Who really killed Prof. Mwaikusa?

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
302
Friday, 16 July 2010 08:31

Fidelis Butahe na Aziza Masoud wa Mwananchi

MTOTO wa Profesa jwan Mwaikusa ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa nje ya nyumba yake, amesema hahusishi mauaji hayo na ujambazi kwa kuwa waliotoa maisha ya baba yake hawakupora chochote.

Magazeti yetu mengine sijui hayana wahariri wakuu?
Shirika la Wabenedition Tanzania ambalo ni tawi toka shirika la Mt. Otilia kutoka Ujerumani kuingizwa kwenye tetesi ya kashfa ya mauaji ya Mwanasheria Mwaikusa, ni jambo la kushtua na si la kawaida, pengine ni mbinu ya kuyumbisha ukweli wa kilichojilia, huku wakihusishwa Br. Aidan OSB na Br. Edmond OSB kwa kile kinachoelezwa sahihi za hao wanashirika la Benediction Fathers Peramiho kukutwa kwenye document ya Mwaka 2003 inayoonyesha wanahisa katika machimbo yamgodi wa Lukarasi.

Jambo linalonishangaza ni kuhusushwa Abate Lambert Dor OSB ambaye ni mkuu wa shirika hilo huko Peramiho, wakati wahusika ni hawa wawili pengine walifanya mikataba binafsi na si shirika.

Ninavyoelewa kuna upungufu mkubwa kuhusu habari hiyo kwa maana kwamba wenye mamlaka katika shirika lao kufanya mikataba si kila mwanashirika, ila ni Procurator wa shirika mwenye dhamana na mambo ya uchumi wa shirika, na udadisi wangu bado sina hakika kama hawa ni wako katika kitengo cha procurator ya Peramiho Abbey, huenda ni miradi binafsi inayofanywa na hao mabradha wawili na hivyo kulitia aibu na miskusuko shirika. Pengine uchunguzi ufanyike kwa kiwango cha kisheria, maana kama habari ilivyoletwa inatoa mswali ambayo kuna upungufu mkubwa wa kulihusisha shirika hilo ambalo makazi yake yako St. Otillien, nchini Ujerumani.

Habari hiyo ni kama ifuatavyo hapo chini nukuru kutoka gazeti la Raia Mwema.


=============

Profesa Mwaikusa alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Sheria. Aliuawa na watu wasiojulikana usiku wa Julai 13, mwaka 2010 wakati akirejea nyumbani.

Mengi yamezungumzwa kuhusu mauaji ya gwiji huyo wa sheria nchini, kila kundi likiibuka na nadharia yake kuhusu wahusika wa mauaji hayo, baadhi wakiyahusisha na kesi za watuhumiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda aliokuwa akiwatetea katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda Jijini Arusha.

Wapo pia waliohusisha mauaji hayo na kifo cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Daudi Balali, hao ni walioamini kuwa Gavana huyo alipata kukutana na Profesa Mwaikusa na inawezekana kuwa walizungumza kuhusu kashfa za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).


Hayo yakiendelea, sasa taarifa za kichunguzi ambazo Raia Mwema imefanikiwa kuzipata, zimeongeza utata zaidi katika sababu za mauaji hayo, zikieleza kwamba mauaji ya Profesa Mwaikusa yanaweza kuwa yalifanywa kwa maelekezo ya baadhi ya watawa wa Shirika la Wabenedikti wa Peramiho, wafanyabiashara, wahalifu na viongozi ndani ya Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma.

Habari zaidi zinasema wahusika kwa mujibu wa taarifa hizo mpya, wamekuwa wakijichimbia Peramiho, Songea, mkoani Ruvuma na Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mauaji ya Profesa Mwaikusa yalipangwa na kuratibiwa ndani ya Shirika la Watawa la Peramiho mkoani Ruvuma ambako inaelezwa ndimo walimo wahusika wakuu wa mauaji hayo kutokana na ugomvi wa umiliki wa mgodi wa dhahabu wa Lukarasi ulioko wilayani Mbinga, uliokuwa unamilikiwa na Shirika la Benedikti la Peramiho.

Taarifa zinasema kwamba Profesa Mwaikusa alikuwa akihifadhi nyaraka za umiliki wa mgodi huo na yalikuwapo maagizo kutoka kwa mkubwa wa Shirika, anayetajwa kwa jina la Fr. Lambert, akiwaagiza wakurugenzi walioteuliwa kusimamia hisa za shirika hilo kwenye mgodi huo kutofanya jambo lolote pasipo kumshirikisha Profesa Mwaikusa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Profesa Mwaikusa naye alikuwa ameteuliwa kuwa mmoja wa wawakilishi wa shirika hilo kwenye mgodi huo wa dhahabu, kwa barua ya Agosti 12, 2003 iliyowekwa sahihi na Buruda Aidan na Buruda Edmund wote wakionyeshwa kuwa na hisa 2000.

Wawakilishi hao wawili waliteuliwa na Mkubwa wa Jumuiya hiyo ya watawa wa Peramiho wakiwa watawa na kuongezewa mtu mwingine, mkazi mmoja wa Songea Mjini anayetajwa kwa jina la Steven Haule ambaye hakuwa mtawa.

Uteuzi wa wawakilishi hao uliibua uhasama mkubwa miongoni mwa watawa wenzao likiibuka kundi la watawa waliotaka wakabidhiwe jukumu la kuwakilisha shirika hilo huko mgodini. Inaelezwa kuwa ni kundi hili lililopanga njama za kupora nyaraka hizo kwa gharama yoyote hata ikiwa ni kutoa uhai wa wawakilishi halali wa shirika hilo.

Taarifa zinasema akiwa mwakilishi wa Shirika la watawa hao, Profesa Mwaikusa alisimamia sheria akiwataka watawa hao kufuata sheria katika kuuchukua mgodi huo wa Lukarasi, msimamo ambao hawakukubaliana nao kutokana na mazingira ya usiri katika umiliki wa mgodi wenyewe, usiri uliowanufaisha zaidi watawa hao.

Vielelezo mbalimbali, ambavyo Raia Mwema imefanikiwa kuvipata, vinawaonyesha baadhi ya viongozi wa zamani wa shirika hilo kuwa nyuma ya kundi hilo la watawa na washirika wao waliopanga mipango ya kupora nyaraka hizo za siri kutoka kwa Profesa Mwaikusa, na wanatajwa kuanzisha uhasama mkubwa na viongozi wapya walioteuliwa na aliyekuwa Mkubwa wa Shirika hilo la Peramiho, Fr. Lambert.

Siri katika umiliki wa Mgodi wa Lukarasi

Nyaraka zinaonyesha kuwa shirika hilo linamiliki mali mbalimbali zikiwamo nyumba, magari, bunduki, viwanja na mgodi wa dhahabu wa Lukarasi huko Mbinga mkoani Ruvuma.

Hata hivyo, nyaraka hizo zinaonyesha kuwa shirika hilo limekuwa likimiliki mgodi huo kwa siri ambapo hutumia wawakilishi wanaojitokeza kwenye nyaraka za shirika hilo.

Shirika hilo la watawa wa Peramiho, lilinunua hisa kwenye Kampuni ya UMICO, inayomiliki mgodi huo wa dhahabu wa Lukarasi, kwa dola zinazoelezwa kuwa zaidi ya laki tatu, na vyanzo ndani ya Shirika hilo la "Roman Catholic Benedict's Abbey of Peramiho" vinabaisha kuwa lilitoa shilingi bilioni mbili na kusimamia uendeshaji wa mgodi huo kwa siri.

Kwa mujibu wa nyaraka za kampuni hiyo kwa mwaka 1997, wanahisa wa Kampuni ya UMICO, wanaonyeshwa kuwa ni Barnabas Mathew, Dismas Ndunguru, Johnson Nchimbi, Francis Kayombo, Kenneth Nchimbi na Karim Hassanali Teja Kanji.

Hisa za shirika hilo kwenye ndani ya UMICO hazikuandikwa kwa jina la Peramiho. Hata hivyo, kumbukumbu za kununua hisa zinalifichua shirika hilo pale zinapoonyesha kuwa Peramiho ni mwanahisa ambazo ameaminishwa Johnson Nchimbi, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya UMICO Ltd azishikilie kwa niaba ya shirika.

Miongoni mwa nyaraka hizo, ni zile za ununuzi wa hisa kutoka kwa mwanahisa Karim Kanji, mawasiliano ya shirika na Kanji kuhusu malipo ya hisa hizo na nyaraka za kisheria kuhusu uteuzi wa wawakilishi wa shirika hilo katika Kampuni ya UMICO, na kila mmoja alisaini nyaraka zake pamoja na mwanasheria wao, Profesa Mwaikusa, Juni 17, 2003.

Nyaraka hizo za uteuzi zilikuwa ni za pamoja na Buruda Mhuwa, Buruda Kimario na Haule, ambapo ni katika nyaraka hizo pia zinatajwa hisa 4,250 za shirika hilo kwenye mgodi wa Lukarasi, mgawanyo ukiwa wawakilishi watawa wawili hisa 2000 kila mmoja na Haule hisa 250.

Katika nyaraka hizo pia ndimo inamobainishwa ushiriki wa Nchimbi katika kulifichia siri shirika hilo hizo hisa 4250.

Utaratibu uliotumiwa na shirika hilo kumiliki mgodi huo wa dhahabu wa Lukarasi, ndio unaowapa nguvu watawa hao pamoja na washirika wao kuwaelekeza wachunguzi wa kadhia hii kwenda Brela wakifahamu fika kuwa kule shirika halipo, lakini wakati huo huo wakisahau kuwa kuna nyaraka nyingine zinazowahusisha moja kwa moja na umiliki wa mgodi huo.

"Sifahamu chochote, hatuhusiki na mgodi wa Lukarasi, I know nothing about it, nenda Brela upate members wa mgodi, sawa? bye," alijibu Buruda Fidelis Mligo alipotakiwa kuelezea anachofahamu kuhusu mgodi huo.

Jibu la aina hiyo hiyo lilitolewa na Johnson Nchimbi katika mahojiano yake na Raia Mwema kwa simu akisema: "Mimi siko authorized (siruhusiwi) kutoa taarifa za kampuni. Ni vema ukaenda Brela." Hata hivyo, baadaye alizungumza kuonyesha yamekuwepo mawasiliano na Buruda Mligo akisema: " Jana Br (Buruda) Fidelis alipigiwa simu kutoka Raia Mwema, hakufurahishwa na maswali, nikamwambia wakikupigia tena waambie waende Brela."

Nchimbi alisema tena baaaye: "Si vema mtu kukupa taarifa, mimi si msemaji wa kampuni, ukitaka taarifa zaidi tuwasiliane."Vyanzo vya ndani ya shirika hilo vinaashiria kwamba mauaji ya Profesa Mwaikusa yana mkono wa baadhi ya watawa ndan i ya shirika hilo.

Aidha, taarifa nyingine zinamtaja mtu ambaye alikuwa karibu kabisa na Profesa Mwaikusa kusaidia kufanikisha mpango huo kama Profesa Mwaikusa asingekubali kutoa nyaraka za shirika.

Vyanzo ndani ya familia ya marehemu pamoja na taarifa za maandishi zinaibua mazingira ya mashaka kuhusu mahusiano ya mtu huyo na marehemu, siku chache kuelekea mauaji hayo. Familia ya marehemu Mwaikusa inathibitisha kupotea kwa mtu huyo tangu ilipohamia Salasala kutoka Kunduchi jambo lililowashangaza kwani haikuwa kawaida yake.

Maelezo hayo yanaoana na ya vyanzo ndani ya shirika hilo vinavyoeleza kuwa marehemu akiwa na mkurugenzi mmoja wa watawa waliokuwa wakisimamia mgodi huo, walikubaliana na mtu huyo wakutane nyumbani kuzungumzia ujumbe uliokuwapo kuhusu kundi la watawa waliotaka kuchukua mgodi kwa nguvu, lakini katika hali iliyowashangaza, rafiki huyo wa marehemu hakufika na hawakuonana naye tena hadi Profesa Mwaikusa anauawa.

Taarifa zinasema wakati wa msiba mtu huyo alifika nyumbani kwa marehemu eneo la Salasala, ikiwa ndiyo mara yake ya kwanza tangu familia hiyo ihamie huko.Mawasiliano ya watawa hao na Profesa Mwaikusa kabla ya mauaji yake, vinaonyesha kuwa mbali ya yeye, kulikuwa na watu wengine watatu zaidi waliokuwa kwenye orodha ya kuuawa, na kwamba tayari walishahisi kuwapo kwa njama hizo.

Profesa Mwaikusa alikuwa mhimili mkuu wa Kampuni ya UMICO na mmoja wa wawakilishi wa Shirika ndani ya UMICO. Baada ya mauaji yake, wakurugenzi waliobaki nao walijikuta katika wakati mgumu, wakilazimishwa kuachia nafasi zao.

Source: Raia Mwema
 
VANgi

Mkuu wakati tunaendelea kuyatafuta majibu ya maswali yote hapo juu, sisi kama Wakristo inatupasa kuachilia damu ya Yesu Kristo ili Mungu aweze kufuta laana kwaajili ya damu iliyomwagika mahali pale, kwa lengo la kutoa laana juu ya nchi dhidi ya damu hiyo.

Hii ni laana na isipofutwa kwa kuachilia damu ya Kristo, Mauaji yataendelea na kuendelea kama ilivyo sasa.
 
Last edited by a moderator:
Wakati mwingine tuchunguze pia maisha ya prof huko nyuma, pengine alitengeneza maadui kutokana na kazi yake, inaweza kuwa ni serikali au watu binafsi all is possible. watu wengi wameuawa kwa style hii, wengine kutokana na dhuluma, wengine kutokana na kujua siri za mambo fulani hivyo kutishia usalama wa kundi fulani n.k

Pengine watu wanaomjua Prof vizuri wanaweza japo kutudokeza..
 
Friday, 16 July 2010 08:31

Fidelis Butahe na Aziza Masoud wa Mwananchi

MTOTO wa Profesa jwan Mwaikusa ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa nje ya nyumba yake, amesema hahusishi mauaji hayo na ujambazi kwa kuwa waliotoa maisha ya baba yake hawakupora chochote.

Magazeti yetu mengine sijui hayana wahariri wakuu?

It don't matter nothing. Dude's dead as a doornail, and whoever did it will never be caught.
 
Tuangalie tafsiri halisi ya neno JAMBAZI. Ukishaipata hiyo ndio utaweza kujadili kikamilifu mada hii.
 
Katika taarifa ya ITV saa mbili usiku huu, jeshi la polisi limeeleza kuwashikilia watuhumiwa sita kwa mauaji ya Prof. Mwaikusa
 
Breaking News?

It might have been a News Alert probably - but not Breaking News!
 
Aisee, kama ni kweli afadhali mkondo wa sheria uchukue nafasi yake na haki itendete.
 
Inanikumbushia mambo ya kina Dumisani Dube,cha msingi ni usikute watu wamepewa kesi ama maigizo bongowood style.
 
Jamaa yangu mmoja ana handle hii issue, walichokosea hawa jamaa walisepa na simu ya mtoto wa Prof, hawajui kwamba ku tract simu ni rahisi mno, halafu wakawa wanaitumia kuwasiliana, so mmoja alikamatwa Dodoma, wengine Mbagala. Prof alikuwa aenda kumfunga mtu Burundi huko kwenye kesi za mauaji ya Kimbari, alikuwa na Doc muhimu sana za hiyo kesi, so jamaa walikuwa wanazitaka hizo doc wakidhani jamaa anatembea nazo kwenye gari kumbe kaziacha ofisini bana. Imenisikitisha sana hii issue Mungu amlaze mahali pema peponi Prof.
 
Jamaa yangu mmoja ana handle hii issue, walichokosea hawa jamaa walisepa na simu ya mtoto wa Prof, hawajui kwamba ku tract simu ni rahisi mno, halafu wakawa wanaitumia kuwasiliana, so mmoja alikamatwa Dodoma, wengine Mbagala. Prof alikuwa aenda kumfunga mtu Burundi huko kwenye kesi za mauaji ya Kimbari, alikuwa na Doc muhimu sana za hiyo kesi, so jamaa walikuwa wanazitaka hizo doc wakidhani jamaa anatembea nazo kwenye gari kumbe kaziacha ofisini bana. Imenisikitisha sana hii issue Mungu amlaze mahali pema peponi Prof.
Asante kwa hii habari. Chimunguru ni kesi ya mauaji ya Burundi au Kwa Kagame wa RPF?
 
Usalama wa taifa una fanya kazi gani?! Inakuwaje watu wageni au kwa faida ya wageni waingue nchini kutenda mauaji bila ya wao kujua!?
 
Aisee, kama ni kweli afadhali mkondo wa sheria uchukue nafasi yake na haki itendete.

Wasiswasi niliokuwa nao tangu mwanzo ni jeshi la polisi kuwa na majibu kati ya haya matatu yaliyotengenezwa
a. majambazi ndio walio husika na mauaji b. wauaji hawajulikani c. mauaji yanahusiana na maisha binafsi ya marehemu, hata kama serikali ya Tanzania inahusika au Rwanda

Suburini, utasikia taarifa ya ajabu ya uchunguzi wa polisi
 
Kwa kweli kama hawa wauaji watakuwa ni wauaji toka Rwanda, Selikali inatakiwa kuchukua uamzi wa kueleweka kabisa, na ikiwezekana, watupiliwe mbali kabisa hata kwenye east africa community, fukuza kabisa hata balozi wao.

Kwa sababu kama mauaji yatakuwa ndo ya aina hiyo ya ICTR tribunal issue, basi selikali ya Kagame lazima itakuwa inahusika....kwa visirani vyao na Wahutu.
 
Back
Top Bottom