Why High Court of Tanzania must issue interm order stopping the migration to DIGITAL TELEVISION

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by R.B, Jan 1, 2013.

 1. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2013
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,575
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 48
  The Consumers Federation of TANZANIA need to open CASE urgency seeking orders to prevent government from effecting the switch-off.
  • The notice for consumers to acquire the set-top boxes was too short given other demands such as Christmas , New year spending and school fees in January.


  • The respondents’ intention to switch off analogue television transmission signal contravenes the doctrine of public participation embraced under Article 10 of the Constitution.
  • The government decision discriminates against Tanzanian's who cannot afford set-top boxes and hence was in breach of the law.
  • “The respondents have failed to address the need to offer subsidy on the set-top boxes to ease the consumer burden,” It many Tanzania 's are unable to afford to buy the set-top boxes whose cost is estimated at between Sh 42,000 and Sh255,000.
  • The switching off analogue signals ahead of the global deadline lacks legal, economic and moral basis, adding that the Digital Television Committee, which is spearheading the move, did not have any consumer representative.
  • The petition a broadcast media incur losses due to the switch-off is effected.
  • “The broadcast media stand to lose business as a result of reduced viewership , decision is implemented,” .
  • The planned switch-off would deny an estimated 2.5 million viewers in Dar es salaam and its environs access to television in the run up to the New constitution.
   
 2. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2013
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 4,211
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 38
  Wabunge wetu wa Dar tena wengine ni wanasheria wako wapi kutetea haki za wanyonge? Wanasubiri tu kujitutumua katika hoja za kisiasa? Hawajui kuwa suala la uchumi ndio kipaumbele ya siasa? Angalia sasa hii haraka ya kuwanenepesha wauza vingamuzi inapelekwa speed 120 kwa Dar kwa kuwa serikali inajua ndipo penye watu wengi wasiojitambua kuliko mkoa mwingine wowote. Angalia sasa zaidi ya theluthi mbili ya watazamaji wa T.V DSM sasa hivi hawatizami na wala hawana mtetezi. Kwani huo mtambo analogy kuzmwa ghafla kuna hasara ya gharama serikali inakwepa? Kivipi inahusika na hizo gharama kama zipo? Some one help this illiterate society P/se.
  .
   
 3. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2013
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,138
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna baadhi ya watanzania wanajifanya hawajui maisha ya mtanzania wa kawaida. Tunaomba tupewe sababu za kuzima mitambo ya Analojia kabla ya 2015 muda ambao ulikubaliwa kimataifa. Ni maslahi binafsi au ni kiherehere kisichokuwa na maana na faida kwa wananchi?
   
 4. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2013
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 484
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Na juu ya yote bado hakuna maelezo ya kutosha kwa mlaji. Kuna wakati walidai ving'amuzi vyote vitaonyesha tv za ndani bure ambapo mtumiaji angelipa zaidi ili kuona channel za ziada, lakini hali siyo hivyo. Wakati TCRA walitumia siku ya jana kusherehesha uhamiaji wa mfumo wa digitali wakiweka kando masuala muhimu kama uhalali wa warusha matangazo kuwatoza watazamaji wake sh. 108,000 kwa mwaka kupata kuona vipindi vya ndani.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 5. L

  Lihove JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2013
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Nadhani hili lina maslahi binafsi,ingekuwa tuko active hata utekelezaji wa mipango mingine ya,kimaendeleo kama kwa hili basi nchi ingekuwa mbali sana
   
 6. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2013
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 7,874
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 48
  Serikali sikivu lacks empathy. We learn they really dont care about us.
   
 7. ha ha ha

  ha ha ha JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2013
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 639
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sisi ni wazee wa kukurupuka, mfumo wa digitali ni maalumu kuhakikisha kuwa;

  • maskini hawatapata tena habari kuhusu siasa na maendeleo ya taifa lao.
  • Kumuweka maskini mbali na upinzani kama CDM na wengine has kuelekea uchaguzi mkuu.
  • Kuhakikisha kuwa maskini hawatajua au watachelewa kujua madudu ya viongozi wao.
  • Kuwanyima maskini ambao ndio wengi fursa ya kuona bunge na mijadala mingine yenye tija kwa taifa.
  • Kwa ufupi the right to be informed imekuwa subject to several unreasonable qualification
  HUU NI MRADI WA MTU.......

  POOR TANZANIA
   
 8. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2013
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe R.B!

  Acha ujuha matangazo ya kuhamia Digital yamekuwa yakitolewa na TCRA kwa muda usiopingika kisheria almost two years . Wacha kuiga kule Kenya ambako wanayo awareness of course level ya elimu iko juu ya elimu yetu ya Kata wadau walikwenda Mahakamani wakishiitaki mamlaka yao ya mawasiliano (CCK) na mahakama ikatoa temporary injunction till mid January 2013 ndipo Kenya wanahama. You don't even follow up what was announced kwamba roll out inakwenda kwa Mikoa kwa sababu za msingi zilizoanishwa.

  Kama una matatizo ya kuelewa utaitakaje Mahakama iinglie na kutoa injunction au zuio la haki kama hakuna mtu aliyelalamika.

  Mimi nilinunua kingamuzi mwezi March kwa shillingi elfu 60. So any serious man you pretend to defend angeweza kududunduliza shillingi elfu 10 kila mwezi tangu Julai 2012 na ilipo fika December angekuwa na kingamuzi cha star times. Watanzania kwa elimu yao ya kupepea always hungojea dakika ya mwisho.

  Tabia hii ni ya kulaaniwa . Just watch over the border Kenya wamezima simu ambazo hazijasajiliwa ambazo ni karibu millioni tano. CCK imesema wanatoa 90 days kwa Watu waliofungiwa simu zao ilipofika Jana tarehe 31/12/12 na hawana mchezo. Watakoshindwa kutumia hiyo grace period simu zitakuwa deleted for ever.

  Hili la vingamuzi kama una tatizo then jikusanye register the number of poor people who can buy a Tv worth over 100,000 and can't afford to go digital then nenda TCRA and build your case.

  Watanzania tuache tabia ya kulalamika bila misingi yenye nguvu. kila mara ukiwa na tatizo just register it and propose a way out vinginevyo just don't pick a pen and write nonsense!
   
 9. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2013
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,575
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 48
  [h=1]Kenya: Court Suspends Nairobi's Digital TV Migration Plan[/h]
   
 10. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2013
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 2,141
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 48
  Jili swala lilijadiliwa bungeni lakini halikupata majibu ya kutosha miongoni mwa waliochangia mada alikuwa mbunge wa cuf Habib Mnyaa aliuliza kwanini kumekuwa na decodar tofauti kwa ajili ya mtu kupata tv ya digital alishauri kama decoder iwe moja badala ya ting,star times na digiter lakini alizungumzia haraka ya nini wakati tuna muda hadi 2015 waziri mhusika hakutoa majibu yaliyotosheleza tatizo bungeni inapotolewa hoja inajadiliwa kishabiki na huyo naibu waziri wenu aliyekuwa anaonekana kama kijana wa mfano ndiyo kaonyesha upeo wake halafu anajitia kuzungumzia maswala ya urais
   
 11. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2013
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,575
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 48
  inflation rate ?????????????????????
   
 12. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #12
  Jan 1, 2013
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,945
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 48
  Ka nchi haka bwana.viongozi wetu ni viherehere kwa mambo ya kipuuzi.ukiwauliza ni lini wamewahi deadline za vitu vya maana,hakuna jibu.

  Deadline za kufuta ujinga,kuondoa umasikini,kutokomeza vifo vya kinamama na watoto.deadline hadi zimeexpire.
   
 13. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #13
  Jan 1, 2013
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,575
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 48
  [h=1]Kenya: Court Suspends Nairobi's Digital TV Migration Plan[/h] By Jillo Kadida and Winfred Kagwe, 21 December 2012

  A television remote control,the government has set December 31 as deadline for digital migration Photo/Joseph Kariuki
  The digital TV migration which was set to kick of in Nairobi from December 31 has been suspended.
  The High Court yesterday issued temporary orders stopping the switch from analogue to digital TV until January 11 when it will make a ruling. Justice Isaac Lenaola granted the order sought by the Consumer Federation of Kenya who are challenging the migration.
  The Information ministry had given notice that it will switch all televisions in Nairobi that are currently broadcast using the analogue system to the digital system by December 31 but Cofek sued arguing that the notice is too short.
   
 14. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #14
  Jan 1, 2013
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 6,934
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 38
  sasa mahakama itatoa order hewa bila kuwa na application?
  ni jukumu lenu saa watu wa dar kuungana kufungua madai yenu
  na kwa vile ni urgent matter mtafungua under certificate of urgency
  suala la 90 days notice kwa vile TCRA ni government agency sidhani kama lia hoja so long wananchi wanaumia
  na mawakili wataeleza kwanini hawatasubiri 90 days notice katika madai yenu.
  hapo mahakama itatoa oder ya kurudisha mitambo ya analogia pending the main application
   
 15. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #15
  Jan 1, 2013
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 4,211
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 38
  .
  Inaelekea wewe ni miongoni mwa wale wafanya biashara wa kariakoo ambao wamefyatua vingamuzi feki china. Watu sasa hivi wana kingamuzi cha tatu kwa miezi minne. Wauzaji ni wale wale wa NO RETURN NO EXCHANGE.
  .
   
 16. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #16
  Jan 1, 2013
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,356
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  .... Inawezekana kabisa umepitia vijidarasa...hujaelimika n your out of touch na maisha ya mtanzania wa kawaida...
  Wakati ambapo umoja wa mataifa umeongeza internet kama haki ya msingi kwa binadamu, sisi kama nchi tunanyima fursa ya habari kwa baadhi ya watu wetu kwa kisingizio cha kwenda digiti! ingekuwa busara kwa mitambo husika digiti na analogia kuendelea kufanyakazi kwa pamoja mpaka 2015...
   
 17. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #17
  Jan 1, 2013
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 7,275
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 48
  huyo ndiyo makamba bwana!rais mtarajiwa!ha ha ha!Dar mkome kwani mmezidi uzembe!
   
 18. b

  blueray JF-Expert Member

  #18
  Jan 1, 2013
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,222
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Surely, I concur with you and this is illegal!

  A court injunction should be sought as a matter of urgency.
   
 19. msafiri27

  msafiri27 Senior Member

  #19
  Jan 1, 2013
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAJITAHIDI KUKUELEWA LAKINI NASHINDWA!!!!!:confused2:
   
 20. steveachi

  steveachi JF-Expert Member

  #20
  Jan 1, 2013
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 2,387
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 48
  Hiyo ni ngumu mkuu,yaani wapingane na wanaowapa mkate wao wa kila siku wakose kula,hao ni mabwana ndioo,yaani kila kitu kipendekezwacho kiwe kizuri au kibaya wao tawilee
   
 21. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #21
  Jan 1, 2013
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,568
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 38
  Mtanzania hata akiongezewa miaka 5 mingine yatasikika malalamiko ya aina hii!
   
 22. P

  Pasco JF Platinum Member

  #22
  Jan 2, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 17,505
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 83
  Mkuu Mokerema, asante kwa kulieleza hili!
  1. Kwanza hilo baraza la walaji tanzania lipo active ? zaidi ya kwenye papwer work?.
  2. limewahi kutoa tuu hata statement yoyote kupinga chochote huko nyuma?.
  3. Jee walipinga hii digital migration kwa TCRA kabla?, au ndio liibukie mahakamani sasa?,
  4. Kwa sababu mitambo imeisha zimwa, anything now will be too little too late!, kanunueni ving'amuzi!.
  Heri ya Mwaka Mpya.
  Pasco.
   
 23. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #23
  Jan 2, 2013
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,789
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 38
  ...Watanzania Bwana! Akishakuwa yeye yuko kwenye Channel ya Ulaji ama ya kuambulia japo makombo basi ghafla macho yake yanakuwa na kiza cha kuona hali halisi ya Watanzania wenzake na kuishia ku..waona ni Majuha! Hivi katika hili kuna haja ya kudhalilishana kweli? Kwani Ukitoa Hoja tu haitaeleweka hadi umuite Mtanzania mwenzako Juha???

  Nchi hii ingebarikiwa Viongozi wenye Busara bila shaka wangejiuliza maswali kadhaa ili kuwasaidia wananchi wao:

  Iwapo imekubalika rasmi duniani kuwa 2015 ndio iwe Mwisho wa kutumika kwa mfumo wa Analogi, Inakuwaje hapa nyumbani uhamaji kutoka analoji kwenye dijitali iwe kama jambo la DHARURA la KUFA na KUPONA??
  Ili Kumfaidisha Nani??

  Kwa Iwapo Viongozi wangetumia busara na kuamua kuwa mifumo yote miwili iende pamoja huku tukiendelea ku-phase out mfumo wa analoji pole pole, kuna tatizo lolote ambalo linaweza kutokea kiufundi??

  Tunapowalaumu wananchi wetu kwa kuchelewa kununua ving'amuzi kwa wakati huku tukijifanya kusahau hali ya Uchumi ya idadi kubwa ya wananchi wetu, mbona Serikali hadi sasa imeshindwa kuwezesha wananchi kuweza kununua king'amuzi kimoja tu na wakapata local channel zote tofauti na vurugu hii ambayo kila mwenye kituo chake cha tiivii anataka awe na king'amuzi chake mwenyewe na hivyo mwananchi kulazimika kuwa na rundo la ving'amuzi ili kuona channel za ndani tu!!!

  With respect brothers Mokerema and Pasco, this shouldnt be just an easy case of 'Juha!' and 'Kanunueni Ving'amuzi!'. Hatuwezi wote Tukawa Sawa.
   
 24. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #24
  Jan 2, 2013
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 6,934
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 38
  Pasco hakuna cha too late hapa
  the court can issue temporary order ya kumaintain status quo
  kuwa mitambo ya analogia irudi hadi hapo service provider watakapotimiza masharti mojawapo ni kuweka for free all local channels na ziwe na good signals sasa kuna watu wana vingamuzi but wanapokaa hawapati kwa uzuri matangazo
  kwenye sheria hakuna cha too late wakili msomi
  ni kazi ya mawakili tu kucheza na vifungu hapo kuiridhisha mahakama.
   
 25. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #25
  Jan 2, 2013
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,575
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 48
  thank's noted
   
 26. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #26
  Jan 3, 2013
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,575
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 48
  Why Consumers Federation of TANZANIA do not open CASE?
   
 27. s

  spiritual-thinker Senior Member

  #27
  Jan 3, 2013
  Joined: Mar 29, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wanapenda kulalama hata wakati mwingine bila kufanya uchunguzi wa kina wa mambo wanayolalamikia. Issue ya ving'amuzi haikwepeki!!

  Teknolojia inaendelea hatuwezi kubaki nyuma, lazima twende nayo.
  Hoja ya gharama haina msingi kwani ving'amuzi vinauzwa sh. Elfu 40 hadi 100,000. Hii ni bei ambayo haiwezi kumshinda mmiliki wa TV ya TZS 200,000+

  Ukizungumzia haki ya kuhabarishwa,Dijitali inatoa haki hiyo kwa hali ya juu zaidi kuliko analojia. Tena hii itaongeza ushindani katika content kitu ambacho hakipo kwenye media ya Tanzania kwa sasa. Sio kila kitu ni ufisadi!!

  Kukwepa kuhamia dijitali ni kufunika moto kwa gunia, tutaumbuka tu in the long run.
   
 28. T

  Tyad of fake Politcs Senior Member

  #28
  Jan 3, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dahhhhhhhh, Biashara za Watu izi jaman, ili nalo litapita.Nakumbuka miaka ya Nyuma zilikuja Road speed Limiters, ziko wap leo ????? cck

   
 29. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #29
  Feb 24, 2013
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,575
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 48
  Haki ya kupata habari na taarifa ni moja ya haki za msingi za binadamu zinazotambuliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria zingine za kimataifa ikiwemo Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu (UDHR) la mwaka 1948.

  Ibara ya 19 ya azimio hilo inasema kuwa kila mtu ana haki ya kuwa huru kutoa maoni yake na kujieleza pamoja na haki ya kutafuta, kupokea, kutoa taarifa na mawazo yake kupitia vyombo vya habari bila kujali mipaka.

  Azimio hilo la Kimataifa limeingizwa kwenye Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 18(2) ambayo inasema “Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote; ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.”
   

Share This Page