Who wounded you???

dah, me hata sitaki kukumbuka aisee. kuna vitu viwili huwa vinaniuma sana.
1. mzazi mwenzangu aliyemtelekeza mwanangu, si kwamba hana pesa (anafanyaka kaz kwenye concern world wide) namshukuru Mungu maisha yanasonga. mwanangu anasoma int.schools, naishi maisha ya kawaida ya kuweza kubadilisha mboga.
2. ndugu zetu kututelekeza hasa baada ya baba kufariki. jamani Acheni Mungu aitwe Mungu. saiv wanafarakana hakuna mfano. . . na hawaamini nimefikaje hapa nilipo tena kazi nzuri bt ni kwa juhud binafsi!
 
jamani
APPOSTLE PDIDY KAFANYAJE TENA??
BE CAREFULL DONT TOUCH MA ANNOINTING
 
This is on of the best thread i have seen in JF.
BOFLO naomba uwe una nitag mkuu
 
mwaJ ni kweli ulichosema ...
Nimeitumia hiyo avatar zaidi ya miaka 3, Nampenda sana Zidane, siku walipokosa world cup na Italy nililia saaaaana
Plz ikubali tu hii....
View attachment 70397

Duh! Boflo umeniweza sanaaaaaaa leo! Khaaaa! Sina hamu! Basi bana itabidi tu nivumilie yote. Mie nina tatizo moja kubwa nikishaizoea avatar ya mtu basi ninamfananisha nayo kwa njia moja ama nyingine basi ikitokea akabadilisha huwa napata shida sana naona kama naongea na mtu mwingine/tofauti na yule nilozoea kujibishana nae. Muulize hata Preta atakuambia!
 
Last edited by a moderator:
aiseee... tamu sana hii...

ila mbona hamsemi kwa mlio waumiza..
 
18. Not me but my uncle suffer this situation to death, aisee ni mbaya sana ukiangalia yeye aliwalea watoto wake kwa mapenz yote wakati anawahitaji sasa wao with no reasons they all left him alone, all by himself kama hakuzaa vile ndugu wa pembeni ndo wamlishe na kumhudumia its so painfull aisee usiombee ikukute..............

Tukiacha kuwachukulia watoto wetu kama mitaji ninaamini itapunguza maumivu sana. Hii mambo ya kusema, aisee inabidi nitafute hata tutoto tuwili, maana nikizeeka watakuja kunisaidia hii ndio matokeo yake, wakiishia zao roho inauuuuuuma hadi inaweza kuchomoka. Zaa for fun of having kids and if they want to go let them go. Lakini pia na watoto sio ndio wachukulie kama ni loophole mimi, ninaamini mtoto ana wajibu mkubwa sana kwa mzazi wake especially pale wanapofikia umri wa utu uzima
 
Uchungu ni kitu kinachoua mahusiano mengi iwe ni kifamilia, kihuduma na hata kindoa. Uchungu unaondoa ukaribu baina ya watu na kujenga ukuta wa uhasama. Kamwe uchungu usiachwe ukakua katika maisha yetu.

Uchungu unakuja na hasira, ghadhabu na kelele na matukano. Utakapoacha uchungu ukue ndani yako utaleta na yote hayo. Kwa wale wanaoamini katika Bibilia "Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya - Efeso 4:31.

Uchungu unakuja pale mtu anapokukosea na wewe ukaweka kinyongo ndani ya moyo wako. Uchungu unakuwa shina ndani yako kwa kukuonyesha kuwa uko sahihi kuwa na kinyongo kwa kosa ulilotendewa. Unapingana na dhamira yako inayokuambia sio sawa kuwa na kinyongo na mtu. Unajikuta unawaza jinsi mtu huyo alivyokukosea na kutokuona kosa ambalo unalifanya la kuweka kinyongo na kutokusamehe.

Again kwa wale wanaoamini katika Bibilia, "Mkiangalia sana mtu asiipunguke neema ya Mungu, shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo" - Ebrania 12:15. Katika mistari hii tunaona kuwa shina la uchungu linachupuka pale ambapo mtu anakuwa ameipungukia neema ya Mungu.

Mtu unapoacha kusamehe hapo ndipo unapoanzisha mizizi ya uchungu na kutokusamehe kutapelekea wewe kupungukiwa na neema ya Mungu. Unaposhindwa kusamehe wengine unakuwa unamwambia Mungu kuwa asikusamehe na ndipo unapopungukiwa na neema ya Mungu.

Unapokuwa na uchungu na mtu, sio nyie wawili tu mnao athirika bali na watu wote wanaowazunguka. Ndio maana kwa wale wanaoamini katika biblia inasema kuwa muangalie sana maana uchungu utasababisha watu wengi kutiwa unajisi sababu yenu. Shina la uchungu linachipuka kwenye mizizi ya kutosamehe, lazima ujifunze kusamehe hata kama mtu amekukosea kwa kukusudia.
 
Kweli kabisa.. u know kuna wakati unatamani uyafute machungu but it is too hard...

kuna watu walibadili jina langu akaenda kusoma mtu mwingine shule ya ya boarding enzi hizo nafasi chache. Afisa elimu akanipigania nikapata shule ya kutwa, nilisoma kwa hasira mpaka leo nawachukia wote waliofanya kazi hiyo japo sijui wako wapi?
 
Back
Top Bottom