Ya Nyerere USSR, Mwinyi USA, Mkapa Japan, Kikwete Malaysia na Magufuli Rwanda

Mada nzuri sana, naaamini Watanzania tunapaswa kwanza kukubali mabadiliko katika mind transition, baada ya hapo tutaenda na kasi zilizopo, tufanye kazi na pia wakubwa wafanye maamuzi mazuri katika kodi zetu na zile dhana za elimu bure au kilebure ziondoke, na watanzania waelezwe kuwa katika kodi zetu watanzania tumefanya a, b, c ... ni vyema pia that we keep on sailing in the same 2025 Tanzania Development vision. Kuiga mifumo ni sawa bora iakisi matakwa yetu kwa wakati na iwe ni sustinable... Binafsi nampongeza kwa hatua hizi ila bado jitihada zaidi katika Capital investment inahitajika... Kiungwana walau 2018 ndio tuanze kuassess progress, as for now the foundation is ok.... stick and carrot motivation is highly needed for behaviral shaping to all unaccountable bearers....
 
Mtoa hii mada ameshindwa sana kujenga hoja kwa kutumia tool of analysis badala yake amekopi model iliyotumika karne ya kumi na tisa na kuamini kuwa ndiyo model inayotakiwa kutumiwa katika karne ya leo. Halafu title yake imetoa tuhuma ambazo siyo sahihi kwa sababu Nyerere hakuwa na uhusiano na URUSI kama anavyodai kwani mpaka leo Tanzania haijawahi kuwa na alama yoyote ya URUSI, angalu China walituletea Tazara na URAFIKI. Hakuna shughuli iliyoendeshwa au kiwanda hata kimoja kilichojengwa wakati wa Nyerere kwa utaalamu wa urusi. Urusi ilitumika tu kama soko la kununua silaha kwa ajili ya kupigania uhuru wa Afrika kwa vile nchi za magharibi zilikuwa hazisapoti ukombozi wa Afrika! Halafu pia urusi ilikuwa inatoa skolaship nyingi sana kwa watu wote wa nchi za dunia ya tatu kusoma chuo cha Urafiki cha Patrice Lumumba na vyuo vingine vya urusi, na hivyo Tanzania kama mnchi nyingine zote za dunia ya tatu ilifaidika na skolaship hizo ila siyo kwa sababu Nyerere aliitegemea Urusi!

Ingawa mtoa mada ana uchungu kuona kuwa huenda serikali inajaribu kukata matawi badala ya kukata shina la matatizo, hata hivyo huenda mada ikapwaya sana iwapo itachambuliwa kwa data na evidence zilizokamilika! Mimi sintachangia ila tukumbushane kuwa model inayofanya kazi sehemu moja huwa haifanyi katika sehemu nyingine. Model iliyofanya kazi Rwanda, inafiti sana katika mazingira ya Tanzania kuliko model iliyofanya kazi Uingereza au marekani ambako uaminifu wa raia unategemewa.

Tatizo kubwa la Tanzania ni uongozi wa sheria, ambao ndio unafuatwa na Rwanda pamoja na nchi zote zilizoendelea, lakini siyo uongozi ruksa ulioletwa na Mzee mwinyi, ambapo kuanzia hapo maafisa wote wa Internal revenue department- baadaye TRA wamekuwa ni matajiri!
 
Mtoa hii mada ameshindwa sana kujenga hoja kwa kutumia tool of analysis badala yake amekopi model iliyotumika karne ya kumi na tisa na kuamini kuwa ndiyo model inayotakiwa kutumiwa katika karne ya leo. Halafu title yake imetoa tuhuma ambazo siyo sahihi kwa sababu Nyerere hakuwa na uhusiano na URUSI kama anavyodai kwani mpaka leo Tanzania haijawahi kuwa na alama yoyote ya URUSI, angalu China walituletea Tazara na URAFIKI. Hakuna shughuli iliyoendeshwa au kiwanda hata kimoja kilichojengwa wakati wa Nyerere kwa utaalamu wa urusi. Urusi ilitumika tu kama soko la kununua silaha kwa ajili ya kupigania uhuru wa Afrika kwa vile nchi za magharibi zilikuwa hazisapoti ukombozi wa Afrika! Halafu pia urusi ilikuwa inatoa skolaship nyingi sana kwa watu wote wa nchi za dunia ya tatu kusoma chuo cha Urafiki cha Patrice Lumumba na vyuo vingine vya urusi, na hivyo Tanzania kama mnchi nyingine zote za dyunia ya tatu ilifaidika na skolashjipi hizo ila siyo kwa sababu Nyerere aliitegemea Urusi!

Ingawa mto mada ana uchungu kuona kuwa huenda serikali inajaribu kukata matawi badala ya kukata shina la matatizo, hata hivyo huenda mada ikapwaya sana iwapo itachambuliwa kwa data na evidence zilizokamilika! Mimi sintachangia ila tukumbushane kuwa model inayofanya kazi sehemu moja huwa haifanyi katika sehemu nyingine. Model iliyofanya kazi Rwanda, inafiti sana katika mazingira ya Tanzania kuliko model iliyofanya kazi Uingereza au marekani ambako uaminifu wa raia unategemewa.

Tatizo kubwa la Tanzania ni uongozi wa sheria, ambao ndio unafuatwa na Rwanda pamoja na nchi zote zilizoendelea, lakini siyo uongozi ruksa ulioletwa na Mzee mwinyi, ambapo kuanzia hapo maafisa wote wa Internal revenue departmenet, na baadaye TRA wamekuwa ni matajiri!
Umenena vyemo ndugu.
Hata hao wa rusi, wachina na wengine hata wao wanaangalia watafaidi nini katika urafiki huo.Sasa, ukiona na wewe una faida na huo urafiki, mtainuana sawa, na nadhani huruhusiwa kwa sababu kuna kitu kipya watajifunza toka kwao. Kwa hiyo kwa ajenda yake ya Magufuli na Kagame, nahisi hajafikilia. Wakati mwingine ukiona mtu kakuzidi, lazima umuulize"Wewe ulifanyafanyaje" na swali hilo litakuwepo ukishaona ukimuiga lazima utapiga hatua. Sasa, Tanzania si mna mfumo wa kutoza kodi! Na hilo ndo hasa aliaadiwa wataaramu wa kumsupport! Mbona wa Tanzania hawajafanya hivyo! Na bora ungefurahia kitendo hicho, watanzania wajifunze kutoka kwa wanyarwanda, af huo utaaram nao wakawauzie nchi nyingine, na ni jambo linalowezekana.
Inaonekana ana hasira na mambo ya zamani hata kabla hajazaliwa, na hasira na wakati uliopo na tena wakati ujao.
 
Uzi Mzuri Sana. Mh Magufuri Kamteua Professor wa UDSM kuwa msahuri wake wa uchumi. Nadhani Kuwe na Sheria Inayomuwajibisha Mtu Kama Huyu Hasa Ikibainika Amemshauri Rais Vibaya.

Kwa Kweli Tunahitaji Wachumi Wenye Kuzua Mijadala Fikirishi Kama Kwenye Huu Uzi.
 
Watanzania hawana jema kazi kulaumu tu inamaana hamjaona hata lamaana hata moja mkashukuru kwanza ndo muanze kulaumu?? Usiposhukuru kwa dogo hata ukitendewa kubwa hutaweza kushukuru
 
Msiangalie ubaya kwani hakuna zuri alilofanya? Ata mwaka hajamaliza lakini maneno yamekuwa mengi. Unafikiri upinzani ni kupinga kila kitu.
muda mwingine sio lazima ucomment mzee mwenzangu...au umekunywa maji ya spirit nn
 
Watanzania hawana jema kazi kulaumu tu inamaana hamjaona hata lamaana hata moja mkashukuru kwanza ndo muanze kulaumu?? Usiposhukuru kwa dogo hata ukitendewa kubwa hutaweza kushukuru
acha sifa za kijinga angekuwa amekunufaisha ungekuwa humu wewe
 
Daima mti wenye Matunda ndo unaopigwa mawe. Shukuru kwanza kwa kidogo ndo uanze kukosoa. Daima watu hutafuta kasoro tu hata jema hawalioni. Kama hujaona jema hata moja hata ungeletewa malaika ungelalamika tu hakuna kiongozi atakaye weza kumridhisha kila mtu kwahiyo watu wa kulialia kama nyie hatuwashangai
 
Well said but as usual nawe umekuja na ndoto kama walivyo wasomi wengi wa Bongo wanavyowaza. Je ulishawaahi kuwaza juu ya aina ya labour iliyopo inayoweza kutekeleza hiyo mipango unayowaza?

Je unadhani viongozi wote waliopita walikwamishwa na nini zaidi ya labour iliyokuwepo?
Pse try to think out of the box.
Nini kifanyike kwa maoni yako mkuu
 
Mada nzuri, inafikirisha lakini kama ilivyo ada yetu tumeishia kuijadili KISIASA, na huu ni ushahidi kwanini tumepotea njia kama taifa,
 
Rostow-model.jpg



Viongozi wetu walikuwa wanatazama economic models toka nchi hizo

Naona aliyefanikiwa alikuwa ni Ali Hassan Mwinyi tuu kwani aliifungua nchi toka kwenye giza na dhiki na kutuweka kwenye Free Market economy.

Mzee Mkapa aliendelea kidogo na alikuwa anatazama sana economic model ya Japan na ukweli alileta fiscal discipline kwenye nchi

Jakaya naye aliona isiwe taabu yeye aliamua ku copy development model ya Malaysia na tukaeletewa Big Results Now na na likaanzishwa Quango pale linaitwa Presidential Delivery Unit na mwishowe mnaujua

Magufuli kaja na mpya hataki cha BRN wala nini nalichoamua kukifanya ni kuivunja hiyo BRN na kawaambia nchi haihitaji Presidential Delivery Unit wakati wapo mawaziri na na technocrats ambao wanalipwa kwa kufanya hayo. Naona kaona isiwe mbali....sasa yeye anaiga Rwanda

Wataalam wa Development Economics mnasemaje kuhusu hili?

Mfano, siamini kama kweli serikali yake iko serious na kufanya mabadiliko kwani bado iko obsessed na personalities badala ya kufanya structural reforms. Mfano hahitaji kuanzisha mahakama za mafisadi wakati mahakama zipo na sheria zipo kinachohitakjina ni enforcement ya hizo sheria.

Huwa sielewi kwa nini kama traffic lights zinafanyakazi lakini kila kukicha asubuhi mpaka usiku kunakuwa na traffic barabarani kuongoza magari. Issue hapa ni enforcement ya hizo sheria na kuacha kupotezeana muda kupelekana Central Police kujaza forms na kuandika statements ndefu bila sababu za msingi.

Ishu ya wafanyakazi hewa ni ndogo sana kama serikali ya nchi hii inge invest kwenye e-government na transparency. Hivi ukishainvest kwenye electronic payment system ambayo iko linked na HR deps za idara ya serikali wafanyakazi hewa watatoka wapi?


egov.jpg


Sielewi kwa nini tumeshindwa kabisa hii ya kupeleka madaraka mikoani na de centralization. Naamini kila mkoa ungewezeshwa na ukajiamulia development na investment plans zake na vitu vikawa linked na haya mambo ya e-government tusingepeana kazi ya kuhakiki nani anafanya nini mikoani kwa style za kupelekeana vimemo.

Mfano nataka niingie kwenye website ya serikali ya wilaya na mkoa na nione kodi zangu zinafanya nini, minutes za tenda zinavyotolewa, na distribution ya kodi na pia tuone nani nalipwa nini kwani ni pesa za walipa kodi and we deserve to know.

Jambo lingine nakumbuka Rais Magufuli alitangaza kwenye mkutano wa hadhara kuwa kaanzisha kikosi maalum ambacho kinaongozwa na mwanamke kuwakamata na kuwashughulikia mafisadi sasa hii inamaanisha kuwa yeye kama commander in chief haaamini vyombo vyake vya dola kama Uslama wa Taifa, Polisi, magereza, mahakama, PCCB na wengineo?

Point nyingine siamini kuwa hii mipango ya maendeleo tuliyonayo inaendana na dulia tuliyonaye ya leo na mpaka sasa wote nadhani mnajua kuwa Tanzania VISION 2025 ni muflis, MKUKUTA haieleweki, na sasa tumeletewa development plan ya miaka 5 na theme kubwa mle ni kujenga viwanda . Sasa nauliza what happened to Tanzania vision 2025? review ilifanywa lini? je inabidi ifutwe na tuwe na tanzania VISION 2050 au tuachane na hizi visions kisha tuende tuu kama pay as you go?

C3Pweb_HomeSlider2.jpg

Mheshimiwa bajeti ya serikali yake inasema sekta binafsi zitashirikiana na seirkali kujenga na kufanya mambo ya maendeleo....kwa kupitia PUBLIC PRIVATE PARTNERSHIP (PPP) few days afterwards anatangaza wakati anafungua mtambo wa umeme wa Kinyerezi kuwa Tanesco alone ndio itakuwa ianafanya kazi ya power generation, sasa hii ni kinyume na MKUKUTA, TANZANIA VISION 2025, BAJETI YA 2016/2017, INVESTMENT POLICY na policies kem kem ambazo kwenye sekta ya energy inasema wazi kuwa PPP ni muhim ili kukaribia malengo ya taifa ya maendeleo na huwezi kufanya haya mambo kama unaleta mixed signals. One minute mawaziri wetu na serikali yetu inasema inaomba wawekezaji kwenye sekta ya nishati waje...next minute mfalme anatakangaza hataki kuona hiyo sekta inaleta Independent Power Producers (IPPs).

Confusing right?


Ohhh well...nimalizie tuuu kwa kusema haya

Maguli anasema anataka nchi iwe ya viwanda

Huwezi kuendesha hivyo viwanda bila ya kuwa na umeme wa kutosha

Tanzania ina watu almost milioni 55

Umeme wetu ni megawati 1,500

public-private-partnerships-10-728.jpg


Ili tufikie huko tunakotaka kwenda kuwa na high speed railway ambayo itakuwa iko linked nchi nzima, na kuwa na hayo maviwanda anayoyataka Magufuli inabidi tuwe na umeme si chini ya Megawati 20,000 (na hii kama tuko serious). Huu umeme tunaweza kuupata kupitia gas, maji, solar, biomas, wind nk

N akuwa na umeme hautoshi lazima tuwe na infrastructure za kufa mtu....lakini hii ndio nchi pekee ambayo naina COMPREHENSIVE infrastructure plan...na hapa nazungumzia barabara, pileline za hizo gezi na mafuta, reli, viwanja vya ndege na kadhalika

sasa pesa zitatoka wapi?

Pesa nyingi zipo humu mitaani lakini lazima Magu na watu wake wafanye serious structural reforms na sio hizi gimics na kufukuzana na watu wanaofanya VAT SCAMS. Kama system ipo in place ni ngumu kwa watu kufanya hizo scams. So the best way ni kwa serikali kuuza bonds ili ku raise hizo pesa. Ethiopia walifanya na bwawa la GRAND RENAISSANCE DAM ambayo ni megawati 6,000 na raia wa Ethiopia wali raise DOLA BILIONI 4 na project nzima ili cost around 6.4 billion usd

YoV856D.jpg




Bila kusahau kuwa EGYPT juzi juzi nao wali uza bonds za dola bilioni 5 kwa wananchi kwa ajili ya upanuzi wa SUEZ ambao umegharimu dola bilioni 8

sasa, sielewi kwa nini sisi tunapigishwa siasa na watawala wetu ambao wao kila kukicha wanatuletea development models ambazo kiukweli zimefeli (kasoro ya Ali Hassan mwinyi ambayo ilitufungua na kutuingiza kwenye soko huria).

Kama kweli Magufuli angekuwa serious na haya mambo anayoyataka ya viwanda na maendeleo sidhani kama NSSF chini ya Mkurugenzi wao bwana Kihyahara leo waneenda kuwekeza pesa za wachangiaji kwenye vibwawa vya samaki wakati tuna maziwa na mito na bahari....na kama wao wana pesa sana kwa nini wasiivest kwenye energy na infrastructure projects kwa kutumia modality ya Finance, design, build,operate and transfer?
$_35.JPG



anyway hizo ndio thoughts zangu leo Jumapili na natumai tubadilishana mawazo zaidi

Salaam..
Nadhani kuna kila haja ya kumpa Mhe Rais muda. Na la msingi zaidi ni wataalamu waliomzunguka wamshauri vyema katika kufikia malengo yake, Naamini kwa binafsi yangu kuwa Mhe ana nia nzuri ya kulifikisha taifa mbali katika sectors mbalimbali na zaidi ikiwa ni kuipaisha nchi mpaka kufikia uchumi wa kati. Mwisho, Serikali ni vyema iwaamini wataalamu wake na education policies ziwe reformed ili graduates wengi wa rely katika creativity kuliko kukariri tu.
 
Ili nchi iweze kutekeleza mipango yake inge lenga zadi kuwapa elimu bora wananchi wake. Hatuna watu wenye ujuzi wa kuzalisha viwandani, usimamizi wetu ni wa hovyo, wale wenye uwezo wa biashara wanatengwa-hawapewi fursa ya kuisaidia nchi.

watendaji wetu wamechoka hawana ubunifu au wamepitwa na wakati au ni waoga, watunga sheria wetu wanaangalia maslahi binafsi, wapinzania hawana nafasi ya kufanya chochote-wamezibwa na dola kila kona. wananchi hawana uhuru wa kusema wanataka nini na hata pale wanaposema hakuna wa kuwasika: Wananchi hawataki mwenge- hakuna anaewasikia, wanataka katiba ya warioba- watawala hawaitaki, hawataki wakuu wa wilaya wanasema DED atosha-watawala hawataki

Nini kifanyike? Watawala wawasikilize wananchi wanataka kuongozwa vipi bila kuuzwa, bila hivyo tusahau ustawi wa wanachi wetu
 
Binafsi namfanisha na stalin wa USSR. Huyo jamaa baada ya kuchukua madaraka kazi kubwa aliyokuwa akiifanya ilikuwa kutumbua (kuua) watu waliokuwa na maoni tofauti na yake. Hakutaka kuona chembe ya upinzani. Ilifika wakati vikao vyote vilikuwa mashindano ya kumsifia stalin.

Walipovamiwa na hitler walielemewa sana mwaka wa kwanza, ilibaki kilometa chache moscow itekwe. Stalin alichanganyikiwa , akawa muda mwingi yuko peke yake. Viongozi wakuu wa chama , au politburo, wakajitosa wakakaa kikao bila stalin wakaafikiana kwa pamoja wamwendee stalin na kumuomba awape uhuru zaidi makamanda wake wa kupanga ni jinsi gani wapambane vita.

Wakamkuta stalin akiwa na wasiwasi sana, wakamtaka radhi kwa kukaa kikao bila yeye na wakamweleza mapendekezo yao. Stalin akasema kama mmeafikiana hivyo yote kheri, nilidhani mmekuja kunikamata. Tokea hapo stalin akaanza kusikiliza ushauri wa makamanda na watendaji wake, upepo wa vita ukabadilika, stalin akawa mhamasishaji mkuu huku makamanda wakifanya vitu vyao. Taifa likawa moja na lenye nguvu zaidi.

Wanasaikolojia wanadai alikuwa katili sababu alihisi anadharauliwa kwa kuwa asili yake ilikuwa jamhuri ndogo ya georgia na hakuweza kuongea kirusi fasaha, yaani aliongea kirusi kwa lafidhi ya kigeorgia, broken za hapa na pale. Na alikuwa mfupi 5'4, kwa kulinganisha na warusi wengi.

Suala la mfalme wetu kutokujua kiingerereza fasaha inaweza kuwa sababu ya yeye kuchukia upinzani wa aina yoyote, au pengine ana mapungufu mengine ambayo hataki yahojiwe e.g kupanda ndege. Au hataki kuhojiwa kwa nini maisha yanazidi kuwa magumu tofauti na ahadi alizozitoa.

Itafika muda atatambua nchi haiwezi songa mbele kwa mawazo ya mtu mmoja. Baraza la mawaziri lina nafasi yake, bunge huru, mahakama huru, media huru, wapinzani , washauri, maoni ya watu, n.k.

Lakini atambue jinsi maisha ya watu wake yanavyozidi kuwa magumu kina cha kaburi la chama cha magamba kinaongezeka pia, nae atashindwa kulala usingizi mnono baada ya kutolewa madarakani.
Heko sana!
 
Kwa kweli Mzee wa Chato kachemka Mbaya sana kuwatumia hawa Wanyarwanda.
Mshindani mtarajiwa wa Air Tanzania anatarajiwa kuwa Rwanda Air halafu unawafanya Wataalam wa Rwanda Air ndio Strategist wa kuanzisha Air Tanzania. Kosa hilo liliwahi kufanyika Pale Basil Pesambili Mramba mmoja wa Wamiliki wa Precision Air alipoteuliwa kuwa Waziri wa Miundombinu ambapo pia alikuwa Msimamiz mkuu wa Air Tanzania.

Rwanda huenda ni moja ya nchi zinazolipa Import na Export tax kubwa zaid kwa kuingiza na kusafirisha bidhaa zao halafu unawapa kazi ya kutengeneza Mifumo ya kudhibiti ukusanyaji wa kodi. Mfungwa anapewa kazi ya kuchagua kufuli bora la kudhibiti Geti la Gereza.

Mtu anaetarajiwa kuiba na kuingia kwny mpaka wa Shamba lako ni Jirani unaepakana nae halafu ndio umempa kazi ya kukutazamia Mpaka huo watu wasihamishe nguzo za Mpaka.

Hapa mzee ame-
upload_2016-7-8_9-17-28.jpeg


Wasiwasi wangu ni kuwa ama awajui hao jamaa au ana undugu nao.
 
Back
Top Bottom