X anataka kurudi...

B'REAL

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
4,279
2,733
habari za mchana na ma greater thinker...kitambo kidogo sijapata msaada kutoka kwenu,kuna mwanamke tumeanza ma uhusiano kama mienzi mitano iliyo pita,kwelii na mpenda na ananipenda,alikujaa kwangu baada ya kuumizwa na kutendwaa na jamaa yake wa kwanza,jamaa alikiwa nae huku ana girlfriend mwingine nje ya nchi.alipo rudi yule aliekuwepo njee ya nchii akamtelekeza huyu mwanamke,kwavilee nilikuwa namtaka siku nyingi ila alisha niambia yuko na huyo jamaa,so nikawa nimepunguza mawasiliano,baada ya kutendwa kulee akawa anawasiliana na mimi like friend wa kawaida na kunisimuliaa yote yalio mkuta.
nika mpa moyo and tukaa ends kuwaa lovers.but now yule jamaa amekujaa kujua yule girlfriend wake alioko abroad anataka kuolewaa,so kuanzia juzii anampigiaa cm huyu x wake akitaka warudiane na machozii anatoa.kwa vile niko mbalii na huyu binti jamaa inakuwa kama kingezo,na jamaa ananijua na tunawasiliana bfr and after kuachana na huyu gal ambe ndo wangu sasaa. je kwa halii hii wakuu mnanishaurii nini?
 
Kuwa mpole tu kijana uone mambo yatakavyoenda siunajua penzi alilazimishwi...so kama anakupenda atabaki kwako kama atarudi kwa x wake ujue anampenda yule...patience pays
 
Mwanamke ambae yupo vulnerable hasa kuhusiana na mambo ya mapenzi, mara nyingi huelemea kule ambako anaona she is needed/loved most; Na hio atajudge tokana na vitendo vya wahusika.... IMO Ukibweteka sio wako tena, it si beta ugangamale so that you know you tried hata akikubwaga... After all you claim mwapendana.
 
Mwache mdada amue nini anataka kama anaakili timamu anajua umuhimu wako na kama bado wali maharage usijute kwanini umemkosa sababu nusu shari kuliko shari kamili.....pole sana ndio ukubwa ukisikia kua uyaone ndio hayoooooooooooo.....
 
Kwa hili sitashangaa kuona huyo mwanamke analudi kwa jamaa yake...wewe akikuacha solemba..
Ujue kuna baadhi ya wanawake anaweza akawa na wewe ili kupooza moyo wake ama kumlipizia mwanaume wake aliyemfumania....
Pia anaweza akawa amekuja kwako just kwaajili ya Kuchukizwa na mwenzake(Boy),sasa hapo usifikilie umempata.....kesho hasila zimekwisha huyo anaanza kuwasiliana na jamaa yake....
Chunguza sana hapo.....
 
Mwenye maamuzi ya mwisho juu ya mustakabali wa mahusiano yenu ni mwanamke mwenyewe.Akiamua kumgomea huyo jamaa anaelialia machozi basi picha litaendelea.Akiamua kurudi kwa huyo jamaa yake basi filamu inaishia hapo.Mwache mwenyewe awe stering wa picha,lakini kuwa makini sana maana mwanamke ni kiumbe mjanja sana!Anaweza akawa anakula tonge mbilimbili wakati wewe unamega mojamoja bila kujua!
 
kaa pembeni jiepushe na msongamano! yasijekukukuta yalomkuta kibwetele! mdada ndo mwenye maamuzi yote,kama kweli anakupenda utaona!
 
nashukuru sanaa kwa mawazo yenu wakuu,ilaa chaa kushangaza mwanamke bado anani call na kusisitizaa kwamba hana feeling tena na jamaa,but kitu kimojaa ninacho shangaa tulipanga tuonane tarehe za mbelee mwezi huu kwa vile niko mbali,nimemwambia nimfate amesema yeye anataka kujaa huku,but now nikimuuliza kuhusu hiyo safari ananipaa visingizo kibao au hataki kuongelea.its so pain...cse i was real inlove na nikajitulizaa,nikawa gentlemen staki kumcheat cse yuko mbalii,nikaacha starehe zangu zote ni mrizishe
 
Mwache achague mwenyewe anamtaka nani.
Unachoweza kufanya ni kumwonyesha tu kwamba ni kwa kiasi gani unampenda na kumwacha afanye maamuzi yake!
 
Kwa kuwa mkuu ulishapigwa chini na huyo mdada kwa sababu ya huyo huyo mkaka, nafikiri uwezekano wa kuwa unapendwa ni mdogo sana. Kukubaliwa kwako kwa sasa ni kwa kuwa alikuwa hana pa kwenda na alikuwa anatafuta faraja baada ya kutendwa. Ni vzr kufikiria maamuzi yako kwa upya.Ila unaweza pia kuusoma uhusiano wa huyu mdada na huyo X wake anapopigiwa simu kama anazichukulia positively au laa na pengine kumsoma kupitia kwenye mazungumzo yenu juu ya huo uhusiano mpya unaozuka. From there unaweza kuwa na maamuzi sahihi ya kufanyaPole mkuu.
 
inaonyesha mlikuwa mnakula wote na jamaa
ukiweza endeleza hiyo hiyo,
mtakapokutana wote kwenye giza ndipo utakapoamua.
 
Kwa kuwa mkuu ulishapigwa chini na huyo mdada kwa sababu ya huyo huyo mkaka, nafikiri uwezekano wa kuwa unapendwa ni mdogo sana. Kukubaliwa kwako kwa sasa ni kwa kuwa alikuwa hana pa kwenda na alikuwa anatafuta faraja baada ya kutendwa. Ni vzr kufikiria maamuzi yako kwa upya.Ila unaweza pia kuusoma uhusiano wa huyu mdada na huyo X wake anapopigiwa simu kama anazichukulia positively au laa na pengine kumsoma kupitia kwenye mazungumzo yenu juu ya huo uhusiano mpya unaozuka. From there unaweza kuwa na maamuzi sahihi ya kufanyaPole mkuu.
nime kuelewaa mkuu...asante
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom