WikiLeaks na JamiiForums ni vyombo muhimu

Status
Not open for further replies.

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Mikataba yote ya UFISADI DUNIA NZIMA inawekwa hapa:

http://wikileaks.org/wiki/Wikileaks

Wikileaks, a wiki-based information clearinghouse for whistleblowers that TIME said "... could become as important a journalistic tool as the Freedom of Information Act.", has had their .org domain taken offline due to an illegal court order out of California. The court took them offline because they leaked files documenting many rich, powerful people in the United States, some of them running for president, using offshore banking to evade taxes.
IMETOLEWA AMRI JANA NA JAJI KULE USA IWE SHUT DOWN KWANI KUNA THOUSANDS OF DOCUMENTS ZA SWISS BANK ACCOUNTS ZILIMWAGWA HUMU NA ZINGINE ZA CAYMAN ISLANDS LAKINI ALTERNATIVE NI HIZI HAPA:

http://wikileaks.la/wiki/Wikileaks


Sasa serikali ya Tanzania ina option:

Either iendelee kuwatisha watu au ishirikiane na online community kupata ufumbuzi wa matatizo ya wasio na uwezo wa kutumia hizi computers.

Kwanza kabisa naona kuna atmosphere ya FEAR ishaingia humu na I can understand kwa nini hili linatokea. Serikali inaona inalose hii vita dhidi ya internet na sitoshangaa kama hii website ikiwa shut down sasa naona bora kuwepo kwa PLAN B

Kwanza kila mmoja humu afungue anonymous blog ambayo atakuwa anweza upupu na leaks zake bila kumoderate kitu

Wana JF inabidi tuachane na kuthink local...we need to think Global na kama mnataka kutia preassure iwepo TRANSPARENCY serikalini inabidi mulobby kwa international pressure groups ambazo nyingi hawajui KISWAHILI sasa hebu kwa wenye uwezo tengenezeni na zingine zenye Kiingereza kisha mnaweza kuzilink na organizations kama TRANSPARENCY INTERNATIONAL etc

Nashauri kama kuna mtu katishwa basi msipate tabu nyie wekeni majina yao, rank zao na kituo gani wanatoka kisha tuone kama wanaweza kuishut down dunia nzima

Mwisho nashauri mtembelee hii WIKILEAKS kwani jana naona Federal Judge ametoa amir iwe shut down lakini kwa walionje ya USA mambo safi kuna mikataba yote ya UFISADI DUNIA NZIMA
 
Gt, Duh si utani mzee yaani umegonga pale pale penyewe regarding the issue ya future ya JF... On the other hand, I salute Mkuu kwenye hizo links umetoa....
 
Mkuu GAME
Post yako ina akili sana na ninaamini kuwa INAWEZEKANA yote uliyoyabashiri kutokea au isitokee, ila one thing iliyonipa faraja sana ni altenative ya kuwe na plan B. Man una uzalendo sana kwa nchi yetu.
Nenda PM nina ujumbe mahsusi wa kufanyia kazi mkuu
 
hESHIMA YAKO MZEE. WATAJITAHIDI KUZIBA LAKINI LAZIMA TUONGEE NA PA KUONGELEA NI HAPA JF,HABARI ZA HAPA WANAZIITA NI ZA MTAANI,LAKINI WE STILL SEE WHAT WE TALK HERE HAVE TRUTH IN IT
 
The same day nilipopost hizo links hapo juu wakaamua kuifunga JF

Hivi kwa nini wasishirikiane nasi badala ya kutafanya hivi?
 
Mkuu GAME THEORY mimi naunga mkono hasa hii ishu ya kuwa na bloggs za kiingereza maana wazimbabwe hii imesaidia sana kuexpozi internationally nini kinaendelea nchini kwao na kumekuwa na international pressure ya nguvu ambayo bongo tungechapwa nayo serikali haiwezi kusavaiv miaka 2. Well pamoja na kwamba so far bado mwanga hauonekani mwisho wa tanuru!!!!!!!!!!

Lakini Bob in some way ameanza kudata na kufikiria namna ya kujinasua!!!!!
 
Admin,

Naomba tuwe na thread za siasa mara mbili, Mara ya kwanza iwe Kiingereza na nyingine iwe swahili. Ya kiingereza tuta i Link na websites za dunia nzima kama wikileaks ya kiswahili tutabakia nayo wenyewe.

Huu ni mkakati wa kuhakikisha kuwa JF inajulikana dunia nzima.
Pia docs zote zilizopo JF za kiingereza tuziweke kote, ili hata kama JF ikiwa down ziendelee kuwepo!

Thanks

FD
 
Leo hii kwenye majira ya saa sita mchana katikati ya jiji la London, mkurugenzi wa mtandao wa habari za uchunguzi ujulikanao Wikileaks bwana Julian Assange alikuwa alikutana na waandishi mbalimbali wa habari kujibu maswali kuhusu taarifa za ndani za kijeshi za Marekani ambazo mtandao huo imezichapisha mtandaoni.

Ni taarifa zaidi ya 90,000 kutoka ndani ya taarifa zaidi ya 150,000 ambazo nazo ni sehemu ya taarifa 1,000,000 ambazo mtandao huo inazo kwenye server yake.

Lengo la Wikileaks ambayo ina ushirikiano na magazeti ya Guardian la Uingereza, New York Times la Marekani na Der Spieger la Ujerumani ni kuonesha kiwango cha vita nchini Afghanstan kilivyo na uendeshaji wake na kwamba taarifa za vifo vingi vya raia wasio na hatia wa Afghanstan zinakuwa zinazuiwa kuchapishwa.

Ndani ya taarifa hizo za ndani ni pamoja na:

1. Marekani inatumia vikosi vya siri (special forces) kuwatafuta na kuhakikisha wanakamata au kuua viongozi wote wa Taliban na washirika wao bila kuhusisha mahakama.

2. Kwamba idara ya ujasusi ya Pakistan (ISI- Inter Service Intelligence) inawasaidia wanamgambo wa Taliban kwenye masuala ya teknolojia na vifaa vya kijeshi vikiwemo vile vya kutungulia ndege.

3. Matukio 21 ambayo yahusisha jeshi la Uingereza.

4. Matukio yote ya wanamgambo wa Taliban (insurgents) yana baraka zote na mkono kamili wa Osama Bin Laden.

Hii ni baadhi tu ya mambo mazito ambayo yanatishia kuharibu uimara wa taarifa zote zitakazokuwa zikitolewa na ISAF-International Security Assistance Force, ambao ndio wana jukumu la kutoa taarifa za vita kwa vyombo mbalimbali vya habari duniani.

Ni mtandao huuhuu wa Wikileaks ndio ulichapisha na kutoa taarifa kwamba takataka za sumu zinazotupwa Afrika katika nchi ya Nigeria na Ivory Coast zinabadilishwa na fedha zinazolipwa kwa serikali za nchi hizo kutoka kwa makampuni yanayotupa taka hizo na zisionekane.

Wikileaks ni chombo cha kupasha habari zenye undani ambazo lengo lake ni kuweka uwiano kati ya umma kupata taarifa na udhibiti wa taarifa za siri za serikali.

Hapa bwana mkurugenzi bwana Julian Assanga anasema ndipo vyanzo vya taarifa zake kuwa salama,taarifa kuwa zimefunikwa uzuri (Encryption) na mawasiliano yote baina ya watumaji taarifa hizo na wapokeaji vyote ni salama.

Jambo hili ni muhimu sana kwa sasa hivi kwani linaonesha umuhimu wa kuwa na vyombo kama Wikileaks na Jamiiforums na mwonekano wa vyombo hivi baadae vikiwa na taswira ya kutoa taarifa za uchunguzi.

Kama Wikileaks, JamiiForums imekuwa ni kama maktaba yenye kutoa habari za ndani zenye kuelimisha na kupanua uwezo wa kufikiri. Mimi nikiwa mmoja wa wanachama wa siku nyingi lakini mwenye nafasi ndogo sana ya kushiriki hapa natumia nafasi hii kuwapongeza waendeshaji wa mtandao huu na wale wanachama wote wanatumia muda wao kuandika hapa.

Jambo la msingi ni kuendelea kutumia majina ya bandia na pale meza ya JamiiForums siku za mbele tutaona mbinu za juu za cryptograpy na za mbinu za kisheria za kulinda reliable sources zikitumiwa na wana jamiiforums.
 
Dear JF members!.How do you regard wikileak documents on fight against terrorism?.In particular to their recent leaks about Afghanistan such fights.
Does the world need WIKILEAKS ?
 
Yani jana usiku nilikua porini sehemu fulani. Nikahangaika ku post topic kama hiihii ya wiki leaks kwenye hii forum kuanzi saa 8 hadi 9 usiku bila mafanikio. Pia nikamtumia invisible msg kupitia hapa hapa JF aifanye hio topic ya WIKILEAKS sticky. Nimerudi mjini nikasema wacha niangalia labda simu yangu ilizingua tu. Kushuka chini nakuta hii topic na kumbe jamaa aliianzisha since 2008.
BIG UP SANA GT.
Ila namwomba Invisible aifanye topic ya wikileaks sticky. Ni muhimu sana hasa katika hichi kitengo cha intelligensia!!
 
Dah! hii wikileaks na JF ni kama mbingu na ardhi... Ni vitu viwili tofauti sana yaani hazifanani hata chembe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom