Wizi waibuka Bandari Dar- Magari yachomolewa vifaa

Hii VIR (Vehicle Inspection Report) Inaandikwa pale gari ikitoka melini na Chief officer au Captain wa meli huisaini kukubali ya kuwa hilo gari hivyo vitu vilivyoandikwa vipo au vimemiss.

Mteja wakati wa kuchukua gari lake kabla ya kuanza kuitupia lawama mamlaka ya bandari, inampasa kwanza kuangalia VIR kama wakati gari linashuka walirekodi kama redio, au power window n.k je vilikuwepo wakati wa upakuzi kutoka melini au la! VIR ndio itakupa majibu.
Kama havikuandikwa wakati gari linashuka, maana yake vimekwapuliwa huko huko melini. naomba udeal na transport wako.
Na kama VIR inaonyesha gari imeshuka na vifaa vyote wakati wa kulichukua gari lako unaona kuna vitu hamna basi wewe lia na Bandari.

Kabla gari haijafika hapa nchini kuna Bandari kadha wa kadha meli inapita, sasa basi mfano imepita Cape town, au Mombasa kabla ya kuja huku nchini, na wakati wa upakuzi wakakwapua kule wakati wakitoa magari ya kwao na wale ma Crew wa meli hawakuwa makini....! huwezi jua

Ection zinachukuliwa sana tu na Usiwe mnyonge fuatilia haki yako ukweli utajulikana tu, na hatua zinachukuliwa juu ya wote wanaosababishia Bandari kila siku inatupiwa lawama

Wateja huchukua magari yao kutoka bandari kavu. Wanaoshusha magari toka melini ni wafanyakazi wa bandari. Hao ndio wenye dhamana ya kuhakikisha kwamba gari imeteremka ikiwa salama au baadhi ya vifaa vimekosekana. Cha kushangaza mtu anapopokea gari hakuna vielelezo vyo vyote kuhusu upotevu au usalama wa gari isipokuwa tu makabidhiano ya gari toka bandari kavu waka limeshapitia mikono ya wengi. Hapo kuna walakini katika utendaji katika bandari yetu. Vigumu Japan kuipa vifaa kama inavyofanyika Dar, hali kadhalika bandari za uarabuni au ulaya, mtindo huu ni bandari za hapa Afrika.
 
Nilikuta gari moja inavuta magari matatu kupeleka bandari kavu na ikapata ajali. Nilijiuliza alijiaminije kuvuta magari ma3 na maaskari huko njiani walikuwa wanawaruhusu vipi wapite? Je wenye magari hayo walipofikia kuyatoa waliambiwaje? Uchunguzi wangu wa haraka nilipouliza katika eneo la tukio niliambiwa magari yalikuwa yanapelekwa Farion ambayo ni bandari kavu.
 
Tatizo Muda wa kufuatilia. Wizi unazidi
Tu ukiibiwa nenda mnadani utaipata
Hata Polisi wanajua ila Again Who cares?
 
Wateja huchukua magari yao kutoka bandari kavu. Wanaoshusha magari toka melini ni wafanyakazi wa bandari. Hao ndio wenye dhamana ya kuhakikisha kwamba gari imeteremka ikiwa salama au baadhi ya vifaa vimekosekana. Cha kushangaza mtu anapopokea gari hakuna vielelezo vyo vyote kuhusu upotevu au usalama wa gari isipokuwa tu makabidhiano ya gari toka bandari kavu waka limeshapitia mikono ya wengi. Hapo kuna walakini katika utendaji katika bandari yetu. Vigumu Japan kuipa vifaa kama inavyofanyika Dar, hali kadhalika bandari za uarabuni au ulaya, mtindo huu ni bandari za hapa Afrika.
Tena hao wa bandari kavu ndio wezi na wana njaa, kama unajua document muhimu kama ipo kwa ajili ya makabidhiano, unashindwa vipi kuichukua kutoka manifest.?
Hao waongo wao ndio wanakwapua alafu wanaisingizia mamlaka ya bandari. Sio kama nawatetea sana bandari, nao wana udhaifu wao lakini taratibu zao ziko.
Na ikitokea bandari VIR yao inaonyesha mfano power window hamna na wakati VIR ya gari ilikotoka inaonyesha ipo, hapo ndio chief officer panakuwa hapatoshi kusign mpaka wakala anaingilia kati kuweka suluhu.
 
Back
Top Bottom