuuliza Shahidi alisema Hawezi Kuzungumza Kuhusu Sauti, alisema hawezi Kuzungumza Sababu za Kiusalama, Naomba Jibu liondolewe au tupate nafasi ya kumuuliza tena.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kuna tatizo hapa, Hili swali aliulizwa Nashon Nkungu, Ambapo Shahidi alisema Haku access Sauti Bali Call Logs na Hata Jibu aliokuwa anatoa

Jaji: Kwamba kwanini Haku access sauti?

Mangula: Mhe Jaji Wakati natoa OBJECTION Sikutaja Swali lilikuwa na Nani

Jaji: Hayo hakuyatoa, isipokuwa nasema anayatoa haya kwenye ufafanuzi, Je ni sawa?

Mangula: Siyo sawa, Ndiyo hoja yetu ipo hapo

Jaji: Suala la Sauti lipo kwa Services Provider Hayakutolewa Jana, Ndiyo Maana anataka Jibu liondolewe.

Wakili wa Serikali: Inspector Ndowo Kila Ulipo Ulizwa Kuhusu Kufanya Extraction Ya Sauti, Na Ulisema Hamku Access, Bali wewe Ulifanya Ku access Call Logs.

Shahidi: Kwa sababu Mnapo wasiliana, Kinacho Bali katika Vifaa Vyao ni Call Logs, Kwa Maana Tarehe Fulani Siku fulani Mtu Fulani alipiga Simu Kwa Mfu fulani

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia kama Wakati Unafanya Extraction, Kama Hivyo Vifaa Uliyotumia Vinaweza Kubaini Simu ni Original au Feki.

Shahidi: Kazi ya Mtambo Ule siyo Kubaini Simu ni Feki au Original, Bali ni Ku Extract Kilichopo ndani ya Simu

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali pia Kuhusiana na Vitu Viwili Pia Kuhusu DECORDING na Analysis ya Data.

Shahidi: Ni Vitu Viwili Tofauti, DECORDING ni Wakati Wa Mchakato Wa Physical Analyser inapo analyse Data Wakati ili Vitu hivyo viweze Kuonekana Inafanyika DESCRIPTION

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kuhusu Reporting Na Uchunguzi

Shahidi: Reporting ni Automatic Process, Mpangilio unapangwa na Mfumo wenyewe.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Kuhusiana na Kama Kazi ya Physical Analyser Kama kazi yake ni Kupanga Mafaili kwa Logical Sequence, Ukasema Siyo Wakati Wote Inafanya hivyo.

Wakili wa Serikali: Kingine Uliambiwa Kuwa Ulinganifu Wake ni sawa tu Na screen Shots za Kwenye Simu, Ukasema Siyo hivyo

Shahidi: Mfumo Umetengenezwa katika Namba ya Kupata Taarifa Kama Imefutwa au Ipo, Katika Kile Kifaa, Tofauti na Screen Shots Hauwezi Kuona Kama Taarifa Imefutwa

Wakili wa Serikali: Ulizwa Maswali Kuhusiana na Vielelezo Katika Extraction Riport, Hasa Kielelezo namba 24,25,26 na 27 kuhusu Cable zilizotumika, Ukasema Cable namba 100 ilitumika Katika Kielelezo 24,na 26 Kwingine Ukasema haionekani.

Shahidi: Taarifa Kuhusiana na Identification Katika hivyo Vifaa Inategemea na.......

Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Hayo sio tu Majibu Mapya, Hata tulipo Muuliza Hakusema

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Naona tupo Sahihi.

Jaji: Swali halijapingwa, Bali Shahidi alicho eleza Leo Jana Hakuyaeleza

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Purpose ya Re Examination ni Kupata Ufafanuzi, Sisi tunaona tupo Sawa

Kibatala: Mheshimiwa Jaji, Msingi wa jibu la Shahidi, alisema alituma Cable ya aina Moja, Bila Kujua inapelekwa Wapi, Na baadae tukaenda kwa Moja Moja Aendelee kama Sisi tutapewa nafasi Ya Kuuliza Maswali zaidi, na Kwa Nini aendelee Wakati Sheria inakataza?

Jaji: anasema Kwamba Kwa Mtazamo wake Na wao Waje Wapate nafasi ya Kuuliza

Wakili wa Serikali: Ni sawa Mheshimiwa Jaji

- Mawakili wa Serikali Wanakutana na Kujadiliana Kama Kikundi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji nimewasiliana na Wenzangu tunaomba tuliache hilo Swali

Wakili wa Serikali: Shahidi Uliulizwa hapa Kama Unachunguza Tuhuma Za Jinai, Ukasema Wewe Unachaguza Vifaa Vilivyohusishwa na Jinai, Maana yake nini

Shahidi: Sisi Kazi Yetu ni Kutoa Taarifa Kwa Wapelelezi Ambao wa naleta Kazi za Uchunguzi Forensic Beaural, Kwa hiyo Sisi Mwisho Wa Kazi yetu ni Kutoa Taarifa akama Vile ambavyo Wameomba.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Pia ni Lini haswa, Vile Vielelezo Vilirudishwa Kwa DCI Ukasema Vilikuja Kuchukuliwa Tarehe 10 July 2021 wakati Wakili Pius Hilla anakuongoza Ulisema Tarehe 06 August 2021, Unasemaje kuhusu hiyo Tofauti.

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Naomba Mahakama Yako ichukue Tarehe 10 July 2021

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Pia Swali Katika Kielelezo namba 26, Kulikuwa na Maneno Kama Down Graded, Ukasema haimaanishi hivyo kama alivyosema.

Shahidi: Features zote ni Automated Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Maswali Kuhusiana na Kielelezo namba 27 kama aina simu ilitajwa Katika Kielelezo hicho kama Katika Vielelezo Vingine, Hebu Ifafanulie Mahakama.

Shahidi: Mazingira kama hayo yanatokea Pale ambapo Property ya a Kifaa Husika Haipo Katika Kifaa Husika, Tunatumia Chipset.

Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Jaji hiyo ni Fact Mpya, Concept anayojemga Sasa hivi Hakuulizwa Swali, Ali Volunteer yeye Mwenyewe, Mimi nikasema Jibu lako limetoka Kwa Mungu, Re:examination purposes yake ni Kufikia Mashimo ya Maswali, Siyo Kwa Kitu ambacho hakuulizwa

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji OBJECTION Yake haina Mashiko, Kwanza ana admits kabisa kama lilijitokeza, Kwanza Jana alikuwa Shahidi akitaka Ufafanuzi anasema Mimi sitaki Ufafanuzi, Swali letu lipo Kutaka Kupata Majibu.

Jaji: Suala la Kwamba aliulizwa au Ali Volunteer siyo Sahihi, process ilikuwa ni Cross examination Suala ni Information inayo letwa Haiku letwa hapo awali

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Ngoja Niulize Kwa tofauti.

Wakili wa Serikali: Shahidi Kwamba Kuna Simu Haijatajwa, Elezea hapo Kwa Kuji Confine

Shahidi: Kwa sababu ilitumika kwa Chipset

Kibatala: Kinachofanyika ni Kile Kile tu Kwa Njia Mpya

Nashon Nkungu: Mhe Jaji Kwa Kugundua Kuwa Suala la Chipset au Simu Card halikuingia Mahakamani, wanataka Kuingiza Ushahidi Mpya Kwa Njia ya Nyuma, Naungana na Kaka Yangu Kibatala

Jaji: Swali nafikiri halina Shida Wao wanasema Katika Majibu ni Ushahidi Mpya, Je Nyie Mnasemaje.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba niliondoe hilo Swali

Wakili wa Serikali: Shahidi Uliulizwa Maswali Kuhusiana na Service Provider, Ukasema ni TTCL Ukaulizwa Kama anaweza Kuwa access Data Ukasema si Kweli, Ni Kwanini Ulisema hivyo.

Shahidi: Mhe Jaji Ni kweli TTCL Anatupa internet ila Control ya Data ni wenyewe

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kuhusiana na Kielelezo namba P35 ambapo Uliandika Kielelezo namba H, ambapo Juu imeandikwa "IMEI namba Imefutwa" Ukaulizwa Kama Kwenye Riport yako Uliandika, Ukasema hukuandika.

Shahidi: Kwa sababu celebrite ina Access na Ku Extract IMEI namba

Wakili Kibatala: It's a New Fact, Hakuna Mahala Popote ambapo alisema Kuwa Celebrite Ina Extract IMEI namba.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji OBJECTION Yake haina Mashiko, Kwa sababu Shahidi ameshasema kuwa Taarifa ni Automatic generated

Jaji: Nakumbuka Alisema Kuwa Taarifa za IMEI namba inaweza Kuonekana Kwa Ile iliyopo Wazi au ambayo ipo Ndani, alisema Barua Ilikuwa Na IMEI namba.

Kibatala: Kuhusu Barua Hakuna Tatizo, Lakini Kwamba Celebrite Kuwa Inaweza Kutoa kama End Product kuwa ni IMEI.

Jaji: alisema Kuwa IMEI namba inaweza Kupatikana ndani ya Simu

Kibatala: Hilo Kweli alisema ila tunapinga Kuwa Ali Extract Kwa kutumia Celebrite Mashine, Hilo tunapinga.

Wakili wa Serikali: Shahidi aliulizwa Kama Kwenye Riport alisema, akasema Hakusema, Sisi tunataka Kujua kwanini Hakusema Kwenye report

Jaji: Sasa Jibu lake lilikuwa Lina Jibu swali

Wakili wa Serikali: Naomba Kurudia Swali.

Wakili wa Serikali: Kwanini Hukuandika suala la IMEI namba

Shahidi: Nilipata Kwa ndani

Kibatala: Anajibu Kitu Kilekile

Jaji: Nafikiri Shahidi Ajibu swali, Kwanini Katika Report Yako hujaandika suala la IMEI namba?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Katika Uchunguzi Wangu IMEI namba huwa naiona.

Wakili wa Serikali: Shahidi Uliulizwa Swali Kuhusiana na Ile Barua Iliyo andikwa Kwenda Kampuni ya Tigo, Kuwa haina Sahihi yako, Ukasema ni Kweli Signature yako haionekani, Je ni Kwanini Shahidi: Ni Utaratibu Wa Ofisi kwa Cheo Changu siwezi Kusaini Barua zinazo enda Nje ya Ofisi

Jaji: Nakumbuka Kuwa yeye alisema Kuwa Hakusaini Kwa Sababu Yeye Siyo Ofisa Mwenye Mamlaka Ya kusaini

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba kukomea Hapa, Sina Swali Lingine la Ziada

Jaji: Shahidi tunakushukuru Kwa Ushahidi Wako Unaweza Kwenda Sasa

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji baada ya zoezi hilo, Hakuna shahidi mwingine Kwa Leo, Tunaomba hairisho mpaka kesho Tarehe 21 January 2022 ilituweze kuendelea na shahidi mwingine Sababu Shahidi ambaye tulimtegemea angefika Jana, hakufika, Ile Jioni tulivyotoka hapa tulilazimika kuita shahidi mwingine, hivi leo atafika, tutafanya maandalizi tuweze kesho kuendelea.

Shahidi tuliye mtegemea Jana si mkazi wa Dar es Salaam na shahidi ambaye anakuja leo Si mkazi wa Dar es Salaam, Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji kama ambavyo tulielekezwa na mahakama jana, Sisi tupo na tupo tayari, kama tungejua mapema tungeweza kufanya mambo mengine.. Naikumbusha Mahakama kuhusu Amri yake ya jana na Juzi. Kuhusu kukosekana na shahidi l, Ni DETRIMENTAL Kwetu.

Nammukuu Dr. Rugemeleza Nshala "Siku za mwanadamu huwezi kuzifidia zikipita" Sisi tumekuwa waaminifu kwa Mahakama, pamoja na changamoto nyingiiiiiii.. Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji

- Jaji anaandika kidogo

- Mahakama ipo Kimyaaaa


Jaji: ni kweli kwamba Mahakama hii kwa Amri Ilitoa siku mbili ilieekeza Jamhuri Kuwa walete Shahidi, kwa Jana ukweli hapakuwa na muda kwa namna shahidi alikuwa anatoa ushahidi Wake ilichukua muda mwingi wa jana lakini ilitegemewa leo ushahidi wake ungemalizika mapema na kuendelea na shahidi mwingine Upande wa mashtaka wamekuja na Sababu kuwa shahidi amekuwa nje ya Dar es Salaam Upande wa Utetezi nimesikiliza concern zao.

Kwa sababu hiyo naagiza upande wa mashtaka kesho walete shahidi tuweze kuendelea na kama Shahidi huyo mnaye muita atakuwa na dharula basi mfanye Utaratibu mapema kuita shahidi mwingine.

Kwa maana hiyo nahairisha shauri mpaka kesho , Washtakiwa wataendelea kuwa Rumande chini ya magereza mpaka kesho asubuhi Saa 3 kamili Asubuhi.

- Jaji anatoka
 
Pamoja sana Mkuu; mnapiga kazi iliyotukuka sana kwa hakika; kazi mnayofanya ya kujitolea kutupasha habari za "kesi hii kubwa" kuwahi kutokea katika nchi yetu, kesi ambayo vyombo vyote vya chama na serikali vimepigwa ganzi havitaki hata kuuhabarisha umma, Mungu atawalipa.
 
... pamoja sana Mkuu; mnapiga kazi iliyotukuka sana kwa hakika; kazi mnayofanya ya kujitolea kutupasha habari za "kesi hii kubwa" kuwahi kutokea katika nchi yetu, kesi ambayo vyombo vyote vya chama na serikali vimepigwa ganzi havitaki hata kuuhabarisha umma, Mungu atawalipa.
Twende pamoja hapa ndugu
 
Nasubiria Re-examination ya ulimaanisha Nini kusema,hukuona kosa la jinai au Ugaidi kwa kuwa wewe ni Polisi?
Wakiuliza mtanikuta makao makuu pale Ilala napata maji baridiii
 
AIgmal.jpg
 
...Reexamination ya leo imekuwa fupi sana; nilitegemea mawakili wa serikali wangetaka ufafanuzi kutoka kwa shahidi kwenye yale maeneo "aliyoonekana ku-support" upande wa utetezi lakini wapi! Kwa mfano, nilitegemea maswali kama;
  • ulimaanisha nini uliposema hukuona neno Sabaya kwenye extraction? (Sikusikia hilo swali).
  • jana nilikusikia ukisema hukuona mipango ya vitendo vya ugaidi kwenye extraction yako; ulimaanisha nini wakati kesi hii ni ya ugaidi? (Sikusikia hilo swali).
  • jana ulisema wewe ni askari polisi na kama ungeona mipango ya vitendo vya uhalifu ungeandika kwenye ripoti yako; mweleze mheshimiwa jaji ulimaanisha nini; (Sikusikia hilo swali)..
Hizo ni kati ya hoja za msingi zinazobeba shauri zima la uhalifu/ugaidi wa Mbowe na wenzake; badala ya kutaka ufafanuzi wa kina wanauliza maswali ya kijinga na kuomba shauri liahirishwe hadi kesho kwani leo hawana shahidi mwingine! Ok, waendelee kutafuna pa diemu fedha za serikali hazina mwenyewe.
 
Nasubiria Re-examination ya ulimaanisha Nini kusema,hukuona kosa la jinai au Ugaidi kwa kuwa wewe ni Polisi?
Wakiuliza mtanikuta makao makuu pale Ilala napata maji baridiii
... wamekwepa hayo maswali Mkuu!
 
...Reexamination ya leo imekuwa fupi sana; nilitegemea mawakili wa serikali wangetaka ufafanunuzi kutoka kwa shahidi kwenye yale maeneo "aliyoonekana ku-support" upande wa utetezi lakini wapi! Kwa mfano, nilitegemea maswali kama...
Kweli naona imekuwa kwa ufupi sana seems kama hawakujipanga vyema.
 
Back
Top Bottom