Where is Separation of POwer BTN BUNGE na SERIKALI - Bunge letu sio huru, Ma speaker wote ni MAMLUKI

George Maige Nhigula Jr.

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
470
149
Ndugu wana Jamii wenzangu,
Imekuwa kawaida sasa kwa kiti cha Speaker kufanya hila na mbinu zote chafu kuilinda serikali kwa Hali na Mali na kiti cha speaker kuwanyima wabunge haki Yao ya kikatiba ya kusimamia na kuishauri serikali hivyo basi tumekuwa tukishuhudia Bunge likifanya kazi Kama ni sehemu ya serikali na si independent body.

Wana Jamii sote tunafahamu kuwa Executive, Legislature and Judiciary are very independent body and acts according to their principle and rules, lakini Bunge letu limekuwa likisubili kupata maelekezo ya serikali hivyo serikali kuingilia muhimili mwingine.

Hivyo basi ma speaker wetu wameendelea kulipotosha Bunge na kuvunja katiba ya nchi kwa kulifanya Bunge lifanye kazi zake Kama dalali wa serikali na kuacha majukumu yake ya kikatiba ya kusimamia na kuishauri serikali .


Tuna ushahidi wa kutosha wa ma-speaker wetu kuzima hoja nyingi nzito zenye maslahi kwa taifa kwa lengo kubwa la kuilinda serikali . Swala hili halikubaliki na nadhamilia kuwafungulia kesi ya kikatiba ma-speaker wote kwa kuvunja katiba ya nchi na kutotutendea haki sisi wananchi wa Jamhuri kwa kuzima mijadala muhimu na kuilinda serikali na kuwanyima wabunge wetu haki Yao ya kikatiba ya kuihoji na kuisimamia serikali .

Naomba ushauri na msaada wa kisheria ili kufanikisha kufungua kesi mahakama Kuu kuwashitaki maspika wetu.
Nashukuru sana.
 
Jambo hili lina hitaji mjadala wa kitaifa na mimi ningependekeza kama inawezekana hata kifugu cha katiba kibadilishwe kwa sasa ili speaker,naibu speaker na wenyeviti wa bunge wasiwe wabunge.Hatuna haja ya kusubiri tume ya katiba kwa hili kwani kwa hali ilivyo 2015 ni mbali na si busara kusubiri.
Vyombo vya habari vinapaswa kulifanya jambo hili ajenda ya kitaifa na sio kuripoti tu kama jambo la kuja na kupita.
 
Ndugu yangu Nhigula nakuunga mkono kweli na Kama kutakuwa na gharama yoyote ya kufungua kesi hiyo ya kikatiba Mimi nipo radhi kuchangia gharama hiyo na wana Jamii forums wengi nahakika watakuunga mkono wa gharama za kesi au ushauri wa kisheria

Naugua sana kuona Bunge letu sisi wananchi linashindwa kuongelea maswala yanayotugusa kwa udhaifu na umamluki wa ma-speaker hawa ambao hawana nia njema kwetu sisi wananchi
 
Back
Top Bottom