Wilaya ya Ukerewe iwe mkoa

zacha

JF-Expert Member
Feb 28, 2009
1,189
1,828
Wakuu! Wilaya ya Ukerewe ni walaya ambayo iko ndani ya mkoa wa Mwanza, Wilaya hii kutokana na utajiri wake wa maliasili, Ziwa, Mistu Minene, Ardhi yenye rutuba na Vivutio vingi tu vya utalii.
Wilaya hii ina Kata Zifuatazo:-

Bukanda • Bukiko • Bukindo • Bukongo (Ukerewe) • Bukungu • Bwiro • Bwisya • Igalla • Ilangala • Irugwa • Kagera (Ukerewe) • Kagunguli • Kakerege • Mukituntu • Muriti • Murutunguru • Nakatunguru • Namagondo • Namilembe (Ukerewe) • Nansio • Nduruma (Ukerewe) • Ngoma (Ukerewe) • Nkilizya • Nyamanga

Kutoka na utajiri huu wa wa Wilaya hii ya Ukerewe, wananchi wa wilaya hii wamekuwa na umaskini wa hali ya juu ikiwa kwamba hamna mbinu mbadala kutoka kwa kiongozi wao ambaye nd' mwakilishi wao Bungeni, kumekuwepo na ukosefu wa huduma muhimu za kijamii kama Zahanati, Shule na Miundo mbinu Mibovu.

Eneo la wilaya hii iko kwenye visiwa ndani ya ziwa Viktoria Nyanza hasa visiwa viwili vikubwa vya Ukerewe na Ukara pamoja na visiwa vidogo.

Hivyo kutokana na na idadi hii ya watu Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 261,944. Hivyo kutokana na idadi hiyo ya mwaka 2002 ningeomba hii wilaya iwe mkoa ili wakazi wa wilaya hii wapate huduma muhimu kutoka serikali kuu, kwani hudumu nyingi zimekuwa zikiishia Mwanza mjini na Nansio mjini

Kuna vivutio vingi tu vya utalii kama Halwego Handebzo, Jiwe la ukara n.k hivi vyote Mwakilishi wa jimbo hilo ameshindwa kuviendeleza, ikiwa kama vikiendelezwa vyema basi wakazi wa maeneo hayo na ya jirani watafaidika kwa namna moja au nyingine, kiuchumi na kijamiii pia
Na hili haya yote yakamilike vyema basi inabidi hii wilaya iwe Mkoa kama ilivyomikoa mingine ya Tanzania ili iwe rahisi kutimiza malengo haya!.
 
Katika orodha ya kata hizo mbona Ukara haimo?

Hoja yako ni sahihi kwa vile Ukerewe ni kisiwa na ukilinganisha ukubwa wa visiwa vingine kama Unguja (mikoa 3) na Pemba (Mikoa 2). Hata hivyo usiwe mwanzo wa kudai kutambuliwa kama Taifa huru la Ukerewe.
 
Kuna vigezo hutumika kuanzisha Mkoa mpya, nadhani hivyo ndio vinafaa kuangaliwa. Sio kulinganisha na mikoa ya Zanzibar (ikumbukwe Zanzibar ni nchi iliyoungana na Tanganyika). Ni kweli Ukerewe hali ya maisha ya watu wake iko chini, lakini hicho sio kigezo cha kuifanya iwe Mkoa, kama umetembelea maeneo mengi ya Tanzania utakubaliana nami hali ni hiyo hiyo. Muhimu ni vipi twaweza kutumia rasilimali zetu kuinua hali za wananchi.
 
Jasusi,
Wasu nja kisi. Shukrani kwa kulipenda jina lako, ila la kwako mh, linatisha!.
 
Yes, ni kweli kabisa!!! kwa hiyo tulawaka, tarime, mirerani, buzwagi zoooote chapa mikoa tu ili watu watajirike!!! ukiona sehemu maskini we chapa mkoa tu au siyo??? au tureview hii mikoa halafu tuunde upya nini???

 
Back
Top Bottom