Wezi wa BoT - EPA warejesha bilioni 50 hadi leo

WanaJF muda huu Waziri wa Mipango na Fedha Mustapha Mkullo, sijui naye ni alhaj au vipi, anatangaza kuwa bilioni 50/- kati ya bilioni 133/- zilizoibwa na wajanja-wajanja wetu, zimerejeshwa Benki Kuu ya Tanzania.
Mkullo anasema kuwa fedha za mwisho kufikisha kiasi hicho ziliingia leo asubuhi sana kutoka akaunti moja ya mwizi ambaye hata hivyo, kama kawaida, kwamba hana haja ya kumtaja kwa sasa.
Anasema hivi sasa kuwa fedha hizo zinazorejeshwa hazina riba. Kila mwizi anarejesha kama alivyochukua, bila kujali kama alizitumia kufanya biashara au vinginevyo.
Wakati akisema hivyo, wananchi nao, kama ilivyo kwa JF, wanataka kurejesha tu isiwe nongwa, wakamatwe na washitakiwe.

Kama wanaosema kuwa pesa zinarudishwa ndio wale wale waliosema kuwa hakuna wizi au upotevu wowote umefanyika in the first place basi inabidi uchukue muda kidogo kuamini maneno yao.
 
Hapa bado tunachezewa tu. Swali ni kwanini hawatajwi? Au ndio hawatajiki? inaonekana hiyo ni trick, au naye Mkullo ni waziri wa fedha jina, kuna mwenyewe anayeoperate under the carpet.

Ndio maana yake mkuu!
 
Jamani waacheni kwanza wazirudishe tuone ngapi zinaweza kuwa recovered hivi hivi kwa pressure za JK baada ya hapo ndio mengine. Good move so far, well done JK.
 
Kama wanaosema kuwa pesa zinarudishwa ndio wale wale waliosema kuwa hakuna wizi au upotevu wowote umefanyika in the first place basi inabidi uchukue muda kidogo kuamini maneno yao.

Hebu tukumbushe ndio kina nani hao, majina ya waliosema hayo? you mean Mkullo? na lini alisema? any proof? au ndio nanihii tena?
 
Ebu tujikumbushe kidogo hotuba aliyoitoa Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Bungeni tarehe 30 Desemba, 2005 kuhusu Rushwa (ufisadi):

"Tutaongeza kasi ya kupambana na rushwa kisayansi kwa kushambulia kiini chake, na kuziba mianya yake. Tutajitahidi kuongeza mishahara na kuboresha maslahi ya watumishi wa umma ili kupunguza vishawishi vya rushwa. Tutaendelea pia kuongeza uwazi katika maamuzi ya Serikali hasa katika manunuzi na mikataba. Tutaimarisha uwezo wa kifedha na kiutendaji wa taasisi zilizo mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya rushwa, hususan Taasisi ya Kuzuia Rushwa, Jeshi la Polisi na Mahakama. Lakini yote hayo ni bure iwapo wananchi hawatajitokeza kusaidia vyombo hivyo. Naomba ushirikiano huo kutoka kwa wananchi.

Katika harakati za kupambana na rushwa yapo mambo mawili mengine ambayo tutayaangalia kwa karibu. La kwanza ni mikataba. Tutaangalia upya taratibu za mikataba mbalimbali inayoingiwa na Serikali, mashirika ya umma na idara zinazojitegemea kwa nia ya kuongeza uwazi na uwajibikaji. Mikataba ni mwanya mkubwa wa rushwa hasa zile kubwa kubwa za wanaotafuta utajiri.

Kadhalika, hatuna budi kuchukua hatua thabiti za kuzuia watumishi wa umma kutumia nafasi zao kujitajirisha na kujilimbikizia mali. Sisemi kwamba ni haramu mtu kuwa tajiri au kuwa na mali. Ninachosema mimi kuwa ni haramu ni kutumia nafasi yako ya utumishi au uongozi wa umma kujipatia manufaa ya kujitajirisha au kujilimbikizia mali.

Jambo hili ndilo linalokera sana watu kuona mtu ambaye hana chochote lakini miezi michache tu baada ya kupata cheo anakuwa tajiri mkubwa. Ona majumba ya fahari, ona madaladala, teksi bubu, anaishi maisha ya kifahari na kadhalika. Wananchi wanayo haki kuhoji, na wanayo haki kupata majibu. Ndugu zangu, naomba tuwe waadilifu. Tusilaumiane. Nataka Tume ya Maadili ya Viongozi isione haya kutuuliza jinsi tulivyozipata mali tunazosema tunazo. Nitawasaidia kujenga uwezo wa kufanya hivyo kama tatizo lenu ni hilo".

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete...ulisema mwenyewe....sasa tunataka majibu sahihi ni akina nani hao wanaorejesha hizo pesa na kwanini hadi sasa hawapo Keko au Segerea...ulituambia mwenyewe kwamba tunayo haki ya kuhoji...sasa twambie tuwajue wezi wetu ni akina nani?

Hii hotuba JK alisoma kama ilivyoandikwa,kwa hiyo yeye kama jk hakuandika hayo aliyoyasoma.ndio maana hata utekelezaji wake unakuwa wa shida sana, kama angejua kuwa itatuwa hivyo basi nafikiri angeruka baadhi ya maneno.
 
Naomba kuuliza wakongwe wa JF, hivi hizi fedha za EPA zilichukuliwa awamu ipi na zilikuwa zirudi lini? naomba mnisaidie kwa hilo.
 
Hebu tukumbushe ndio kina nani hao, majina ya waliosema hayo? you mean Mkullo? na lini alisema? any proof? au ndio nanihii tena?

Ndugu yetu una tatizo gani??
Inatuhuzunisha kuwa kila kitu humu unahitaji proof ina maana kwako JF ndiyo source za findings zako au ina maana unakitu unatafuta humu so unafanya monitoring. Siyo bure unajiumbua kwa kujifedhulisha mwenyewe.
Kumbuka kuwa sources zote zipo clear and hakuna atakayekuambia kuwa usome magazeti na ripoti mbalimbali. pia unaonesha hufuatilii bunge wala mijadala ya kitaifa, kama ufahamu wako wa current issues upo nyuma omba tuisheni hapa JF utafundwa. acha maswali ya kitoto dareslam.
 
Hii hotuba JK alisoma kama ilivyoandikwa,kwa hiyo yeye kama jk hakuandika hayo aliyoyasoma.ndio maana hata utekelezaji wake unakuwa wa shida sana, kama angejua kuwa itatuwa hivyo basi nafikiri angeruka baadhi ya maneno.

Bila shaka!
Ndio sababu ilibidi akane hata ile aya ya "Mahakama ya Kadhi" kwenye ilani yao na kusema hakuiandika yeye!
 
Wakuu,

Hebu turudi kwenye ile taarifa ya vyombo vya habari kuhusiana na EPA kama ilivyo hapo chini

Baada ya kuipitia Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na ya Mkaguzi wa Nje, yaani, Kampuni ya Ernst and Young, Mhe. Rais amesikitishwa na kukasirishwa na taarifa ya kuwepo vitendo vya ukiukwaji wa makusudi wa sheria, kanuni na taratibu za uuzaji wa madeni ya nje vilivyofanywa katika taasisi muhimu na nyeti kama vile Benki Kuu. Kwa hiyo, ameamua kuwa hatua za kisheria na kiutawala zichukuliwe dhidi ya makampuni na watu waliohusika na vitendo hivyo viovu.
"
Kwa ajili hiyo Rais ameamua yafuatayo:-

1. Ametengua uteuzi wa Dkt. Daudi A. Balali kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

2. Ameagiza Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ikutane mara moja kujadili taarifa ya ukaguzi na kuchukua hatua zipasazo za kinidhamu dhidi ya Maofisa wote wa benki, walio chini ya mamlaka yake waliohusika na kusababisha hasara hii kwa taifa.



3. Shughuli za ulipaji wa madeni katika Akaunti ya EPA zisimamishwe mara moja mpaka hapo taratibu za uhakiki na utaratibu mpya utakapotengenezwa.

4. Rais amewaagiza; Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Inspekta Jenerali wa Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kuchunguza na kuchukua hatua zipasazo za kisheria kwa makampuni na watu waliohusika na uhalifu huu. Rais amewataka watumie ipasavyo mamlaka na madaraka waliyo nayo kwa mujibu wa sheria. Aidha, amewataka wakamilishe kazi hiyo katika kipindi cha miezi sita. Amemuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali awe kiongozi wa kazi hii. Amewataka wahakikishe kuwa fedha zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa.

5. Rais pia amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kushirikiana na kuwasaidia watendaji wakuu hao wa vyombo vya dola katika kufanikisha jukumu lao hilo.
“Watu wengine wenye taarifa za ziada pia wazitoe kwa Timu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na wenzake”."

Sasa tukinangalia hii si ni maelekezo ya raisi yanayotekelezwa hapo.Mimi naona ni hatua nzuri tu kwa sasa.

Ila inajenga precedence gani kama wakirudisha hawatashtakiwa?

Ina maana kama 100% ya hizi fedha zikirudi, rais atatengua uamuzi wake wa kumfuta kazi Ballali?Maana Ballali naye anaweza sema hakupewa nafasi ya kujitetea(rule of natural justice)

Je hivi Kasusura naye akirudisha zile USD. 2 Million za citi bank naye aachiwe huru?

Mimi mtizamo wangu ni kuwa hawa mabwana wana kesi za jinai za kujibu maana wametumia "kumbukumbu,nyaraka na hati zilizo batili na za kugushi". Na kwenye kesi za jinai si zinaendeshwa in accordance to the penal code na anayeshtaki si ni Jamhuri. Sasa mambo ya kupatana kulipa hizo pesa kunatokea wapi?Kwanza wanalipa kwenda kwenye account gani? na ya nani? Hapa hamna issue ya out of court settlement maana hizi si kesi za madai na kwenye criminal offences, kitu cha karibu na settlement ni plea bargain/deal ambapo mtuhumiwa anakubali kosa(ana pleadge Guilty), then ndo Prosecution wana present grounds for a lesser punishment. Sasa hawa waliorudisha wame plead guilty wapi?

Hii ni kesi yetu(Jamhuri si ndo sisi wananchi, Polisi na Mwanasheria Mkuu wanatu present sisi wananchi(the people). We can demand prosecution kwenye hili. Na mimi pia nasupport petition.
 
mbangaizaji ahsante sana kwa kubandika hiyo post, watu wengine humu JF huwa wanabwabwaja tu. kwa wale wanaobwabwaja kama hampati jibu katika hiyo post ya mbangaizaji ndio muanze kuleta hoja, la sivyo fanyeni subra kazi inafanyika, muda wa tume ukiisha na kama hakuna action yeyote kutoka kwa waliokabidhiwa hiyo kazi na JK akikaa kimya tu, hapo ndio tuandamane, tuchukuwe sheria mkononi, tufanye kila tuwezalo kuhakikisha mambo yanakwisha kwa faida yetu walipa kodi, au mnasemaje?

Kwa sasa na kama nilivyoisoma hiyo post ya mbangaizaji na hii post ilioanzisha thead hii, naona waliopewa kazi wanaifanya.
 
zimerudi wapi?
soma post iliyoanzisha thread hii halafu muulize huyo, hizo billioni 50 zimerudi wapi? ukiniuliza mimi unanionea kwani nimechangia mada tu na nimeona hapo mwanzoni kuwa billioni 50 zimerudi. Au umekurupuka tu, hukusoma mwanzo wa thread? kwa kukusaidia tu nabandika hapa kipande cha hiyo post:

...bilioni 50/- kati ya bilioni 133/- zilizoibwa na wajanja-wajanja wetu, zimerejeshwa Benki Kuu ya Tanzania...
 
soma post iliyoanzisha thread hii halafu muulize huyo, hizo billioni 50 zimerudi wapi? ukiniuliza mimi unanionea kwani nimechangia mada tu na nimeona hapo mwanzoni kuwa billioni 50 zimerudi. Au umekurupuka tu, hukusoma mwanzo wa thread? kwa kukusaidia tu nabandika hapa kipande cha hiyo post:

...bilioni 50/- kati ya bilioni 133/- zilizoibwa na wajanja-wajanja wetu, zimerejeshwa Benki Kuu ya Tanzania...

Hakuna uthibitisho wowote ulioonyesha kuwa hizi pesa zimerudi. Hakuna independent body yoyote iliyoonyesha kuwa hizi pesa zimerudi. Na kwa vile hakuna majina yanayotolewa, mpaka sasa haya ni maneno ya Kikwete na wasanii wenzake tu kama vile walivyoanza kwa kukataa kuwa hakuna wizi umetokea!
 
Ndugu zangu,

Hili kosa si la Kikwete wala si la serikali yake wala si la Chama chake cha CCM. Hili ni kosa letu na upumbavu wetu wa kukiweka chama hiki cha CCM (TANU/ASP) madarakani kwa miaka yote hii (1961-2008). Tunakubali kiini macho cha kubadilishiwa sura ya mtu kila baada ya miaka 10.

Asilaumiwe mtu wala kitu hapa. Ni sisi wenyewe na ujinga na uwoga wetu. Tunavuna tulichopanda.

Mapinduzi na mageuzi ya nchi yetu yataletwa na sisi wananchi wenyewe. Si CCM si CUF si CHADEMA si TPL si UDP si NCCR-Mageuzi ni Wananchi wenyewe, hizo ni platforms tu tunazoweza kuzitumia kujiletea Mapinduzi na Mageuzi.

Kama tumekasirika kikweli kweli, tu-organize na ku-moblize tufanye kweli 2010.
 
Ndugu zangu,

Hili kosa si la Kikwete wala si la serikali yake wala si la Chama chake cha CCM. Hili ni kosa letu na upumbavu wetu wa kukiweka chama hiki cha CCM (TANU/ASP) madarakani kwa miaka yote hii (1961-2008). Tunakubali kiini macho cha kubadilishiwa sura ya mtu kila baada ya miaka 10.

Asilaumiwe mtu wala kitu hapa. Ni sisi wenyewe na ujinga na uwoga wetu. Tunavuna tulichopanda.

Mapinduzi na mageuzi ya nchi yetu yataletwa na sisi wananchi wenyewe. Si CCM si CUF si CHADEMA si TPL si UDP si NCCR-Mageuzi ni Wananchi wenyewe, hizo ni platforms tu tunazoweza kuzitumia kujiletea Mapinduzi na Mageuzi.

Kama tumekasirika kikweli kweli, tu-organize na ku-moblize tufanye kweli 2010.

Hapa mkuu nakubaliana na wewe ila huu mfano ni kama wale ambao wanawalaumu watoto wadogo (au wazazi wao)wanaobakwa na mizee mifisadi kuwa ni kwa nini walikwenda kuteka maji kisimani peke yao bila wazazi wao badala ya kudeal na wabakaji kwanza.

Hapa tunadeal na wezi na mafisadi wanaoendelea na wizi wao this moment na sio masuala ya historia ya Tanu na Asp!
 
Ndugu zangu,

Hili kosa si la Kikwete wala si la serikali yake wala si la Chama chake cha CCM. Hili ni kosa letu na upumbavu wetu wa kukiweka chama hiki cha CCM (TANU/ASP) madarakani kwa miaka yote hii (1961-2008). Tunakubali kiini macho cha kubadilishiwa sura ya mtu kila baada ya miaka 10.

Asilaumiwe mtu wala kitu hapa. Ni sisi wenyewe na ujinga na uwoga wetu. Tunavuna tulichopanda.

Mapinduzi na mageuzi ya nchi yetu yataletwa na sisi wananchi wenyewe. Si CCM si CUF si CHADEMA si TPL si UDP si NCCR-Mageuzi ni Wananchi wenyewe, hizo ni platforms tu tunazoweza kuzitumia kujiletea Mapinduzi na Mageuzi.Kama tumekasirika kikweli kweli, tu-organize na ku-moblize tufanye kweli 2010.

Amen to that..tutaongea mpaka tuwe machizi..personally uzalendo umenishinda..sasa naona niangalie tuu..Serikali na Mafisadi sisi wenyewe ndo tumewaweka hapo na tuliwachekelea wakati wanapiga kampeni na maneno matamu matamu (ndugu na jamaa zetu mikoani etc etc)...Sometimes i wonder kama the education levels in bongo are kept low so that the government keeps hold of power..coz we all knw 80% of tanzanians will think we are crazy for the views we have on the govt.. :-(
 
Imemshinda wakati unaona anavyijituma mpaka fedha zilizolambwa zinarudi, unanishangaza sana.

Ndugu, bongo

Hakuna mtu angependa kuwa na mashaka na JK kwa sasa, lkn kama yeye ni kiongozi anatamka nini kwa haya yanayo endelea? Kama unavyo onyesha upendo na kumshiba JK basi na kama uko jirani naye mwambie arekebishe haya mambo! Watendaji wake wanamharibia sana kama hawa kina Hosea, Chenge, Mustafa etc
 
Back
Top Bottom