Wizara ya afya imeshindwa kazi yake...?

kipindupindu

JF-Expert Member
Dec 16, 2010
1,053
170
Kuna msemo wa kiswahili unasema "usipoziba ufa utajenga ukuta"

inasikitisha kuona maelfu ya watanzania wakipoteza imani kwa matibabu yanayotolewa na hospitali hususani kwa magonjwa sugu kama kisukari,high blood preassure,ukimwi,vidonda vya tumbo n.k.

Kumekuwepo na wimbi kubwa la waganga wa jadi, wachungaji na mashekhe ambao hujitokeza na kujinadi kutoa tiba za magonjwa haya.

Kumekuwepo vipindi maalum kwenye radio na T.v vinavyoelezea ''KWA KUPOTOSHA'' jinsi magonjwa haya yavyotokea na jinsi tiba zao zinavyofanya kazi.

Mifano ni mingi sana,mama teri,dr ndodi, mch.kakobe na sasa Babu wa loliondo.

Natambua uwepo na umuhimu wa tiba mbadala lakini inasikitisha wizara ya afya kufumbia macho upotoshaji unaofanyika kwenye vyombo vya habari kwa mwamvuli wa tiba mbadala.

Mamlaka kama baraza la madaktari,bodi ya wafamasia,TFDA ziko wapi?kwa nini hazina nguvu ya kutoa maelekezo sahihi?au ndio mko kifisadi zaidi.

Kwa kuendelea kulea upotoshaji leo hii janga (crisis)limetokea,watu wapatao 6000 wakiongozwa na mawaziri, wabunge na wakurugenzi wamejazana kule loliondo wakipata sips za dawa ya ajabu,mlishindwa kumzuia kakobe na ndodi(kuziba nyufa) kamwe hamtaweza kumzuia BABU wa loliondo.
Kwa sasa wizara itakuwa na kazi kubwa(kujenga Ukuta) ya kurudisha trust ya watanzania juu ya matibabu ya magonjwa sugu.

Uzembe huu wa kuwafumbia macho watu waenezao uvumi ulipelekea Nigeria kuwa kati ya nchi zilizoshindwa kutokomeza polio duniani.

Endeleeni kukaa kimya tu huku watu wakipoteza maisha kwa kusitisha matibabu ya kisukari,hypertension na ukimwi.

Ni mimi,
mdau wa afya
kipindupindu.
 
Umesema yote. In a country where a witch doctor can become a member of parliment what do you expect?

dont be surprised if this witch doctor becomes a minister of health. These are very important people to Mr President, they are among people ensuring his survival in the political arena.

Nothing gonna happen to them, people will continue dying no body cares as long as they (leaders) are getting what they want.
 
Kuna msemo wa kiswahili unasema "usipoziba ufa utajenga ukuta"

inasikitisha kuona maelfu ya watanzania wakipoteza imani kwa matibabu yanayotolewa na hospitali hususani kwa magonjwa sugu kama kisukari,high blood preassure,ukimwi,vidonda vya tumbo n.k.
Kumekuwepo na wimbi kubwa la waganga wa jadi,wachungaji na mashekhe ambao hujitokeza na kujinadi kutoa tiba za magonjwa haya.kumekuwepo vipindi maalum kwenye radio na T.v vinavyoelezea ''KWA KUPOTOSHA'' jinsi magonjwa haya yavyotokea na jinsi tiba zao zinavyofanya kazi.mifano ni mingi sana,mama teri,dr ndodi,mch.kakobe na sasa Babu wa loliondo.
Natambua uwepo na umuhimu wa tiba mbadala lakini inasikitisha wizara ya afya kufumbia macho upotoshaji unaofanyika kwenye vyombo vya habari kwa mwamvuli wa tiba mbadala.mamlaka kama baraza la madaktari,bodi ya wafamasia,TFDA ziko wapi?kwa nini hazina nguvu ya kutoa maelekezo sahihi?au ndio mko kifisadi zaidi.
Kwa kuendelea kulea upotoshaji leo hii janga (crisis)limetokea,watu wapatao 6000 wakiongozwa na mawaziri,wabunge na wakurugenzi wamejazana kule loliondo wakipata sips za dawa ya ajabu,mlishindwa kumzuia kakobe na ndodi(kuziba nyufa) kamwe hamtaweza kumzuia BABU wa loliondo.
Kwa sasa wizara itakuwa na kazi kubwa(kujenga Ukuta) ya kurudisha trust ya watanzania juu ya matibabu ya magonjwa sugu.

Uzembe huu wa kuwafumbia macho watu waenezao uvumi ulipelekea Nigeria kuwa kati ya nchi zilizoshindwa kutokomeza polio duniani.

Endeleeni kukaa kimya tu huku watu wakipoteza maisha kwa kusitisha matibabu ya kisukari,hypertension na ukimwi.

Ni mimi,
mdau wa afya
kipindupindu.

kipindupindu ni kibaya jamani.
 
Kwa watoto au vijana wanaotumia sindano ku-control sukari yao ni hatari mno kumwambia aache sindano zake kwa siku 14, naamini wataalamu wa wizara ya afya wanafahamu hatari kama hizi lakini wanashindwa kutoa matamko makali dhidi ya upotoshaji unaoendelea nchini.
 
Nashukuru kwa kauli iliyotolewa na naibu waziri wa afya katika siku ya T.B duniani.
 
Japo ni vigumu kuzuia imani na hisia za watu, kwa kweli nakuunga mkono kwamba serikali, kupitia wizara ya afya, ingetoa tahadhali na maangalizo kwa bidii.

Nina hakika ingewaokoa baadhi ya hawa watu kutokana na madhara yanayowakabili wanapoacha dawa za kawaida.
 
Japo ni vigumu kuzuia imani na hisia za watu, kwa kweli nakuunga mkono kwamba serikali, kupitia wizara ya afya, ingetoa tahadhali na maangalizo kwa bidii. Nina hakika ingewaokoa baadhi ya hawa watu kutokana na madhara yanayowakabili wanapoacha dawa za kawaida.

goverment kupitia wizara ya afya ina wajibu ya ku-play central role,inawajibika kuweka muongozo wa matibabu(standards),isipofanya hivyo kila siku yataibuka matibabu feki au yale yanayotishia afya za binadamu.
 
Kweli hii ni hatari, tusubiri matokeo miezi michache tuone, maana wengine baada ya kupata kikombe wameacha hata kutumia dozi zao za ARV.
 
Back
Top Bottom