kupelwa
JF-Expert Member
- Aug 24, 2011
- 1,087
- 450
Kwa takribani kama siku tano hivi, maeneo mbali mbali wilayani kinondoni hasa mapori ya madale karibu na magereza ya boko, kulifanyika bomoabomoa ya wavamizi iliyosimamiwa na mkuu wa wilaya na RPC wa kimkoa wa kinondoni.bomoa bomoa hii ilikwenda mbali na kuhamia maeneo mengine kadhaa wilayani kinondoni na hasa kata ya wazo.Alipouulizwa mkuu wa wilaya na RPC kinondoni wanatekeleza ubomoaji huu kwa amri gani,walijibu,"ni kwa amri ya mahakama".amri hiyo ya mahakama ilikuwa inataka ubomoaji wa kaya sita kwenye soko moja maeneo ya madale, ambayo pia hukumu haikuzingatia walalamikiwa kuwa hawakutakiwa kuwa wananchi bali manispaa ya kinondoni ambayo ndo anatakiwa kumiliki soko.Pia maelezo yao yalienda mbali zaidi kuwa kuna wakimbizi ambao ni mungiki wamevamia mashamba ya watu na kuwa tishio kwa maisha ya wamiliki wa mashamba hayo.
jana kwenye ,kipindi cha pambanua, wanasheria wa LHRC walijaribu kuchambua kisheria na kisiasa kuhusu haki na mazingira yalitumika katika bomoabomoa hiyo, kumeonyesha mapungufu mengi kama ifuatavyo;
1.haikuzingatia haki ya upande wa wavamizi/wakimbizi nao hata kama walikuwa wakimbizi , kwa sababu kati yao wana haki ya kuwa maeneo hao walipewa kwa taratibu za kiuongozi , enzi hizo mkuu wa mkoa makamba aliwapa maeneo hayo sababu wenye mashamba hayo waliitwa wayaendeleze lakini hawakuonekana, hivyo makamba akawapa kwa nyaraka sahihi.
2.wlalamikaji wa mashamba yaliyovamiwa, walienda mahakamani kuomba haki ya wavamizi hao kuondolewa kisheria, na kesi yao ilikuwa inatajwa jana, lakini kabla ya mahakama kutoa nani mmiliki halali wa maeneo hayo, tayari mkuu wa wilaya na RPC alikuwa ametekelza ubomoaji huo bila mahakama idhini hiyo.
3.amri ambayo ilikuwa ya kubomoa kaya sita ambazo zinalalamikiwa kuwa ni soko na mmoja wa walalamikiji, ilikuwa ya kaya sita tu.na pia amri hiyo tayari ilikuwa imepingwa mahakamani sababu walalamikiwa si manispaa ya kinondoni ambaye ndo mmiliki wa soko.lakini tayari huku kukiwa na kesi ya kupinga hukumu hiyo bado ipo mahakamani, mkuu wa wilaya na RPC walikuwa wanaendesha bomoabomoa hiyo.
4.Je, kama ilikuwa amri ya kaya sita , na ilikuwa imepingwa mahakamani iweje kubomoa makazi ambayo hayakuwa kwenye hukumu na amri hiyo , huku RPC anafurahia kufanya hivyo kwa kuchoma mali zilizokuwa ndani ya nyumba hizo.
5.je kama kweli walikuwa wakimbizi na wahalifu , uhamiaji imekuwa wapi miaka yote taratibu za kisheria zifuate ?na je inakubalika kuharibu mali za mkimbizi bila kuwa na ushahidi wa wazi na ulithibitishwa?
katika mada hii nisingependa kuwwatetea watakaothibitika kuwa kwli ni wavamizi, je kama hatawatakuwa wavamizi , huo uharibifu wa mali na makazi ya familia 1000, nani atawafidia?je kwanini mkuu wa wilaya na rpc kama kunawavunja sheria za jinai kama kutishia, kubaka, kujeruhi, kwanini asingewashughulikia ipasavyo hicho kikundi kuliko kubomoa makazi ya watu wote hata wasonkuwa na makosa?piakulikuwa na kesi mahakamani , je DC RUGIMBANA na RPC wako juu ya sheria za nchi na mahakama?na pia , je srikali hii ya ccm inafurahia kuona wananchi wake wakiwa hawana makazi wanalala nje bila chakula, na namna nyingine ya kujikimu kimaisha.
ikumbukwe, diwani wa wazo, mwenyekiti wa serikali ya mtaa, wajumbe wamekiri hawakushirikishwa katika zoezi hili ambalo linapingana na haki za binadamu.
TAFAKARI:WAPI SERIKALI YETU YA CCM INATUPELEKA?NDO UTEKELEZWAJI WA AGIZO LA PINDA LA MADC KUKOMOA WANANCHI ILIKUSUDI CCM IENDELEE KUTAWALA?
CHANZO:LHRC