Wizara ya Maliasili na Utalii tengenezeni maelezo sahihi ya kuwaeleza watu wanaotembelea vivutio vyetu mfano "Mapango ya Amboni"

Singo Batan

JF-Expert Member
Apr 24, 2020
292
191
Wiki kadhaa zilizopita nilipata nafasi ya kupeleka familia katika mapango ya AMBONI - TANGA. Eneo ambalo vijana wetu walio shuleni wanalisikia na kusoma sana taarifa zake katika somo la jiografia (physical geography).

Binafsi pamoja na kusoma darasani miaka mingi iliyopita sikuwahi kufika na kuona hizo features tulizokuwa tunafundishwa na kuziona vitabuni au kuchorewa ubaoni na walimu wetu na inawezekana hata Mwalimu wangu alokuwa ananifundisha nae kasimuliwa tu (Tatizo la mfumo wa elimu yetu). Lakini nilipofika Amboni matarajio yangu yalikuwa huu ni kupata maelezo ya kitaalamu na yenye kuakisi uhalisia kuhusu mapango hayo. Pamoja na kukutana na vijana wanaojitolea kufanya kazi pale, wanaotoa maelezo kuhusu mapango yale na kwakweli maelezo yao mazuri sana yenye kuchagizwa na uongo wa hapa na pale nimeshawshika kushauri Wizara itengeneze maelezo sahihi yanayopaswa kutolewa kwa watalii.

Taifa letu kwa sasa halihitaji kusaidiwa kila kitu na wazungu. Wasomi na wataalamu wa masuala hayo ya utalii na elimu wanaweza kukaa pamoja na kutengeneza muongozo wa taarifa zenye ukweli na za kitaalamu ili vijana wale wanaofanya kazi kubwa ya kueleza kuhusu vivutio vilivyomo Amboni na hata maeneo mengine watumie matini hizo.
Nitatoa mifano;

1. Tukiwa katika Pango la kwanza, Muongozaji alisema hapo nje kuna ramani ya Afrika na mfano wa sanamu ya Simba (Huo ni UONGO) ni taarifa ya kufikirika kama watu wengi tulivyozoeshwa na watengeneza habari wanaposema, mawingu yametengeneza picha mara ya Yesu, mara Afrika nk.

2. Kule ndani tukaambiwa kuna njia ya uzima, kuna feature ya kibra ikihusisha masuala ya imani kuhusu dini ya kiislamu, kuna feature ya bikira maria ikihusishwa na imani ya ukatoliki, kuna mfano wa mlima Kilimanjaro nk. Maneno mengi hapo ni ya UONGO na yanakinzana kabisa na elimu inayotolewa huko shuleni. Elimu ya darasani inasema yapo Maumbo mbalimbali yanayotokea wakati wa mchakato wa kijiolojia, maumbo hayo aghalabu yana shepu na mionekano ya kuvutia (hakuna dini inayotengeneza maumbo yale mle ndani)

3. Tunasisitiza kuhusu kiswahili, ingefaa Wizara ilete majina ya kiswahili ya maumbo kama vile Natural pillars, Stalactites, Stalagmites nk kufikiri kwa lugha ya kitumwa kulitokana na mfumo wa kiutumwa tuliojengewa na wakoloni kunatufanya tusimulie masuala yetu kwa lugha ya watwana na kukosa umiliki wa rasilimali zetu. Tunapaswa kubadilika!

4. Kuna imani inajengwa kwamba katika mapango hayo kuna pango lina jinsia ya kiume na jingine lina jinsia ya kike jambo ambalo ni UONGO kabisa.

Wizara na wataalamu ya jiografia ni muda sasa wa kutengeneza historia yetu, elimu inayosadifu mazingira yetu kwa mahitaji yetu. Wageni wakija waione fahari ya TANZANIA sio fahari ya uongo wa wazungu iliyopandikizwa vichwani mwa watanzania.
View attachment 2403080View attachment 2403079
 
Back
Top Bottom