Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Detective Afande Goodluck atoa Ushahidi, Kesi yaahirishwa hadi Novemba 24, 2021

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Leo tarehe 23/11/2021 kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe inaendelea baada ya kuahirishwa siku siku ya Jumatatu, tarehe 22 Novemba, 2021.

Kujua kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Novemba 22, 2021. Mahakama yatupilia mbali hoja tatu za utetezi. Kesi imeahirishwa hadi Novemba 23, 2021

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

=========

UPDATES:

JAJI AMEINGIA MAHAKAMANI

Jaji ameshaingia Mahakamani

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021, Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa

Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha Jopo lake
Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Esther Martin
Nassoro Katuga
Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi
Jeremiah Mtobesya
John Mallya
Fredrick Kihwelo
Seleman Matauka
Idd Msawanga
KHadija Aron
Maria Mushi

Jaji anaita Majina ya Washtakiwa wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: tuna shahidi Mmoja na tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Na sisi pia tupo tayari

Jaji: Enhe

Wakili wa Serikali: Shahidi ameenda Kuitwa

Shahidi anaingia

Jaji: Jina

Shahidi: 4347 Detective Afande Goodluck

Jaji: Miaka 32

Jaji: kabila

Shahidi: Mchagga

Jaji: Dini

Shahidi: Mkristo

Shahidi: Naapa kwamba Mimi H4347 Detective Sargent Goodluck Naapa kwamba Ushahidi Nitakao toa ni kweli, kweli tupu Eeh Mungu Nisaidie

Wakili wa Serikali: Pius Hilla Shahidi Unaitwa nani

Shahidi: Naitwa H4347 sergeant Goodluck

Wakili wa Serikali: Kazi yako

Shahidi: Askari Polisi

Wakili wa Serikali: Umeajiliwa tangu lini

Shahidi: 2013 Wakili wa Serikali Kituo chako cha Kazi ni wapi

Shahidi: Central Arusha

Wakili wa Serikali: Shahidi ieleze Mahakama Mnamo tarehe 04 August 2020 ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikuwa Kazi I Maeneo ya Central Police, Arusha

WS: Majira ya Jioni Siku hiyo Kitu gani Kilitokea

Shahidi: Afande Wangu Inspector Mahita alinipigia Simu na Kuniita Ofisini kwake

Wakili wa Serikali: Afande Mahita ni nani sasa hivi

Shahidi: Msaidizi Wa Mkuu wa Upelelezi

Wakili wa Serikali: Wa Wilaya gani

Shahidi: Arusha Mjini

Wakili wa Serikali: alikueleza Jambo gani

Shahidi: Aliniambia kuwa Mimi na Afande Francis tunahitajika kwa Afande RCO

WS: Wakati huo nani alikuwa RCO wa Arusha

Shahidi: alikuwa Afande Ramadhan Kingai

WS: Kwa Kingai Kitu gani kilitokea

Shahidi: Tulipofika kwa Kingai alituambia Kwamba tujiandae Kwa Safari Kuna kazi ya kwenda Kufanya

WS: Safari ya Kuelekea wapi

Shahidi: Wakati ule hakutuambia zaidi ya Tujiandae kwa Safari

WS: Ulijiandaaje Shahidi Baada ya Kutupa Maelekezo akatuambia tukachukue Silaha

WS: Baada ya hapo Nini Kilifanyika na Mkaelekea Wapi

Shahidi: Tulikuwa Afande RCO, Inspector Mahita, Mimi na Dereva wa RCO na Coplo Francis

WS: Taratibu Shahidi Jaji aweze Kuandika

Shahidi: Baada ya hapo tukaambiwa twende Arumeru Tukampitie Afande Jumanne ambaye ni OC CID wa Wilaya ya Arumeru

WS: Huko USA River Kwa Afande Jumanne Kitu gani Kilifanyika

Shahidi: Tulifika pale, tuka ingia ndani wote na Afande Kingai Akatupa Briefing Ya kazi tunayo kwenda Kufanya

WS: alisema Kitu gani

Shahidi: Akisema Kwamba amepata Taarifa Kwamba Kuna Kikundi KinajiPanga Kufanya Matendo ya Kigaidi hapa Nchini, na Kwamba ni Maeneo ya Arusha Kilimanjaro, Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya.

WS: akiwataka Kwenda Kufanya kazi gani

Shahidi: Katika Briefing Alisema Kuwa Kikundi hicho Kina watu ambao wapo Mkoa wa Kilimanjaro, Moshi kwa hiyo Tunatakiwa kwenda Kuwakamata Kuzuia wasiendelee na Matendo yao

WS: Kwa hiyo Mlikuwa mnakwemda wapi

Shahidi: Tulikuwa tunakwenda Moshi

WS: Ukamataji Ukifanyika lini

Shahidi: Ukamataji Ulifanyika Tarehe 05 August 2020

WS: Ulifanyikia Eneo gani na Majira gani

Shahidi: Eneo la Rau Madukani na Majira Ya Saa Saba Mchana

WS: Rau Madukani Ipo Mji gani

Shahidi: Rau Madukani Ipo Moshi

WS: Kwa Mujibu wa Taarifa za Kingai Mlikuwa mnakwemda Kuwakamata watu wangapi Waliokwepo Moshi

Shahidi: Kwa Mujibu wa Taarifa Za Afande Kingai Alisema Watu waliofika Moshi ambao tunakwenda Kuwakamata ni watano

WS: Mliofanikiwa Kuwakamata hiyo Tarehe 05 August 2020 ni akina nani

Shahidi: NI Mohammed Ling'wenya na Adam Kasekwa

WS: Ieleze Mahakama Iwapo Watu Mliwakamata hiyo Tarehe 05 August 2020 Kama wapo Mahakamani na Kama unawakumbuka

Shahidi: Wapo Mahakamani Wamekaa Upande wa Kulia

Wakili wa Serikali: Upande wa Kulia Wamekaa watu wengi

Shahidi: Ni Mtu wa Pili

Shahidi: anawafuata Walipo na Kuanza na Mohammed Ling'wenya na Adam Kasekwa

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi ameweza Kuwatambua Washitakiwa wa Pili na watatu

Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Naona hii inajirudia Mara ya tatu Sasa, Mwenye Uwezo wa Kujua Kama Shahidi ametambua Washtakiwa ni kazi ya Mahakama

Jaji: ni Sahihi Na Mimi napokea Ushahidi tu

Wakili wa Serikali: Baada ya Ukamataji, Mlielekea Wapi

Shahidi: Central Moshi

WS: Baada ya Kuwa Mmefika Kituoni Mambo gani Yalifanyika Shahidi Afande Jumanne na Afande Mahita Waliekezwa Kushuka Kwenye gari, Mimi Afande Kingai na Dereva Tulikaa Kwenye gari

WS: Kwanini Mlibaki Kwenye Gari

Shahidi: Tulikuwa na Lengo la Kwenda Kumtafuta Mtuhumiwa Wa Tatu

Wakili wa Serikali: Kwenda Kumtafuta Mtuhumiwa Wa Tatu wapi Shahidi

Shahidi: Maeneo Mbalimbali ambayo watuhumiwa Walikuwa wanatupitisha

Wakili wa Serikali: Huyu Mtuhumiwa Watatu ulipata Kujua ni Yupi

Shahidi: Nilipata Kumfahamu kwa Majina ya Kakobe au Moses Lijenje

WS: Ufutailiaji Wa huyu Kakobe au Moses Lijenje Ulianza Muda gani

Shahidi: Baada ya Kutoka Central Polis Moshi Tulienda Kumtafuta Moses Lijenje

WS: Mlipotoka Central Mlienda Maeneo gani

Shahidi: Tulipofika Central Tulienda Maeneo ya RAU Madukani

WS: Tofauti na Rau Mlikwenda Maeneo yapi Mengine

Shahidi: tulienda Majengo, Pasua, Aishi Na Boma

WS: Aishi Ipo wapi

Shahidi: Machame

WS: Boma Ipo wapi

Shahidi: Wilaya ya Hai

WS: Utafutaji wa Mtuhumiwa Uliendelea Mpaka Saa ngapi

Shahidi: Tulienda Mpaka Majira ya Saa Tano Usiku

WS: Matokeo ya Utafutaji wenu Ukoje

Shahidi: Hatukufanikiwa Kumkamata

WS: Baada ya Hapo

Shahidi: Tulitoka Boma Ng'ombe Tukarudi Moshi na Kwa Maelekezo Ya Afande Kingai Kwamba Watuhumiwa Wawekwe Lockup

WS: Baada ya Kufika Moshi Nini Kilifuata

Shahidi: Afande Kingai alisema amepokea Maelekezo Kwamba Tuwapeleke Watuhumiwa Dar es Salaam

WS: Ni Saa ngapi Mlianza Safari ya Kuelekea Dar es Salaam

Shahidi: Tulitoka Majira ya Saa Moja Jioni Kuanza Kuelekea Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Mnakumbuka Sasa Dar es Salaam Mlifika Lini na Majira ya Saa ngapi

Shahidi: Tulifika Alfajiri ya Tarehe 07 August 2020

Wakili wa Serikali: Dar es Salaam Mlifika wapi

Shahidi: Tulifikia Kituo Cha Polisi Central Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Mlipofika Central Mlielekea Maneno gani haswa

Shahidi: Tukielekea Sehemu ya Mapokezi, Charge Room (CRO)

Wakili wa Serikali: Kwa Madhumuni gani?

Shahidi: Ya Kuwakabidhi Watuhumiwa Wawekwe Lockup

WS: Kwa hiyo ni Kitu gani Kilifanyika hapo CRO

Shahidi: Afande Kingai na Afande Jumanne Waliwakabidhi Watuhumiwa

WS: baada Kuwakabidhi hawa Watuhumiwa Mlielekea wapi na Kitu gani kilifanyika

Shahidi: Afande Kingai alitoa Maelezo, to take Break, Tukanawe uso alafu turudi

WS: Mnakumbuka ni Majira ya Saa ngapi mlirejea Kituoni Shahidi Tulirejea kituoni Majira ya Saa 1 Asubuhi

WS: baada ya Kurudi Kituoni nini Kilifuata

Shahidi: Nilimkabidhi Vielelezo nilivyokuwa navyo, na Afande Kingai akasema kuna Taarifa amepata Juu ya Watuhumiwa wengine Walikuwa DSM Wamepatikana, akataka tukaendelee na Upelelezi wakati akiwaandika Maelezo.

WS: Wakati wote Kuanzia Tarehe 05 Mpaka Tarehe 06, Mpaka Mnaanza Safari, Watuhumiwa walikuwa Chini ya Uangalizi wa nani

Shahidi: Walikuwa Chini ya Uangalizi Wa Afande Mahita pamoja na Mim

WS: Ikumbushe Mahakama Watu Mnazunguka Kuanzia, Moshi, Arusha Mpka Dar es Salaam Watuhumiwa walikuwa na Hali gani

Shahidi: Watuhumiwa Walikuwa na Hali Nzuri Wakati wote

WS: Ieleze Mahakama Kwamba Tarehe 5 kwakuwa Mlikuwa Mnazunguka Na Watuhumiwa wakati wote, Je Mlikuwa wapi

Mallya: OBJECTION, Leading Question Hakuna Sehemu Yoyote katika Testimony Yake Shahidi alisema Walikula

Jaji: badilisha hilo swali

WS: Baada ya Tarehe 07 Wewe Ulielekea Wapi

Shahidi: Nilikwenda Kutafuta Taarifa Kama tukivyoelekezwa na Afande Kingai Kukamata Watuhumiwa Wengine

WS: Shahidi Sasa Washitakiwa Wapo Central na hiyo Tarehe Saba Unasema Mlienda Kutafuta Taarifa zingine, Je ni lini tena ulipata Kushughulika na Watuhumiwa tena

Shahidi: Tarehe 08 August 2020 baada ya Afande Kingai Kusema amepata na Maelekezo tuwapeleke Watuhumiwa Kutoka Central Kwenda Mbweni, Na tuliwahamisha

WS: Wakati Mnawahamisha kutoka Central kwenda Mbweni, Je washitakiwa Walikuwa na Hali gani

Shahidi: Washtakiwa wote walikuwa na Hali nzuri

WS: Unakumbuka ilikuwa saa ngapi

Shahidi: Majira ya saa mne asubuhi

Shahidi: Tukiwakabidhi, Wakaimgizwa Lockup na Baada ya hapo tuliondoka

WS: Na Kurudishashwa Nyuma, Elezea Mazingira ya Ukamataji yalikuwaje

Shahidi: Yalikuwa ni Salama Hapakuwa na Purukushani, Mazingira yalikuwa ni Salama

WS: Eneo la Rau ni Eneo la namna gani

Shahidi: Eneo la wazi ambalo lina watu wanafanya Biashara zao Shahidi Tulipofika eneo la Boma, Gari ilisimama, Afande Kingai alishuka na akarudi na Chakula akiwa na Mtu amebeba, Ndizi na Nyama tukala na Watuhumiwa na Vinywaji tukawapa

Shahidi: Tulipofika Njia panda Himo Gari Ilipata hitilafu ya Umeme, Afande Kingai akaomba Gari kwa RPC wa Kilimanjaro, Wakati tunasubiria Gari tukala Chakula na baada ya muda Gari Iiifika na Kuanza Safari

Wakili wa Serikali: Pale Njia panda Himo Mlikula Chakula watu gani

Shahidi: Tulikula watu wote Pamoja na Watuhumiwa

WS: yapo Malalamiko Hapa Mahakamani, Kwamba Baada ya kuwakamata Watuhumiwa Pale Moshi Siku ya Tarehe 05, Mliwapeleka kituoni na Kuanza kuwatesa na wewe Ulishiriki Shahidi anahamaki hapa anasema SIYO KWELI

Shahidi: Tulipofika Kituoni Pale Moshi Sisi Hatukushuka kwenye gari

WS: TARATIBU SHAHIDI

JAJI ANAANDIKA

Shahidi: Baada Ya Kufika Kituoni Watuhumiwa Hawakushuka kwenye gari na baada ya Mizunguko yote ile tulirudi Saa 5 Usiku kuwarudisha na baada ya hapo tuliwafuata kesho yake

WS: Yapo Malalamiko Pia kwamba washtakiwa Hakuwafikisha Central Police Dar es Salaam na Kwamba Tarehe 09 wewe ukiwa na Bastola ulimlazimisha Kwa kumshikia Bastola, na Kwamba Asipo Saini yake Mateso ya Moshi yatajirudia rudia

Shahidi: Siyo Kweli Kwamba hatukuwa fikisha Central Polisi Dar es Salaam, hiyo Tarehe 09 Sisi Tulipofika Pale Central Tuliambiwa kwamba tuendelee Kuwatafuta watuhumiwa wengine na Siku hiyo zoezi lilizaaa Matunda Baada ya kumkamata Khalfani Bwire.

Shahidi: na hata kule Moshi hatukuwatesa kabisa

WS: TARATIBU SHAHIDI TWENDE KWA VITUO JAJI AWEZE KUANDIKA

Shahidi: Baada ya Kumkosa Moses Lijenje tulielekea Dar es Salaam, Hakuna Mahali Watuhumiwa Waliteswa

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo kwa Hapa Dar es Salaam Watuhumiwa Mliowakamata Moshi Mliwapeleka Vituo vipi

Shahidi: Siku ya Tarehe 08 Mimi na Inspector Mahita Ndiyo tuliwapeleka Watuhumiwa Mbweni na baada ya Kukabidhi tuliondoka.

WS: Shahidi Umeeleza Vyema Washtakiwa kutokuteswa, Vipi hili la Kumtishia Mohammed Ling'wenya Kusaini na Kwamba Asiposaini Mateso yatajirudia

Shahidi: Si kweli Kwa sababu Baada ya Kuwakabidhi Kituo cha Polisi Mbweni Hatukurudi Tena.. Na Moshi....

WS: SUBIRI KWANZA

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kwa Leo Niishie Hapo

Mtobesya anamfuata Shahidi Mahala alipo

Mtobesya: Unafahamu Kitu kinaitwa Occurance Book

Shahidi: Ndiyo nakifahamu

Mtobesya: Mueleze Mheshimiwa Jaji ni Kitu gani

Shahidi: Ni Kitabu cha Mahudhurio ya Askari akiwa kazini

Mtobesya: Wakati Unaongozwa na WS, Ulitoa Occurance Book?

Shahidi: Sikutoa

Mtobesya: Hebu tuambie Kituo cha Polisi Central Moshi Ni kituo kilichokamilika Kumuwezesha Askari Kufanya kazi yake..?

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Mtobesya: Kuna Karatasi, pen, Viti na Meza

Mtobesya: Je, Unamfahamu kwamba Kuna Mashahidi Kwenye kesi hii Walichukuliwa Maelezo Yao wakiwa Moshi

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Mtobesya: Kuna Askari ambao Mlikuwa nao Kwenye Timu ambao hawakutoka Moshi

Shahidi: Sahihi

Mtobesya: Nimesikia Mtu anaitwa Swila Je Mlikuwa naye

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Tulikuwa naye, Ni Inspector Wa Polisi Hapa Dar es Salaam

Mtobesya: Tarehe 08 August Swila alikuwa anafanya kazi Kituo gani Cha Polisi

Shahidi: Sifahamu

Mtobesya: hamkumkuta Central Police Dar es Salaam

Shahidi: Hatukumkuta

Mtobesya: Nilisikia Ulimtajia, We ulijuaje anaitwa Swila

Shahidi: Ni Baada ya Afande Kingai Kusema tutaungana Na Inspector Swila huko Dar es Salaam

Mtobesya: Kwa hiyo nikisema Swila anatokea Central Dar es Salaam Utakuwa hufahamu

Shahidi: Mimi sifahamu

Mtobesya: Isaidie Mahakama, Je Unakumbuka Kuwa Uliandika Maelezo Kitu Unachokitolea Ushahidi leo

Shahidi: Nafahamu

Mtobesya: Uliandika lini

Shahidi: Tarehe 10 December 2020

Mtobesya: Uliandika Mwenyewe?

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Ukiyaona Utayafahamu

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba nipewe Maelezo yake halisi

WS Robert Kidando: Hatuna Pingamizi

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba Kumsogelea Shahidi

Jaji: anaandika, Bado Kimya na Mtobesya bado hajamsogelea

Jaji: Kumu' approach kwa namna gani Mahakama:

Mtobesya: Kwa Maana ya Literal Meaning

Mtobesya: Shahidi Unaweza Kuikumbuka

Shahidi: Ndiyo nafahamu ni ya Kwangu

Mtobesya: Naomba Sasa Usome kwa Sauti

WS ABDALLAH CHAVULA: OBJECTION. Mheshimiwa Jaji Hatuelewi, naona Ghafla Shahidi anapewa Statement asome

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji hawa ndiyo walisema Kwamba Shahidi asome kwanza Kisha ndiyo ahojiwe

Jaji: Miye Nakumbuka walisema Kwanza tuwaongoze Mashahidi

Mtobesya: Haya shahidi Ulisema ulikuwa Unazunguka na Watuhumiwa haya tuonyeshe Kwenye Statement Yako ni Wapi Uliandika

Shahidi: Hakuna nilipoandika

Mtobesya: Nilisikia Kwamba Mlipofika Central Polis Moshi Kwamba Mlibaki Kwenye gari, Je ipo Kwenye Statement yako

Shahidi: Haipo

Mtobesya: Nilisikia Kwamba Mlipozunguka Mlirudi Kituoni Saa Tano Usiku Mkawakabidhi CRO. Je hiyo nayo Ipo wapi Katika Statement yako

Shahidi: Haipo

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Baada ya Hapo Naweza Kumkabidhi asome hii Statement yake sasa

Jaji: Mr Kibatala tusaidie kidogo

Kibatala: Mwanzo nakubalina na Mr. Mtobesya Kwamba tulikubaliana asome kwanza lakini Kwa Mood ya Leo tunakubali, Hata hivyo naona sasa ni wakati Muafaka kwa sababu Shahidi ameshaji' contradict

WS Robert Kidando: Hatuna Kipingamizi

Mtobesya: Basi naomba Shahidi Usome Kwa Sauti

Shahidi ASOMA STATEMENT YAKE YOTE, KWA SAUTI

Amemaliza Kusoma Sasa

Mtobesya: Kwakuwa umeyatambua na Kuyasoma Maelezo Yako Je Ungependa yaiingie Kama Sehemu Ya Ushahidi Wako

Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji basi tunaomba Yaingie Kwa Uleule Utaratibu, Exhibit D1

Jaji: Basi tunayapokea Maelezo haya kama Kielelezo namba 1 cha Upande wa Utetezi Mawakili Wote wa Pande zote mbili wanakubaliana na Jaji.

Mtobesya: Tangu Mwaka Jana Mwezi wa 12 Wakati Unatoa Maelezo Yako, Ni Muda gani Umepita

Shahidi: Takribani Mwaka Mmoja

Mtobesya: Kwa hiyo Kwa maelezo Yako uliyoandika Takribani Mwaka Mmoja, Hakuna Sehemu Uliyoandika Kwamba Mlizunguka na Watuhumiwa ni sahihi

Shahidi: NI SAHIHI

Mallya: Nitakuwa Na Maswali Machache Kwa Shahidi, Naomba nipatiwe Exhibit D1

Mallya: Nakuuliza Maswali Machache ila nitataka Ujibu kwa Sauti ileile Uliyo kuwa Unamjibu Kaka Yangu Hilla

Mallya: naomba Uniseomee kwa Sauti, Sehemu hii Mheshimiwa Jaji asikie

Shahidi: "Tuliwa +chukua watuhumiwa hawa na Kuwapeleka Kituo cha Polisi Moshi"

Mallya: Hapo hapo.. Je hayo uliyasema hayo

Shahidi: Nilisema Leo Kwamba tuliopowakosa tukawarudisha Kituoni

Mallya: Kwenye Maelezo Yako Umeandika hayo Maneno

Shahidi: Hapana

Mallya: Ni sahihi Umesema Pale Moshi Kwenye Gari hukushuka

Shahidi: Sahihi

Mallya: Sasa Anza Kusoma Ulipoishia Mwanzo

Shahidi: "aliendelea kuandika Maelezo ya Mashahidi, Mimi Nilikabidhiwa Silaha pamoja na Simu"

Jaji: Mnaniacha hapo

Mallya: Naona Kuna Utofauti na Maelezo na yale yaliyochapwa ambayo tunayo

Jaji: Kwa hiyo tunafanyeje

Mallya: Unaweza Kuondoa hilo Swali

Mallya: Ulihusika Kumtoa Mtuhumiwa Yupi pale Central

Shahidi: Mimi sikuwa toa aliyewatoa ni Afande Jumanne

Mallya: na wewe uliyashuhudia

Shahidi: Hapana Sikushuhudia

Mallya: Kwa hiyo huna uhakika

Shahidi: Mimi nilikuwa naimarisha Ulinzi, lakini aliyewatoa Mahabusu siwajui

Mallya: Maelekezo ya Kuwatoa uliyapokea wewe

Shahidi: Hapana

Mallya: Kwa hiyo Sababu Ya Kuwahisha watuhumiwa kwenda Mbweni hukusikia kwa Masikio yako

Shahidi: Sikusikia

Mallya: Kwa hiyo hujui

Shahidi: Sijui

Mallya: Wakati unasema Mmeitwa na Inspector Mahita kwenda Kwa RCO Ulichukua Silaha, Je ulisema ni silaha gani

Shahidi: Sikusema

Mallya: Kuna Mahali umesema Kwamba Kuna wakati Ulihifadhi Silaha yako sehemu

Shahidi: Hapana Sikusema

Mallya: Unafahamu Gari ya RPC Kilimanjaro lina siti ngapi

Shahidi: Lina Siti 4

Mallya: Wakati Mmeharibikiwa na Gari Njia panda Himo Mlikuwa wangapi

Shahidi: Jumla Watu Saba

Mallya: Gari ya Watu 4 mmepanda Watu 7, nani alimkalia Kingai?

Shahidi: Alikaa Mwenyewe

Mallya: Siti inayofuata

Shahidi: Siti ya Pili ni Kubwa Walikuwa Wamekaa Siti Moja watu 3

Mallya: Ni Gari aina gani hiyo ambayo ina siti 1 ya Kukaa watu 3

Shahidi: FOTON

Mallya: Wakati mnawakamata Muda wa Saa Saba, uliwauliza watuhumiwa Kama Walikula?

Shahidi: Kazi yangu ilikuwa ni Kuimarisha Ulinzi, Sikuuliza

Mallya: Ulipata Kueleza Kama Walienda Msalani Wakati Wakili wa Serikali anakuongoza

Shahidi: Sikueleza, ila ni Huduma za Kibadamu

Mallya: Jibu Swali Langu

Mallya: Wakati Siku ya Tarehe 06 Mpaka Mnapata Breakdown Njia panda Himo, Ulielezea Kwamba walipata Huduma ya Chakula

Shahidi: Sikueleza

Mallya: Ulishawahi Kuajiriwa Kazi ya Polisi Dar es Salaam

Shahidi: Hapana

Mallya: Umezaliwa Wapi

Shahidi: Kilimanjaro, Himo

Mallya: Ni sahihi nikisema Wewe ni Mwenyeji wa Kilimanjaro

Shahidi: huenda ni sahihi

Mallya: Nimeona Ujavaa Saa, Je Kilichokufanya Ujue Uliwakamata Saa Saba ni Kitu gani

Shahidi: Kwenye Gari Kwenye Dashboard Kuna Saa

Mallya: Kwani wale Uliwakamata Ndani ya Gari

Shahidi: Hapana, Kabla ya Kushuka niliona kwenye gari

Shahidi: Ilikuwa Ni Saa Saba Kasoro kabla Sijashuka

Mallya: Kilichokufanya Uangalie Muda ni Kitu gani

Shahidi: nilijikuta tuh nimengalia

Mallya: Kwa hiyo wewe Kwako Muda ni Kitu cha Muhimu au Siyo

Shahidi: Kitu cha Muhimu

Mallya: Kwa hiyo Kutoka Rau Mpaka Central Moshi unachukua Muda gani

Shahidi: Siwezi Kukadiria

Mallya: Ingawa sehemu zote mbili unazifahamu

Shahidi: Ndiyo

WS Robert Kidando: OBJECTION Mheshimiwa Jaji hili swali la Kwamba ameandika Saa Saba, Sijui ameandika wapi

WS: Inaweza Kupotosha, tunaona Jinsi lilivyo Halipo Sawa

Mallya: huo Muda nimeutoa Kwemye statement yake Shahidi ambayo amesoma

Jaji: anachosema Wakili Wa Serikali ni pale Unaposema Kwamba "Umeandika hapa Saa Saba"

Mallya: Shahidi Soma hapa

Shahidi: "Tuliwa kamata Saa Saba

Mallya: Mheshimiwa Jaji ni hapo

Jaji: Sawa sasa Endelea

Mallya: Ulipata wapi Kujua kuwa ni Saa Saba

Shahidi: Kwenye gari

Mallya: aliyeandika Maelezo ya Ushahidi wa Upekuzi, Maelezo aliyapeleka wapi

Shahidi: Sijui aliyapeleka wapi

Mallya: Kwa Kawaida mkiandika mnayapeleka wapi

Shahidi: Kwenye Jalada

Mallya: Kuna uwezekano alienda nayo Nyumbani kwake

Shahidi: Sifahamu

Mallya: Kuna uwezekano aliyapeleka kwenye Jalada

Shahidi: Sifahamu

Mallya: Kwa hiyo aliyeandika Maelezo hamkuonana naye tena

Shahidi: Hatukuonana naye tena

Mallya: Kuna Uwezekano Aliyepelela Dar es Salaam Maelezo Hayo

Shahidi: Sifahamu

Mallya: Kwenye Maelezo Yako umesema Kwamba Mlikuwa na Askari Wengine wa Moshi ni sahihi

Shahidi: Sahihi

Mallya: Kuna Sehemu Yoyote Umepata Kueleza Kwamba Mliachana Nao wapi hao Askari Wa Moshi

Shahidi: Sikueleza

Mallya: Idadi ya Askari Mliokutana nao Moshi Unakumbuka?

Shahidi: Sikumbuki Idadi yao

Mallya: Shahidi Washtakiwa Wanasema Mlikuwa watu zaidi ya 10 mliwavamia, na Kuwawekea Madawa na Bastola

Shahidi: Si kweli, Tulikuwa watano

Mallya: Jaji ataona wapi Kwamba Mlikuwa watano

Shahidi: Kwenye Statement Hakuna

Mallya: Kwenye Maelezo Yako Uliandika Idadi ya Watuhumiwa Wangapi Wakati Mnatoka Arusha

Shahidi: Hapana Siku andika Watuhumiwa Wangapi

Mallya: ilituamini kwamba Watuhumiwa Walikuwa Idadi ya watatu, Je ni sehemu gani gani

Shahidi: Hakuna

Shahidi: Wakati wa kwenda Tulikuwa na Moja na wakati wa Kurudi tulikuwa na Gari mbili Fredrick Kama Mlikuwa na Ulazima kwa nini hamkushuka

Shahidi: Kimya

Kihwelo: Nitakuwa Sahihi au sitokuwa Sahihi Nikisema Kwamba Mlipofika Central Police Moshi mlipaswa Kuwakabidhi kwanza Kisha Muwachukue kwa Hatua zingine za Upelelezi

Shahidi: Unaweza Kuwa Sahihi au siyo sahihi

FREDRICK: Jibu Moja tuh

Shahidi: Hautokuwa Sahihi

Fredrick: Je Unafahamu Kwamba Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya Ni Wageni pale Moshi

Shahidi: Sifahamu

Fredrick: Wakati Mnawatafuta Adamoo na Mohammed Ling'wenya Mliwakamata bila Mtu kuwaongoza

Shahidi: Sifahamu, Afande Kingai

Fredrick: Palikuwa na Ulazima wa Kuzunguka na Watuhumiwa

Shahidi: Kwa sababu walionyesha nia ya Kusaidia Kumtafuta Mtu wa tatu

Fredrick: Nyie Mnafanya kazi Masaa 24 Siku Saba za wiki?

Shahidi: Ndiyo

FREDRICK: kwanini Mliporudi Saa 5 Usiku hamkuwahoji Watuhumiwa

Shahidi: Tulikuwa bado tunamtafuta Mtuhumiwa wa tatu

Fredrick: Ni sahihi nikisema Kwamba Kuna Kiongozi Aliwaaagiza Msiwahoji watuhumiwa

Shahidi: Hapana Siyo Sahihi

Fredrick: Ni sahihi uliwafikisha Watuhumiwa Mbweni

Shahidi: Ndiyo

Fredrick: na Kwamba Mlipowafikisha Mbweni Mkawapa Majina bandia

Shahidi: Siyo sahihi

Fredrick: Johnson John ni nani

Shahidi: Simfahamu

Fredrick: Ni sahihi upo hapa Kutoa Ushahidi Wa kweli

Shahidi: Sahihi

Fredrick: Je Msiri wa Afande Kingai ni nani

Shahidi: Sifahamu

Fredrick: Ulisema Kwamba Ulimkabidhi wa Silaha A5340 na Simu

Shahidi: Ndiyo

Fredrick: Ni sahihi pia Kwamba pale Moshi hukushuka kwenye gari

Shahidi: Sahihi

Fredrick: Nitakuwa Sahihi Nikisema Ulikuwa unatembea na Vielelezo Muda wote Ukiwa Moshi

Shahidi: Ni sahihi Nilikuwa navyo Kwenye Begi Muda wote

Fredrick: Wakati watuhumiwa Wanakabidhiwa pale Central Police Moshi ulikwepo

Shahidi: Ndiyo nikwepo lakini Nje

Fredrick: Afande Jumanne Shahidi namba Moja wa Kesi Ndogo hii, Wakati anatoa Ushahidi Hapa alisema Yeye ndiye alielekezwa kabidhi watuhumiwa pale Central, Swali kati ya wewe na Yeye nani Mkweli

Shahidi: Miye sijui lakini najua Afande Jumanne na Afande Kingai Ndiyo wakikabidhi watuhumiwa Kituoni na Mimi nilikwepo

Fredrick: Kwa Mujibu wa Maelezo yako Umesema Afande Kingai aliwapa Ruhusa Mkanawe Uso au Kupata Break

Shahidi: Ni sahihi

Fredrick: Na baada ya Kuna wa Uso na Kupata Break, Vielelezo Vilikuwa wapi

Shahidi: Vilikuwa Kwenye Begi

Fredrick: Wakati Unatoa Maelezo Yako hapa na Wakili wa Serikali, Je kuna Mahakama Popote alikuongoza ilikusema ni wapi ulivitoa Vielelezo hivyo

Shahidi: Hapana

Kibatala: Shahidi Habari

Shahidi: Salama

Kibatala: Wakati wa Ushahidi Wako Ulionyeshwa Kitabu (naomba nipate Detention Register)

Kibatala: Wakati Unatoa Ushahidi Wako wote ukiongozwa Je Ulionyeshwa hiki kitabu.?

Shahidi: Si Kuonyeshwa

Kibatala: wakati wa Ushahidi Wako Kuna Mahala Uliongozwa kumwambia Jaji Pale CRO ulimkuta Mtu fulani au Mwenye Haiba fulani

Shahidi: Sikusema

Kibatala: We Unamfahamu Mtu aliyekuwa CRO Duty?

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: je akiwa Mahakamami Askari huyo unaweza Kumtambua

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Pale Mapokezi Central Police Dar es Salaam palikuwa na Askari Wangapi na jinsia zao

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Je katika Ushahidi Wako Kuna Mahala Popote Umemwambia Jaji Kwamba Ulishuhudia Kwamba Washtakiwa Wakifanyiwa Upekuzi

Shahidi: Sikusema Lakini...

Kibatala: sitaki lakini hapa.

Shahidi: Nataka Kufafanua, najua hatokasirika

WS Pius Hilla: Sijakasirika ila namkumbusha siyo Hilla ni Wakili Mwandamizi wa Serikali Pius Hilla.

Jaji: Kibatala Umesikia

Kibatala: Sitotilia Maanani

Kibatala: Shahidi Mwanzo nimesikia umetambua mshtakiwa kama ADAM KASEKWA

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Statement D1

Kibatala: Soma Hapo Kwenye Statement Umeandika kama nani

Shahidi: ADAM HASSAN.. Lakiniiiiiiii...

Kibatala: Sitaki lakini hapa

Kibatala: Wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikali Kuna sehemu Umesema Kwamba Adam Hassan ndiye Adam Kasekwa

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Nimesikia Sasa hivi Unacheo tofauti na Wakati ukiwakamata

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Umepanda Umeshuka

Shahidi: Nimepanda

Kibatala: Wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikali Kuna sehemu Umesema Kwamba Adam Hassan ndiye Adam Kasekwa

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Nimesikia Sasa hivi Unacheo tofauti na Wakati ukiwakamata

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Umepanda Umeshuka

Shahidi: Nimepanda

Kibatala: Nitakuwa sahihi Umepanda Cheo baada Kuwakamata Watuhumiwa

Shahidi: Nimepanda Cheo Kwa Elimu yangu

Jaji: Shahidi Wakili anauliza kwamba Umepanda Cheo Baada ya Kuwakamata au kabla

Shahidi: Nimepanda Mwaka huu 2021, Tarehe 13 August

Jaji: Kwa hiyo baada ya Kuwakamata

Shahidi: Ndiyo baada

Mahakama: Kicheko

Kibatala: Ni Muhimu Kuingia Kwenye Record hiyo

Kibatala na Je Wakati Unaongozwa na Wakili Wa Serikali Kuna Mahali alikuongoza Kufafanua Ulivyo panda Cheo

Shahidi: Kimya

Kibatala: Kuna Sehemu Kwenye Statement Yako Umeandika KAKOBE Kama Jina lingine la Moses Lijenje

Shahidi: Kimya

Kibatala: Katika Kielelezo Namba D1 cha Utetezi Katika hiyo Statement Yako, kuna sehemu Ipo Kwamba Watuhumiwa Walikwambia kwamba Moses Lijenje Ndiyo Kakobe

Shahidi: Haipo

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Dakika Moja na Mr. Mtobesya

Jaji anaitikia kwa kichwa

Kibatala: Unafahamu Kwamba Kuandika Maelezo ni Jambo la Kisheria

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unafahamu akama Afisa Wa Polisi ni Muhimu Kuweka Kumbukumbu zote katika Maelezo yako

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Ulishiriki Kuandika Maelezo Ya Nyongeza ya Shahidi Kwamba Uliwahi Kushuhudia Kuwakabidhi Wakina Mohammed Ling'wenya Central Dar es Salaam

Shahidi: Sijawahi Kushiriki

Kibatala: Jaji ataangalia wapi sehemu yoyote ambayo umeandika Kwamba Ulishuhudia Zoezi la Kuwakabidhi Watuhumiwa

Shahidi: Viongozi Ndiyo wanaandika

Kibatala: Pale Central Police Arusha Kuna CCTV camera

Shahidi: Ndiyo zipo

Kibatala: Zimewekwa Lini

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Central Moshi zipo CCTV?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Central Dar es Salaam zipo CCTV?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je unajua Kwamba Video Recording ni sehemu ya Kifaa Kazi?

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Ulishawahi Kushiriki kwenye kesi ya Ugaidi

Shahidi: Hapana

Kibatala: hii Ndiyo ya kwanza

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ulifahamu kwamba Unaenda Kushughulikia Watuhumiwa wa Ugaidi Tangu tarehe 04 August 2020

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Toka Mnapata Taarifa ya Kushughulika na Watuhumiwa wa Ugaidi Tarehe 04 August 2020 Mpaka 05 August 2020, angalau ni Siku Moja

Shahidi: Siku...? Angalau Masaa 12

Kibatala: Kwa hiyo ni Masaa 12 ya Maandalizi, Lakini hamjarekodi Mahali

Shahidi: Hatuja Rekodi Mahali

Kibatala: Maoni yenu Kiupelelezi Watuhumiwa walikuwa Wako Nje walikuwa ni Hatari siyo Hatari

Shahidi: Siyo kwa Maoni, Kwa Taarifa Zilizotolewa ni Watu Hatari

Kibatala: Lakini pamoja na Uhatari huo bado Mlikuwa Mnazunguka Na Watuhumiwa Wawili wanawaambieni Twendeni huku na huku

Shahidi: Tulikuwa tupo tayari na Hatari yake

Kibatala: Kwani Si Mlikuwa mnaelekezwa Pa Kwenda na Njia ya Kupita kutoka kwa Watuhumiwa Maliowakamata

Shahidi: Ndiyo, Ndiyo tulikuwa tunawafuatisha wanachosema

Kibatala: Mlikuwa mnafahamu kwamba Huyo Lijenje anasilaha za Kivita

Shahidi: Miye sifahamu

Kibatala: Nilisikia Mlienda Arusha na wewe na Mahita ni Wakazi wa Arusha

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Wakati Unaongozwa na WS uliwasiliana na Watu wa Arusha, Kwamba Kwa kuwa Nyie Mpo Moshi wao waende

Shahidi: Palikuwa hakuna Ulazima

Kibatala: Swali langu ni Je Ulimwambia Jaji, Ufafanuzi Utampa Mr. Pius Hilla Wakili Mwandamizi Wa Serikali?

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Shahidi Boma Kuna Ofisi ya Polisi

Shahidi: Kipo Kibatala: Ofisi za Serikali pia zitakwepo

Shahidi: Ndiyo Kibatala na Mlisimama Boma Kula?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: unafahamu PGO ya 354(7) Chakula Mnakula Kituo chochote cha Polisi au Ofisi za Serikali

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Pamoja na Kujua Mkala Chakula na Watuhumiwa Boma

Shahidi: Ndiyo sababu PGO inasema kama Hakuna Ofisi ya Serikali na Mnauwezo Wa Kuwalinda Mtakula popote

Kibatala: Himo pia Mlisimama Kupata Chakula

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na pia Himo pana Ofisi ya Serikali na Kituo cha Polisi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Wakati Unatoa Ushahidi wako ukiongozwa na Wakili wa Serikali Pius Hilla, Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Mlijihifadhi Ofisi ya Serikali, Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji au hukumwambia

Shahidi: Si kumwambia

Kibatala: Nilisikia Unasema Mlipata hitilafu ya Umeme Njia panda Himo, Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba hitilafu ni sehemu gani au Ilifanya Vipi lishindwe Safari

Shahidi: Si kumwambia

Kibatala: Sasa Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba nani alibaki ndani ya Gari au Nje

Shahidi: Nilimwambia Kwamba tulikaa ndani

Kibatala: Nani aliye mkabidhi Mtuhumiwa Ling'wenya CRO Central Dar es Salaam, Ni Jumanne au Mahita

Shahidi: aliwakabidhi watuhumiwa Pale Central Police Dar es Salaam ni Afande Kingai na Jumanne

Kibatala: Ni Ushahidi Wako Kwamba Kingai na Jumanne Walifikia hadi Counter

Shahidi: Nimewaona Wakiwa Kingai na Jumanne Counter wakikabidhi Watuhumiwa

Kibatala: Central Pako hivi Kuna Counter Ya Polisi ya Cement na Sehemu za Kukaa Ndugu (ANAONYESHA KWA VITENDO), Ulikaa wapi

Shahidi: Enheeeeee hapo Kwenye Ngazi

Kibatala: Kwa hiyo Ukiwa hapa Unaona Pale Counter Shahidi: Naona pale Counter, Wanachoandika Sioni ila watu nawaona

Kibatala: Mkiwa kwenye gari nani alimuuliza Mohammed Ling'wenya kuhusu Moses Lijenje?

Shahidi: Ni Afande Kingai

Kibatala: Unafahamu Kwamba hapo anakuwa ameanza Kukiri Kosa?

Shahidi: Hapana yalikuwa ni Maongezi tu ya Kawaida

Kibatala: ila Nyie ni Polisi na Mlienda Kwa ajili ya Kuwakamata

Shahidi: Ndiyo ila Ilikuwa Maongezi ya Kawaida

Kibatala: Wakati Mnawakabidhi Watuhumiwa Pale Central, Je Wakati Wanakabidhiwa wewe Bunduki Ulikabidhi Saa ngapi

Shahidi: Ndiyo nilisema Nilienda Kukabidhi Saa Moja

Kibatala: Nimekusikia Vyema Kwamba Tarehe 08 August 2020 mlipewa Maelekezo na Afande Kingai Kuwatoa Watuhumiwa Central Kuwapeleka Mbweni

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Kuna Mtu aliwaambia Kwamba walikuwa wameshahojiwa na wamekiri

Shahidi: Siku ya Tarehe 07 August 2020 Afande Kingai Alisema anabakia Kuwahoji

Kibatala: Kwa hiyo wewe hufahamu Chochote Kuhusu Maelezo Ya Ling'wenya?

Shahidi: Hapana Sijui

Kibatala: Mohammed Ling'wenya alifikishwa Mahakamani lini

Shahidi: 19 August 2020

Kibatala: Wewe Ulishiriki Kumpeleka Ling'wenya Mahakamami

Shahidi: Hapana sikuwepo

Kibatala: ulijuaje Wamepelekwa Mbweni

Shahidi: Nilisikia Kwa Afande Kingai

Kibatala: Wewe ulifika Mbweni?

Shahidi: Sijawahi kufika Mbweni

Kibatala: Wewe si uliwapeleka Mbweni

Shahidi: Ndiyo Nilifika Mbweni

Kibatala: Sasa watuhumiwa wanasema ulikuwepo Mbweni

Shahidi: Sijawahi kufika Mbweni

Kibatala: Sawa mimi kazi yangu Kuuliza Maswali, Ukijichanganya ni Kazi ya Jaji Sasa Kujua Ukweli.

Kibatala: ulisema Ulikuwa na Silaha, Je ukiongea lolote kuhusu Silaha yako

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ilikuwa silaha gani

Shahidi: ilikuwa AK 47

Kibatala: Ulizungumzia kuikabidhi pale Central

Shahidi: Hapana

Kibatala: Vituo Vyote Mahabusu Wanakuwa Chini ya OCS

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mlimtaatifu OCS kwamba Mnampelekea Watuhumiwa Pale Mbweni

Shahidi: Hapana, hiyo ni kazi ya Viongozi

Kibatala: Wakati Mnatoka Moshi Tarehe 06 August 2020, Je ulikuwa unafahamu Kwamba Moja Wapo ya Mambo yatayofanyika Kufika Dar ni Ling'wenya Kuandika Maelezo ya Onyo

Shahidi: Hapana Sikufahamu

Kibatala: Wakati Mnatoka Moshi Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Afande Kingai, Inspector Mahita, na ASP Jumanne Ambao wa Kubwa zako wakimwambia Ling'wenya Kwamba Tunakwenda Dar es Salaam na Tulifika Dar es Salaam Kuna Maelezo ya Onyo yataandikwa

Shahidi: Sikusikia

Kibatala: Wakati wote simu zilikuwa wapi

Shahidi: Nilikuwa nazo Mimi

Kibatala: Na wakati wote Unaongozwa na Wakili Wa Serikali Hukusema Kwamba Ulitoa Simu kwa Ling'wenya Kwamba Unaweza Kuwapigia Ndugu zako au Mawakili wako

Shahidi: Sikusema Ndiyo

Kibatala: Kuna Mahala Popote Umemwambia Jaji Kwamba Wakati wowote tunazunguka Pale Moshi Mpaka Arusha, wakimwambia Ling'wenya Kwamba hapa tupo Kwenye Mazoezi Mazito ya Kisheria Mpaka Unamtaja Lijenje, Je Nikupe Simu Uongee na Ndugu au Mwanasheria

Shahidi: Hapana Sijamwambia

Kibatala: Kwa kuwa Ling'wenya alikuwa anatoa Ushirikiano Kwenu Mpaka Mkaenda Stendi ya Mabasi, Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Lijenje alikuwa anaenda Mkoa gani

Shahidi: Hapana Siku Mwambia

Kibatala: Kuna Mashahidi hapa wanasema Kwamba, Ling'wenya alishakiri na Kutoa Maelezo Yake JUU YA ushiriki wake, Je Ulishawahi Kusikia Afisa yoyote akisema Kwamba Kwa kuwa Ling'wenya ameshakiri Ngoja nimpeleka Mahakamani?

Shahidi: Siku sikusikia

Kibatala: Ulishawahi Kufanya Kazi CRO

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kuna Karatasi Yoyote ambayo Mtu Alisha kabidhi Mtuhumiwa Hakuna Mahala Popote ambapo ANAPEWA katasi lolote pale CRO

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kama Ulimtajia Dereva Mlitoka naye Arumeru Mpaka Moshi

Shahidi: Sikumtaja Jina, Nilitaja Dereva

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama ulitaja Jina la Derava aliyewatoa Njia panda Himo Mpaka Mpak Dar es Salaam

Shahidi: Hapana Sikutaja jina

Kibatala: Mliwahi Kumuona Mkuu wa Kituo cha Polisi Central Dar es Salaam

Shahidi: Hapana

Kibatala: Pale Rau Madukani kuna Ofisi ya Mtaa au Kituo cha Polisi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Mheshimiwa Jaji sina swali lingine

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Tumefanya Assessment Ya Maswali na Hakuna Swali la Kufanya Re examination Anakaa Chini

Jaji: Tunakushukuru kwa Ushahidi Wako, sasa unaweza Kwenda

Shahidi anatoka kizimbani

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba Hairisho Mpaka Kesho tarehe 24 November Ilituweze Kuja na Shahidi Mwingine

Jaji: Nyinyi ndiyo Mnaojua huyo Shahidi anayekuja anaushahidi Gani, Kama mnaona ni Mfupi Waje wawili

Kibatala: Sahihi Mheshimiwa Jaji

WS Robert Kidando: Tutaona Cha Kufanya, Lakini kwa huyu wa Kesho tayari yupo

Jaji: Upande wa Utetezi

Kibatala: Hatuna Pingamizi

Jaji: anaandika Kidogo Mahakama: bado ipo Kimya

Jaji: basi Mahakama inakubiana na maombi ya upande wa mashtaka kuhairisha kesi, mashtaka mnaelekezwa kwamba ukiona ushahidi siyo mrefu walete mashahidi wawili. Na washtakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya magereza mpaka kesho Asubuhi saa 3 kamili

Jaji anatoka
 
Hii nchi hatuko serious. Mama anasifia kifua cha Harmonize huku kesi ya kubumba inapoendelea yeye anaona fresh tu. Duh!🤦🏾‍♂️
Wewe endelea kudharirisha watu badala ya kuhangaika na ushahidi- mtu wenu atafungwa kibudu
 
Mashahidi wa mchongo🤡🤡🤡
qsD.jpg
 
Umefuatilia aibu aliyoileta huyo shahidi Goodluck siku ya leo? Hii kesi ni aibu tupu kwa Taifa letu.
Ndo hayo hayo-sasa aibu yake inamsaidiaje Mbowe kwa mfano?

Jaji: basi Mahakama inakubiana na maombi ya upande wa mashtaka kuhairisha kesi, mashtaka mnaelekezwa kwamba ukiona ushahidi siyo mrefu walete mashahidi wawili. Na washtakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya magereza mpaka kesho Asubuhi saa 3 kamili
 
Umefuatilia aibu aliyoileta huyo shahidi Goodluck siku ya leo? Hii kesi ni aibu tupu kwa Taifa letu.
Pamoja na hiyo aibu ya leo haya ndiyo matokeo yake

Jaji: basi Mahakama inakubiana na maombi ya upande wa mashtaka kuhairisha kesi, mashtaka mnaelekezwa kwamba ukiona ushahidi siyo mrefu walete mashahidi wawili. Na washtakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya magereza mpaka kesho Asubuhi saa 3 kamili
 
Mallya: Kwenye Maelezo Yako umesema Kwamba Mlikuwa na Askari Wengine wa Moshi ni sahihi

Shahidi: Sahihi

Mallya: Kuna Sehemu Yoyote Umepata Kueleza Kwamba Mliachana Nao wapi hao Askari Wa Moshi

Shahidi: Sikueleza

Mallya: Idadi ya Askari Mliokutana nao Moshi Unakumbuka?

Shahidi: Sikumbuki Idadi yao

Mallya: Shahidi Washtakiwa Wanasema Mlikuwa watu zaidi ya 10 mliwavamia, na Kuwawekea Madawa na Bastola

Shahidi: Si kweli, Tulikuwa watano

Mallya: Jaji ataona wapi Kwamba Mlikuwa watano

Shahidi: Kwenye Statement Hakuna

My take: kama kati ya hao askari watano hakuna aliyetokea Moshi, basi watuhumiwa walisema ukweli kwamba askari waliowateka na kuwawekea madawa ya kulevya na bastola walikuwa 10 jumla. Wao kwenye maelezo yao yote walidai ni askari 5 ndiyo walioenda kuwakamata kina Adamoo. Huyu anasema askari wa Moshi walikuwepo pia.

Kaaazi kweli kweli!
 
Wengine tunashangaa wao kubambikiwa kesi na ushahidi wa hao vilaza wewe unashangaa wao kuwa rumande?
 
Back
Top Bottom