Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
- Thread starter
- #1,101
The debate has only begun in earnest!
WAKATI SERIKALI
IKINUNUA
BOMBARDIER,FAST
JET WAAGIZA
EMBRAER 190..!!!
jacob gamaly
about 8 hours ago
0 No comments
Kampuni ya ndege ya Fastjet
imepanga kuingiza nchini ndege
moja jamii ya Embraer 190 ili
kukabiliana na hali ngumu ya sasa
ya kibiashara.
Jana Mkurugenzi Mkuu wa kampuni
hiyo, John Corse amesema ndani ya
wiki mbili zijazo wataingiza ndege
mpya katika safari zake ikiwa ni
sehemu ya majaribio ya kutekeleza
mkakati wa mabadiliko.
“Tunatarajia ndege hiyo itakuwa
jamii ya Embraer 190 na itafanya
kazi kwa mujibu wa kanuni ya
‘waitlist’. Baada ya kufanya
uchambuzi wa kina tulibaini aina hii
ya ndege zinaendana na mazingira
ya kibiashara ya sasa,” amesema
Corse.
Amesema mchakato wa kubadilisha
aina ya ndege utafanyika polepole
na huenda ukachukua zaidi ya miezi
sita ili kuendana na mahitaji ya sera
na sheria za udhibiti wa mawasiliano
ya anga nchini.