Why Foreign Aid is hurting Tanzania and other African countries!

Insurgent

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
469
18
Hivi hawa ndugu zetu zimo kichwani?! Kuumiza watu wengi ili kupata njia ya kutawala?!

Ama kweli, kuongoza chama kama disco ni hatari...sasa hivi wanatumia "muziki" unaopendwa kwenye masikio ya wengi kuleta chuki? Labda kuna wenye mawazo zaidi...lawakilisha kwenu.

CHADEMA YADAIWA KUTAKA TANZANIA INYIMWE MISAADA
Serikali yafuatilia,
Dk. Slaa alipua mabomu
Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha upinzani cha CHADEMA kinadaiwa kuwa kimeanzisha kampeni ya siri na ya chini chini kuyashauri mataifa ya Magharibi kusitisha misaada yake kwa Tanzania. Habari zinadai CHADEMA kupitia Mwenyekiti wake, Bw Freeman Mbowe, kimeanzisha kampeni kuzishawishi nchi zinazotoa misaada kwa wingi Tanzania, kusitisha misaada.

Habari hizo zinadai katika hatua ya kwanza ya kampeni hiyo, Bw Mbowe tayari amezungumza na maofisa wa balozi mbili Dar-es-salaam akiziomba kusitisha misaada hiyo.

Hoja yake ni kuwa misaada inayotolewa Tanzania inatumika vibaya, bila kuwafikia walengwa, Watanzania wa kawaida.

Habari hizo hata hivyo zinathibitisha kuwa hata hizo nchi mbili ambazo Bw. Mbowe amezungumza nazo, zimekataa mpaka sasa kumpa msimamo kamili kama kweli zinaona zinao ulazima wa kusimamisha misaada kwa Tanzania.

Kwa mujibu wa habari hizo kampeni hiyo ya Bw. Mbowe na CHADEMA inalenga kuzuia Tanzania kupata fedha ambazo zingesaidia kuimarisha sekta ya kijamii ya maeneo muhimu sana kwa wananchi ya elimu, maji, kilimo, afya, miundombinu.

Serikali mbili za CCM, katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, zimeelekeza nguvu zao katika maeneo hayo matano muhimu ambayo yanagusa moja kwa moja maisha ya wananchi wote.

Katika bajeti ya mwaka huu, zimeweka kiasi cha asilimia 52 katika maeneo hayo matano tu kwa sababu ya umuhimu wake kwa wananchi, na sehemu kubwa ya fedha hizo itatokana na misaada kutoka nchi za Magharibi.

Mkakati wa CHADEMA ni kwamba kama itafanikiwa kusitisha misaada kwa Tanzania, basi itakuwa haiwezekani tena kwa CCM kutekeleza Ilani yake hiyo na hivyo chama hicho kufanikiwa kujenga chuki kati ya wananchi na serikali yao.

Bajeti ya Serikali kwa mwaka huu wa fedha ambao umeanza miezi miwili iliyopita, inategemea misaada ya wafadhili kwa asilimia 39, ambayo ni kubwa kiasi cha kuathiri mno maisha ya Watanzania kama fedha hizo zinasitishwa na wafadhili.

Habari zinadai mkakati huo wa CHADEMA...baadhi ya wachunguzi wa masuala ya kisiasa waliozungumza na gazeti hili wanaulezea kama tahayari ya kiwango cha chini kabisa.
"Hizi siyo tu mbinu za vyama kuharibiana kisiasa, bali ni kuwatesa moja kwa moja wananchi", alisema mhadhiri mmoja mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam.

Wachunguzi pia wanasema huo ni mkakati ambao hauwezi kufanikiwa kwa sababu nchi za Magharibi haziwezi kukubali kuvuruga uhusiano wake na Tanzania kumfurahisha mtu au kutimiza ajenda na matakwa ya kisiasa ya CHADEMA.

Kama historia inavyoonyesha kusimamisha misada kwa Tanzania ni mkakati ambao unafanikiwa tu kuwaumiza zaidi Watanzania wa kawaida kuliko hao viongozi ambao CHADEMA inadai wanatumia vibaya misaada hiyo.

Uzoefu wa Tanzania wakati wa utawala wa Rais Ali Hassani Mwinyi, unadhibitisha kusimamishwa kwa misaada ni sera itakayowaumiza zaidi wananchi CHADEMA inayodai kuwatetea.

Wakati huo, nchi kadhaa za Magharibi zilisimamisha misaada kwa visingizio mbali mbali, hatua ambayo iliwaumiza sana wananchi wa kawaida wa Tanzania na kuvuruga sera za misaada za nchi za Magharibi.

Usitishaji wa misaada, hata hivyo, ni moja tu ya mikakati mipya ya CHADEMA inayolenga kuharibiana kisiasa baada ya chama hicho kukiri sera na mikakati yake imeshindwa kufanya kazi kwa kupunguza nguvu na kasi ya CCM.

Mkakati mwingine wa CHADEMA ni kujaribu kuwapaka matope watu wote ambao wanaonekana ama kudaiwa kuwa karibu na Rais Jakaya Kikwete, kama njia ya kujaribu kumlazimisha Rais kujitenga na watu hao.

Habari kuhusu mkakati huo zinadai CHADEMA kwa kushirikiana na baadhi ya watu
wakiwamo wafanyabiashara wanaoficha sana msimamo wao wa kisiasa, sasa itawalenga na kuwapaka tope baadhi ya watu hao wanaodaiwa kuwa karibu na Rais Kikwete.

Miongoni mwa watu hao ambao wanalengwa na kampeni za sasa za CHADEMA ni pamoja na Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa; Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM, Bw. Rostam Aziz.

Habari hizo zinadai orodha hiyo ni ndefu zaidi kuliko viongozi viongozi hao watatu, ambao karibuni wamekuwa wakilengwa sana na kampeni za CHADEMA pamoja na washirika wake.

Shabaha ya mkakati huo wa CHADEMA ni kujaribu kumgombanisha Rais na watu ambao kw miaka mingi wamekuwa na msimamo wa kamoja kisiasa.

Viongozi hao watatu walipoulizwa kuhusu mkakati huo wa CHADEMA walikataa kusema lolote na walionyesha kutohangaishwa na jitihada hizo mpya za CHADEMA.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mwandishi wa Habari wa Waziri Mkuu, Bw. Said Nguba alisema wamepata taarifa za hatua hiyo ya CHADEMA na vyombo vya dola vinafuatilia.

Hata hivyo, alisema wao kama watekelezaji wakuu wa sera za chamba tawala, CCM hawasumbuliwi na propaganda hzio bali wataendelea kutekeleza kwa vitendo mambo ya msingi ya kuondoa kero za wananchi kwani uwezo huo Serikali inao.

Alipoulizwa jana kwa simu alikanusha kwenda ofisi za ubalozi kwa ajili ya hiyo akidai kukatiwa misada sio ajenda ya CHADEMA lakini akasema hana uhakika kama watendaji wengine walienda "kwani huenda huko kwa mambo yao"

Naye Said Mwishehe anaripoti kuwa, Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa ametaja majina ya orodha ya kundi la viongozi, maofisa wa umma na mawakala anaodai ni miongoni mwa watu ambao wanaihujumu nchi kutokana na kula fedha za umma na kutoa maamuzi yanayolisababishia taifa madeni.

Katika orodha ya mafisadi aliowataja Dkt. Slaa jana katika mkutano wake na wananchi wa Temeke Mwembe Yanga, Dar-es-salaam wakiwemo wenyeviti na viongozi wa kambi ya upinzani alisema orodha yake ina mafisadi 11 ambapo kabla ya kutaja hadharani alitoa vigezo vya kisheria alivyotumia kuwabainisha mafisadi hao kwa wananchi.

"Katika kundi la orodha ya mafisadi wamo viongozi wa umma ambao kwa kutumia nyadhifa na vyeo vya katika utumishi wa umma wamefanya maamuzi ambayo taifa limepoteza mapato, utajiri na rasilimali zake na kuneemesha raia au taasisi za kigeni.

Kwa mfano wapo viongozi ambao wameshiriki kusaini mikataba mibovu katika sekta za madini pamoja na maeneo mengine", alisema Dkt. Slaa katika mkutano huo aliohutubia yeye, mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa TLP, Bw. Augustine Mrema. Viongozi hao walitua hapo kwa helikopta.

Pia alisema viongozi ambao wamo katika orodha hiyo wamekiuka na kuvunja masharti ya katiba ya Jamhuri ya Muungano na seria ya maadili ya viongozi. Aliwataja baadhi ya mafisadi kwa kutumia ushahidi aliotaka kuutoa Bungeni alipowasilisha hoja binafsi.

Alidai viongozi hao walihusika katika mambo mbalimbali yaliyochangia kuwatia umaskini Watanzania kutokana na fedha za wananchi kutumiwa vibaya na viongozi hao.

"Ushahidi wa viongozi wote hao ambao nimewataja katika orodha ya mafisadi ambao wanaihujumu nchi ninao na nipo tayari kwenda kokote kutoa ushahidi huo kama utahitajika kwani ninao wa kutosha na wala kambi ya upinzani hatuogopi kitu katika vita hiyo ya kupambana na mafisadi wa nchi yetu", alisema Dkt. Slaa.

Bw. Mrema akihutubia wananchi hao alisema umefika wakati kwa Watanzania kuwaunga mkono wapinzani 2010 CCM isirudi madarakani upinzani uongoze nchi. "Wananchi nawaomba mbadilike. Hakuna sababu ya kuendelea kuing'ang'ania CCM wakati inashindwa kutimiza ahadi zake kwa wananchi. Nawaomba wananchi mtupigie kura upinzani ili tuongoze nchi na kuleta maendeleo kw wananchi wote", alisema.

Mwenyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe alisema kambi ya upinzani itaendelea kushughulikia maovu yote yanayofanywa na viongozi na kamwe hawarudi nyuma kwa kuwa mapambano yameanza na yataendelea hadi kieleweke. Alisema yeye yupo kutetea maslahi ya wananchi na ataendelea kuwa mstari wa mbele kukemea maovu na yupo tayari kukamatwa na Polisi kwani yote yale ambayo anawaeleza wananchi ana uhakika nayo.

"Nimepata taarifa Polisi wanachunguza kauli zangu na Bw. Zitto Kabwe ambazo tunazitoa kwa wananchi eti kwa madai kwamba kunachochea kuvunjika kwa amani lakini tunasema Tanzania haina amani na ndio maana wananchi wamechoka na kusikiliza maneno ya Serikali", alisema.

Baadaye alizungumza kwa simu, Bw Mbowe alisema wana ushahidi na tuhuma zote zilizotolewa na Dkt Slaa kuhusu mafisadi wa nchi hii.

Source: Majira, Sunday 16th Sept 2007
 
Hivi hawa ndugu zetu zimo kichwani?! Kuumiza watu wengi ili kupata njia ya kutawala?!
Ama kweli, kuongoza chama kama disco ni hatari...sasa hivi wanatumia "muziki" unaopendwa kwenye masikio ya wengi kuleta chuki? Labda kuna wenye mawazo zaidi...lawakilisha kwenu.

Source: Majira, Sunday 16th Sept 2007



Huu ni usani tu. Hawa jamaa wa MAJIRA wamejiunga katika ligi ya kina HOJA na TAZAMA katika kutengeneza habari. Yaani wako tayari kuhandisi habari hata zinazotoka live kwenye TV kama walivyofanya katika suala la hivi karibuni wakati Zitto alipohojiwa na kituo cha televishen cha Iringa. Wanageuza maneno na kutengeneza yao kwa minajili ya kuudanganya umma ili kukidhi maslahi yao na wafadhili wao kina ROSTAM. Kwa kweli hali inaendelea kuwa mbaya kila kukicha kiasi ya kwamba karibia kila habari inayotoka katika magezeti haya inakuwa ama ya kubadili maneno ama hata kutengeneza kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Ni bahati mbaya sana kuwa wanaojigamba kuwa wana responsibility ya kulinda amani na utulivu wa nchi yetu wameamua kufumba macho na masikio juu ya hili na hata kuwa sehemu ya haya kwa kweli tunaelekea kubaya mno.

Tanzanianjema
 
Hiyo misaada yenyewe haiwafikii walengwa inaishia kwenye matumbo ya wachache na kuishia kufanyia mambo ambayo hayamsaidii raia wa chini.
Labda wakitunyima tutajifunza kutumia rasilimali zetu kugenerate mapato.
Kama Kenya iliweza kudunda bila misaada kwa muda mrefu sioni kwa nini sisi tushindwe.
 
CHADEMA hawana sababu ya kuwashawishi wafadhili wasitishe misaada, hiyo sio sehemu ya ajenda za chama hiki makini. Kinachofanyika ni kuweka ukweli wa mambo hadharani. Viongozi wa CCM wemeji-portray kwa muda mrefu kwamba ni wasafi wakati sio. Wamezoea kubadili uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo! Bahati mbaya kwa taifa na nzuri kwa CCM ni kwamba watu wa kwanza kuaminishwa uongo kuwa ukweli ni wafadhili ambao walifika mahala wakaiona Tanzania kama model katika usafi na katika kupambana na ufisadi. Sasa kwa yale ya majina ya jana, ile list of shame, it is so obvious kwamba wafadhili watakaa chini na kujiuliza hivi hawa jamaa kweli ni wasafi? Sasa hatua gani watachukua wakigundua viongozi wa CCM sio wasafi kama walivyofikiria hiyo ni juu yao sio ya CHADEMA au mtu mwingine.

Kama hatua ya CHADEMA ya kufichua ufisadi na ufedhuli katika nchi itaonekana ni kuwashawishi wafadhili wainyime nchi misaada then, that will just be a bad coincidence but surely it cannot be said to be a thoughful and systematic strategy of our party.
 
Hiyo article nimecheka sina mbavu. Hizo kampeni za hayo magazeti ni za kizamani. I guess they can fool the majority of the population.

Jinsi mambo yanavyokwenda, CHADEMA hata hawana haja ya kufanya hiyo kazi kushitaki eti kwa watoa misaada.

Kinachotia aibu, ni huyo mwandishi (hata haandiki jina lake) na ugonjwa wake wa kuona misaada ya nje ndio uzima wa Tanzania. Wachambuzi wa siasa waliowahoji nao hawana majina, kama kweli wana nia nzuri na Tanzania (wananchi) wasingeona noma kutoa majina yao. Mtu mwenye nia nzuri na nchi lazima achambue habari katika pande mbili. Huyo mwandishi anaonyesha kabisa yuko upande gani (definetely sio upande wa maslahi ya nchi).

Opposition wana momentum nzuri sana sasa hivi, its for them to lose it.
 
Sometimes hii misaada huwa inatulemaza sana kutufanya tuendelee kuwa tegemezi kwa wafadhili na kuifanya serikali isiwe creative kwenye kutafuta vyanzo vingine vya mapato. Kauli ya Meghji wakati wa bajeti kwamba wafadhili wana imani na Tanzania na ndiyo maana wanaendelea kutoa misaada zaidi, ni kauli potofu kwa kiasi kikubwa. Tafiti zilizofanyika kuhusu misaada zinasema kwamba misaada ikiongezeka sana huwa inatend kufuata the law of diminishing marginal returns. Ugonjwa huu uko kwenye serikali yetu ya Tanzania na ndiyo maana utashangaa tunafutiwa na kusamehewa madeni lakini figure ya deni la nje kila mwaka inaongezeka na mchango wa misaada hiyo katika kukuza uchumi wa Tanzania unapungua kwa kadri misaada inavyoongezeka. Misaada (aid) haimaanishi kwamba unapewa bure, bali unapewa hizo fedha kwa riba nafuu (isiyo ya kibiashara) na unatakiwa kulipa baada ya miaka mingi. Lakini mwandishi wa habari the way anavyoshabikia ni kana kwamba misaada hiyo inakuja bure na haitakiwi kurejeshwa!

Ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania haiwezi ku-survive bila ya misaada, lakini swali la msingi ni moja, je misaada hiyo inatumika jinsi inavyotakiwa? Jibu ni HAPANA, na ndiyo maana misaada ya Benki ya Dunia inayoelekezwa kwenye sekta ya elimu na afya imekuwa inaliwa na wajanja wachache na matokeo yake deni linaongezeka na haiwafikii walengwa. HAKIELIMU wamekuwa wakipiga kelele kila siku juu ya matumizi mabaya ya fedha za World Bank kwenye sekta ya elimu, lakini serikali ya Tanzania imekuwa inapambana na HAKIELIMU ili kuficha huo ukweli mpaka wabunge wanapendekeza hiyo NGO ifungiwe, kwamba itakuja kusababisha serikali ya CCM ipigwe mweleka kwenye uchaguzi iwapo matangazo ya HAKIELIMU yataachwa yaendelee kuwafikia wananchi. Je, CHADEMA wakiongelea huo uozo ni dhambi? Ina maana waendelee kukaa kimya huku kizazi kijacho cha watanzania wakiendelea kubebeshwa mzigo wa madeni huku wachache walio serikalini wakiendelea kutafuna hayo mapesa?

Jiulize swala la fedha za External Debt Account ya Tanzania ambayo ni fedha ya wafadhili ilivyotafunwa kwa kugaiwa kama njugu kwa makampuni hewa, je hiyo ni haki? Bado mnataka CHADEMA/wapinzani wakae kimya tu eti kwa kuanika huo uozo tutasababisha tukose misaada? Misaada ina faida gani kama haiwafikii walengwa? Hoja ambayo iko wazi ambayo mwandishi ameamua kuiweka kivyake ili kuwapaka matope CHADEMA ni kwamba CHADEMA iko interested kujua kama misaada hiyo inawafikia walengwa au la, na je kuna faida gani kwa wafadhili kuendelea kutoa misaada ambayo haiwafikii wananchi wa kawaida? MMEM na MMES hela zake zinaenda wapi? Je, zile dollar 10 kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi zinawafikia? Wanazitumia kwa matumizi yapi? Vitabu vipo mashuleni? Hali ya vitabu mashuleni ni kama jinsi Kayumba anavyogombea kitabu na wenzake wakati Emmy ana kitabu chake peke yake, Kayumba hawezi hata kuazima kitabu akafanyie homework zake nyumbani, anaambiwa abaki shule ili asome na wenzake! WB wametoa hela kwa ajili hiyo lakini ziko wapi? Matokeo yake wananchi wanaishia kulazimishwa kujenga madarasa na nyumba za walimu huku hela za MMEM haijulikani zinaishia wapi. Halafu serikali inadai kwamba wamejenga madarasa mengi sana ambayo hayana wadawati wala hakuna vitabu, shule ni majengo tu au pamoja mazingira mazuri + walimu, vitabu, madawati na mengineyo?

It is very unfortunate kuwasingizia CHADEMA kwamba wanataka Tanzania inyimwe misaada, motive yao ni kuhakikisha kwamba serikali inatumia vyema hiyo misaada na siyo ku-misuse na kuendelea kuongeza deni la taifa. Ninashawishika kusema kwamba mwandishi wa hiyo news alikuwa biased, kwenye swala la misaada, he needed to do more homework ili kujua hoja ya akina CHADEMA kuhusu misaada na siyo kuiweka hoja kwenye perspective ya kivyake ili kukidhi matakwa ya wanaomlipa kwa kuandika hiyo news. No wonder hajadiriki kuweka jina lake kwa kuwa anajua anachokifanya (spinning, na si ajabu ni spinning chini ya Spin Dr RA)!
 
Hivi hawa ndugu zetu zimo kichwani?! Kuumiza watu wengi ili kupata njia ya kutawala?!
Ama kweli, kuongoza chama kama disco ni hatari...sasa hivi wanatumia "muziki" unaopendwa kwenye masikio ya wengi kuleta chuki? Labda kuna wenye mawazo zaidi...lawakilisha kwenu.

Huo ni mchezo wa siasa.

Hata hivyo hiyo misaada wanayosema si bure huwa mara nyingi ni 'grants', ni bora wasitupe tunaweza kuamka na kujikwamua katika lindi la ufukara.

Fikiri dhahabu, almasi, tanzanite, magogo, gas etc bado hiyo uranium, mafuta n.k
 
CHADEMA ninayoifahamu haiwezi fanya hivyo, CUF well ni sera number moja!!! Ila kama CHADEMA nayo itaingia huko hapo ndio tutahitaji kupuuza wanasiasa wote nchini,,, maana CHADEMA ndio chama tunachokiona mbadala!

Kuhusu wafadhili sidhani kuna wasilolijua kuhusu hao waheshimiwa,,, in any case makosa ya hao waheshimiwa karibu yote ni kwa manufaa yao... hakuna kitatokea of course,,, ndio maana hata maalim seif hawamsikilizi tena...
 
CHADEMA ninayoifahamu haiwezi fanya hivyo, CUF well ni sera number moja!!! Ila kama CHADEMA nayo itaingia huko hapo ndio tutahitaji kupuuza wanasiasa wote nchini,,, maana CHADEMA ndio chama tunachokiona mbadala!

Kuhusu wafadhili sidhani kuna wasilolijua kuhusu hao waheshimiwa,,, in any case makosa ya hao waheshimiwa karibu yote ni kwa manufaa yao... hakuna kitatokea of course,,, ndio maana hata maalim seif hawamsikilizi tena...

Hapa wewe ndio wa kupuuzwa kabisaaaaaa...

Hivi chuo ulichosoma walikuwa hawana mandatory courses za uchumi (hata kama political economy za wakati wa Nyerere).....

Hakuna nchi inayoendelea kwa misaada ya nje ya muda mrefu... Hii huwa inatakiwa kuwa ya muda mfupi 1 to 5yrs baadaye inakoma. Ila inaonekana sera ya CCM ni kuifanya Tz kutegemea misaada ya nje ya nje for the rest of the what we can see...... hujasikia msemo kuwa hakuna free lunch dunian (By Friedman) na "kwamba mdomo huponza......."
 
CHADEMA ninayoifahamu haiwezi fanya hivyo, CUF well ni sera number moja!!! Ila kama CHADEMA nayo itaingia huko hapo ndio tutahitaji kupuuza wanasiasa wote nchini,,, maana CHADEMA ndio chama tunachokiona mbadala!

Kuhusu wafadhili sidhani kuna wasilolijua kuhusu hao waheshimiwa,,, in any case makosa ya hao waheshimiwa karibu yote ni kwa manufaa yao... hakuna kitatokea of course,,, ndio maana hata maalim seif hawamsikilizi tena...

Just because CHADEMA might have a point, sio kwamba wote tunakiona chama hicho ni mbadala. Don't generalize.
 
Mimi si mfuasi wa chama chochote cha Siasa. Tumepata misaada na mikopo mingi sana Tanzania lakini manufaa yake hatuyaoni. Tunachoona ni wizi ulioshamiri wa viongozi wachache wa kujilimbikizia mali na kuagiza magari ya kifahari mbayo yanaigharimu sana Tanzania. Labda wakati umefika wa kufanya kampeni ili misaada hiyo isimamishwe mpaka hapo kutakapokuwa na uongozi bora utakaokuwa tayari kutumia misaada hiyo kwa manufaa ya Tanzania.
 
Ni ukweli unaofahamika kuwa hii misaada ndiyo chanzo cha rushwa.

Naomba kuuliza swali.

  1. Mapesa ya "Kikwete" yanakopwa na kulipwa + riba katika kipindi cha miezi sita. Hizi pesa zikisha rudishwa benki zinakwenda wapi?

Theory moja ninayo ifahamu kuhusu wizi wa pesa za misaada, pia ina sadikika ndiyo chanzo kikubwa cha utajiri wa Lowassa. Tukipewa misaada, kinatumika kiasi kidogo kwa ajili ya shughuli lengwa. Hayo matumizi yanaambatana na publicity kubwa sana kama tunavyosikia mapesa ya "Kikwete". Baadae tunasikia kimya kingi ambacho mshindo wake ni mgao wa zile pesa kati ya mafisadi.

Kwa mtaji huu, hata tukipewa misaada for the next 100 yrs, mtanzania wa wastani hatoona mabadiliko zaidi ya mahekalu masaki na magari makubwa makubwa...sababu hii misaada haiwafikii walengwa (wananchi).
 
Kwanini wanaoomba tukatiwe misaada wanaonekana ni wasaliti, lakini wale wanaoifuja wanaonekana waungwana? Kwani hiyo misaada imetusaidia kiasi gani? na kama tukikatiwa tutaathirika kiasi gani? Nina wasiwasi sana na nchi yangu na wananchi wake inaonekana wameshapoteza uwezo uwezo wa kujishika wao wenyewe, kiasi kwamba tumeshaanza kufikiri kuwa misaada ni haki yetu na yeyote yule anayeleta kauzibe hatutakii mema!
 
Kwanini wanaoomba tukatiwe misaada wanaonekana ni wasaliti, lakini wale wanaoifuja wanaonekana waungwana? Kwani hiyo misaada imetusaidia kiasi gani? na kama tukikatiwa tutaathirika kiasi gani? Nina wasiwasi sana na nchi yangu na wananchi wake inaonekana wameshapoteza uwezo uwezo wa kujishika wao wenyewe, kiasi kwamba tumeshaanza kufikiri kuwa misaada ni haki yetu na yeyote yule anayeleta kauzibe hatutakii mema!

Hii "generalization" ndio inayotuumiza. Muungwana ndio kwanza ana miaka miwili lakini kelele za kujaribu kumzuia asifikie malengo ni nyingi.
Kwa nini hivi vyama vya upinzani havimpi nafasi ya kutekeleza malengo aliyojiwekea kabla ya kuanza kupiga kelele? Hivi kama mwalimu unaweza kuanza kusahihisha mtihani kabla mwanafunzi hajamaliza?

Hii nayoiona sasa ni kampeni inayofanywa mapema na vyama vya upinzani kwani vinaelewa wazi Muungwana akiweza kuperform hawatapata kura...cha kufanya haribu mipango yake ili achemshe.

Watu wa namna hii sio watu wanaoweka maslahi ya nchi mbele kama wanavyodai, ni watu wanaoweka political ambitions kwanza.

Naamini Muungwana atafanya maajabu given time and chance.
 
Hii "generalization" ndio inayotuumiza. Muungwana ndio kwanza ana miaka miwili lakini kelele za kujaribu kumzuia asifikie malengo ni nyingi.

Miaka miwili ni mingi sana kwa kitu cha maana kufanyika..

Kwa nini hivi vyama vya upinzani havimpi nafasi ya kutekeleza malengo aliyojiwekea kabla ya kuanza kupiga kelele? Hivi kama mwalimu unaweza kuanza kusahihisha mtihani kabla mwanafunzi hajamaliza?

Vyama vya upinzani havina bunge, media kubwa, na mahakama.. je vimemzuia vipi JK kutekeleza malengo yake?..... Wanaomzuia Kikwete kufanya kazi yake ni wezi wenzake kina Lowasa, Rostam Azizi, Karamagi, nk..... usiwalaumu wengine kabisaaaaa

Watu wa namna hii sio watu wanaoweka maslahi ya nchi mbele kama wanavyodai, ni watu wanaoweka political ambitions kwanza.

Naamini Muungwana atafanya maajabu given time and chance.

Maslahi ya nchi ni kuukata utegemezi wa Tanzania kwa misaada ya nje (ECON 347) na wala sio kuuendeleza kwa imani kuwa misaada ambayo inaishia kuliwa na wabadhirifu itafanya kazi given time and chance
 
Ukweli ni kuwa misaada haiisaidii Tanzania, ila ndiyo inayoilemaza Tanzania na kuididimiza kwenye umaskini zaidi. Kama serikali isingekuwa na misaada hii, wangekuwa wakali sana kwenye raslimali zetu.
 
Ukweli ni kuwa misaada haiisaidii Tanzania, ila ndiyo inayoilemaza Tanzania na kuididimiza kwenye umaskini zaidi. Kama serikali isingekuwa na misaada hii, wangekuwa wakali sana kwenye raslimali zetu.

Ni kweli misaada haisaidii LAKINI huwezi kutegemea Muungwana aachane na utegemezi ghafla. Planning ndio muhimu, na vitu hizi vinahitaji kufanyika gradual.

Unfortunately wengi wana simplistic views. Huwezi kutegemea taifa ambalo limekuwa tegemezi kwa miaka 34 liwe independent in just 2 years! Lets be realistic.
 
Ni kweli misaada haisaidii LAKINI huwezi kutegemea Muungwana aachane na utegemezi ghafla. Planning ndio muhimu, na vitu hizi vinahitaji kufanyika gradual.

Unfortunately wengi wana simplistic views. Huwezi kutegemea taifa ambalo limekuwa tegemezi kwa miaka 34 liwe independent in just 2 years! Lets be realistic.

Naona kama wewe unafikiri kwa kuangalia pafupi sana ndugu yangu, unachukulia kuwa misaada ni right ya nchi yetu. Hata kama views zangu ni simplistic, they are more realistic: lazima tubebe msalaba wetu. Misaada itumike kama nyongeza ya juhudi zetu. Hatuwezi kutegemea misaada kama sehemu ya mapato yetu na kuipangia bajeti hata kabla haijafika; mwaka jana serikali imelalamika kuwa misaada iliyokuwa wanaitegemea kwenye bajeti haikufika. Kumbuka kuwa misaada hii haiji at no cost, na watoa misaada wanaweza kuikata ghafla bin vuu, utasemaje. Swala la kukatiwa misaada siyo geni sana.
  1. Mwaka jana bajeti ya serikali yetu ilipata pigo kwa vile "wahisani" waliokuwa wameahidi kutoa misaada hawakufanya hivyo. Kumbuka kuwa "wahisani" hao hupata fedha hizo kutokana na kodi zinazolipwa na raia wao pamoja na makampuni yanayofanya biashara nchini mwao. Kwa nini sisi tusijikusanyie kodi kama wao. Misaada inayokuja ni ziada ya mapato yao; kama hawakupata ziada hiyo hawataleta midsaada hiyo.
  2. Miaka ya hivi karibuni, Kenya ilikatiwa misaada yote lakini kama tunavyoelewa, uchumi wa Kenya na serikali yao leo ni imara kuliko wetu.
  3. Mwaka 1965, mwaka mmja tu baada ya muungano, tulikatiwa misaada mingi sana kufuatia muungano wetu wa Tanzania na msimamo wa nchi hii kuhusu UDI ya Smith huko Rhodesia. Jambo hilo ndilo lilimsukuma sana Nyerere kufuata siasa ya ujamaa na kujitegemea kwa nguvu. Ilikuwa kuwa baada ya muungano ule, walimtaka Nyerere afanye mambo kadhaa kuhusu Zanzibar, ambayo hayakuwa in the interest za nchi ila kwa ajili ya interest zao wenyewe; Nyerere hakukubaliana nao. Vile vile walitaka Nyerere akubaliane na UDI huko Rhodesia, jambo ambalo pia hakukubaliana nalo. Kutokana na msimamo huo wa Nyerere wakasimamisha misaada yao yote. Ndiyo maana ile Nkurumah Hall pale UDSM haikukamilika, na kuna baadhi ya barabara zilivunjwa pale Dar kwa vile zilikuwa zimejengwa na wajerumani. Hospitali ya Ocean Road nayo ilipata msukosuko wa namna hiyo.


Kwa hiyo mwenzangu sijui una maana gani unapotaka tuendelee kuwa wategemezi kama vile wao ni baba zetu. Ndiyo maana wakishasema jambo kuwa raia wao waruhusiwe kuchima dhahabu ama sivyo watakatisha misaada, tunatetemeka. Kwa maoni yangi, ni wazi kabisa kuwa overnight independence over foreign aid inawezekana.

Je umesoma ile post ya TOSCO kuhusu foreign investment? Anatishia kuwa nchi yake ya Uimgereza itasitisha misaada kwa Tanzania kutokana na kesi ya Middleton na Ben Mengi, come on!
 
Back
Top Bottom