Wizi ulikithiri DSM Container Terminal - Bandarini

Sep 29, 2011
92
18
Kumekuwa na wizi mbalimbali bandarini ikiwemo Kontena 4 za shaba zenye thamani ya million 900, Kontena hizi zilitakiwa zisafirishwe nje ya nchi lakini zikaibiwa na hazijulikani zilipo.

Ukweli ni kwamba kontena hizi zimeibiwa pale TICTS na kusafirishwa kwenda destination ingine. TPA, Police na walinzi binafsi mnahakikishaje usalama wa mali za watu.

Hii ni wazi kuna viongozi wa TICTS wanahusika pamoja na walinzi. Polisi msinganganie kutuliza chadema badala ya kulinda njia za uchumi kama bandarini.

Kuna ufisadi mkubwa sana Container terminal kwani kuna mtu anawadai gharama za mali yake ya tumbaku kavu ambayo ilitakiwa isafirishwe kwenda UK na wao wakaichelewesha hata iliposafirishwa ilikosa ubora kule UK.
 
Shehena ya mizigo yaibwa Bandari Dar

Mwandishi Wetu | Toleo la 253 | 8 Aug 2012


Dar-es-Salaam-Port.jpg



HALI ya usalama wa bidhaa zinazoingizwa nchini kupitia Bandari ya Dar es salaam, hususan katika Kampuni ya Kupakia na Kupakua Mizigo (TICTS), si ya kuridhisha na baadhi ya wafanyabiashara wameanza kuikimbia bandari hiyo na kuanza kutumia Bandari ya Mombasa, nchini Kenya, Raia Mwema limebaini.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili unathibitisha kwamba wafanyabiashara wengi tayari wamesitisha kupitishia bidhaa zao kupitia Tanzania, kwa kuhofia wizi huo unaoonekana kukubuhu bandarini hapo.

Hali hii inaonekana kuwaathiri zaidi wafanyabiashara kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambao wengi wao hivi sasa wanapitishia mizigo ya katika Bandari ya Mombasa.

Wafanyabiashara hao ambao wengi ni kutoka maeneo ya Bukavu nchini Kongo, kwa nyakati tofauti wamethibitisha kuathiriwa na wizi katika Bandari ya Dar es Salaam.

Mbali na wafanyabiashara hao kutoka Bukavu, wengine ni kutoka maeneo ya Lubumbashi ambao nao wameikimbia Bandari ya Dar es salaam na kuamua kupitishia mizigo yao nchini Afrika Kusini na katika Bandari ya Beira, nchini Angola.

Akizungumzia hali hiyo, Bernard Makita, ambaye ni mmoja wa maofisa kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, ambaye pia ni mwakilishi wa Kampuni ya Serikali ya OGEFREM (sawa na Sumatra Tanzania) anasema hali hiyo ni hatari kwa uchumi wa nchi.

"Ndugu mwanadishi ni bora kama wafanyabiashara hao wamechukua jukumu hilo kwani mambo yanayofanyika katika Kampuni ya TICTS yanakatisha tamaa kwani wizi, ubabe usiokuwa na msingi vimetawala katika kampuni hiyo," alisema Makita kwa masikitiko.
Alionya kuwa, kama hali hiyo haitafanyiwa kazi na kuiachia kampuni hiyo ya kigeni kufanya watakavyo, bandari hiyo inaweza kufungwa kwa kukosa wateja na hivyo kuhatarisha uchumi wa taifa hili.

Kwa upande wake, Faines Kiwia, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TRIPLE. D. inayojishugulisha na utoaji wa mizigo ya wafanyabiashara bandarini kwa miaka mingi, alisema hali ya wizi wa mizigo imefikia kiwango kibaya kiasi cha kuikosesha serikali mapato kwa kiwango kikubwa.

Katika mazungumzo yake na mwandishi wa habari hii, mkurugenzi huyo mtendaji akatolea mfano wa makontena yanayodaiwa kupotea mikononi mwa TICTS. Katika upotevu huo, inadaiwa kuwa kontena moja lilikutwa kwenye kambi moja ya jeshi nchini likiwa tupu na jingine kukutwa maeneo ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, likiwa tayari limekwisha kufunguliwa.

Alidai kuwa kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, kuna upotevu wa makontena takriban 40 ya wafanyabiashara kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Makotena hayo yamepotea ‘mikononi' mwa Kampuni ya TICTS.

Mwandishi wa gazeti hili alipofanya jitihada za kuwatafuta wasemaji kutoka TICTS ili kuzungumzia tuhuma zinazoelekezwa katika kampuni hiyo, jitihada hizo hazikuzaa matunda, kama ilivyokuwa kwa juhudi zilizofanyika ili kuwapata viongozi wa Mamlaka ya Bandari kuzungumzia malalamiko hayo ya wafanyabiashara. Hata hivyo, juhudi hizo zinaendelea.
 
....Duuh! Inamaana hatua mbadala za UDHIBITI wa hali hii hakuna kabisa kabla nchi zingine ambazo ndiyo wateja wetu kuendelea kuwabakisha....

Je, serikali itajisikiaje pale tu bandari yake kuu itakapokimbiwa na hao wachache waliobaki?
 
1.jpg


Matumaini yangu ni kuwa Waziri Mwakiembe ataweza kulifanyia kazi tatizo hili, kwani ameanza kazi hiyo karibuni na mlolongo wa matatizo ni mengi, ameanza na tatizo la kupunguza msongamano wa usafiri kwa kusimamia uanzishwaji wa commuter reli jijini Dar.

Atakaposikia hilo natumaini ataenelekeza nguvu huko na kwa kweli wakae chonjo sasa hivi, huyu waziri anaonekana kuwa msikivu.
 
We are never serious.

Familia yangu ilikuwa na mipango ya kupitishia mizigo yetu pale lakini tumesitisha, licha ya tishio la wizi huo, mwanzoni mwa mwaka huu nilipitishia pale kamzido taabu niliyopata katika kukatoa kamzigo hako ni mwezi mzima wakati ingekuwa ni masaa tu. Ulimbukeni huu wa bandari ya Darisalama ni nuksi kabisa bora tuwanufaishe wakenya.
 
Hao wafanyabiashara wanatakiwa waishitaki hiyo kampuni ya TCIST kwa uzembe uliosababisha kuibiwa kwa makontena yao.

Bandari ya Mombasa ndio inayoaminika kwa sasa na mizigo yote ya maana inapitishwa hapo kwenda Tanzania na kwingine Africa.

Ni kwamba watu hawataki tu kupoteza muda kufuatilia kesi lakini wizi bandarini Dar-es-Salaam umekithiri na kila mtu amejua kula vya bure basi imekuwa ni kawaida.
 
Hao wafanyabiashara wanatakiwa waishitaki hiyo kampuni ya TCIST kwa uzembe uliosababisha kuibiwa kwa makontena yao.

Bandari ya Mombasa ndio inayoaminika kwa sasa na mizigo yote ya maana inapitishwa hapo kwenda Tanzania na kwingine Africa.

Ni kwamba watu hawataki tu kupoteza muda kufuatilia kesi lakini wizi bandarini Dar-es-Salaam umekithiri na kila mtu amejua kula vya bure basi imekuwa ni kawaida.

Mtu umepoteza mali zako na unapodai haki unatakiwa tena utoe cho chote vinginevyo utazungushwa wee hadi unakata tamaa. Inasikitisha kana kwamba hatuna vyombo husika kufuatilia hilo wakati malalamiko yapo kila wakati.

Magari yanayotolewa bandarini na kupelekwa bandari kavu utakuba matairi yamebadilishwa na kuweka mabovu, radi zimechomolewa, speaker hazipo, spare-tire hakuna na mengine mengi wakati gari hiyo imehakikiwa kuwa salama wakati linaingizwa bandarini huko majuu.

Karibuni nimetoa gari pale nimeona head rests za passenger in the back seat of the car hakuna, kujaribu kuulizia nimeona napoteza muda wangu na gharama kuliko gharama ya head rests
 
Mtu umepoteza mali zako na unapodai haki unatakiwa tena utoe cho chote vinginevyo utazungushwa wee hadi unakata tamaa. Inasikitisha kana kwamba hatuna vyombo husika kufuatilia hilo wakati malalamiko yapo kiwa wakati.

Magari yanayotolewa bandarini na kupelekwa bandari kavu utakuba matairi yamebadilishwa na kuweka mabovu, radi zimechomolewa, speaker hazipo, spear tire hakuna na mengine mengi wakai gari hiyo imehakikiwa kuwa salama wakati linaingizwa bandarini huko majuu.

Karibuni nimetoa gari pale nimeona head rests za passenger seat ha hakuna, kujaribu kuulizia nimeona napoteza muda wangu na gharama kuliko gharama ya head rests

Matatizo yako ni moja ya matatizo ya watu wengi tunaotumia bandari hiyo.

Mimi nilituma gari aina ya Land Rover Freelander na humo ndani nikaamua kuweka 20 laptops ambazo zingenisaidia kupata pesa ambazo ningetumia kwa mambo mengine.

Laptops hizo nilizieleza kabisa kwenye manifest idadi yake na matumizi yake.

Gari lilipofika bandarini Dar-es-Salaam na lilipotolewa wiki tatu baadae sikukuta laptops na kioo kimoja kidogo cha sehemu ya nyuma kilikuwa kimevunjwa na hakukuwa na maelezo ya kutosha.

Kwahio wizi upo sana na umezoeleka ila ni pale utakapofanyika usafi wa kuondoa kila aina ya uovu huu ndipo sehemu hiyo itakuwa ya maana.

Wapo watu wengi tu ambao mitaani wanaabudiwa kwa kuonekana wa maana lakini kumbe ni wezi kule bandarini.
 
Matatizo yako ni moja ya matatizo ya watu wengi tunaotumia bandari hiyo.

Mimi nilituma gari aina ya Land Rover Freelander na humo ndani nikaamua kuweka 20 laptops ambazo zingenisaidia kupata pesa ambazo ningetumia kwa mambo mengine.

Laptops hizo nilizieleza kabisa kwenye manifest idadi yake na matumizi yake.

Gari lilipofika bandarini Dar-es-Salaam na lilipotolewa wiki tatu baadae sikukuta laptops na kioo kimoja kidogo cha sehemu ya nyuma kilikuwa kimevunjwa na hakukuwa na maelezo ya kutosha.

Kwahio wizi upo sana na umezoeleka ila ni pale utakapofanyika usafi wa kuondoa kila aina ya uovu huu ndipo sehemu hiyo itakuwa ya maana.

Wapo watu wengi tu ambao mitaani wanaabudiwa kwa kuonekana wa maana lakini kumbe ni wezi kule bandarini.

Kila kona kumejaa uchovu tu, hata wale maajengi watoa mizito bandarini utafikiri wanamawasiliano na wizi, kwani wanakuzungusha kutoutoa mzigo au gari haraka, wanachelewesha kwa makusudi ili mission zao zikamilike ndio watoe mzigo na utakapoupata ni kasoro nyingi tu ya kukosekana vitu vingi tu.
 
Back
Top Bottom