mzado
JF-Expert Member
- Jan 12, 2014
- 1,013
- 1,483
Kwema wadau,
Sio kwa lengo la kupima kukubalika au ubora wa JF bali kama passive member wa muda mrefu kidogo nimeona niulize, labda kuna namna naweza itumia kwa manufaa zaidi.
Binafsi JF kwangu ni sehemu ya kupumzikia nikitaka kukimbia uhalisia, nikiingia huwa najihisi nipo ulimwengu wa uhuru wakutoa maoni na kushiriki mijadala ni mdau mkubwa wa Habari na Hoja mchanganyiko na MMU. Kwa majira ya mchana huwa ni jukwaa la habari na hoja mchanganyiko na jioni ni MMU na hii huwa inatokea automaticaly, marachache sana huwa nahudhuria majukwaa mengine.
Jinsi naichukulia sasa ni kama vile kijiwe/maskani flani hivi yenye wadau wa kila aina, wataalam, wasomi, wajanja wajanja, na wajuaji lakini wazee wa fix na wakurupukaji hawa ndio wengi. Ni maskani ambayo ukikuta wanastori za kujenga, basi unatulia unamskiliza mtoa mada kwa makini lakini kwa tahadhari, na wadau wakianzia kuchangia tu basi kwa zaidi ya asilimia 90 kunauwezekano wakutoka nje ya mada na kuweka data za uongo kwa sifa l, labda iwe mada juu ya mapenzi na kunyanduana angalau wanaweza stick kwenye point kwa asilimia kubwa,
JF kama kijiwe chochote kina characters wake wakubwa, ambao ukikaa kwa muda kuna baadhi unaweza watambua na kujua tabiazao na kuna wafuasi wao, pia kuna wale ma-star wa msimu wanakuja wana-hit na kupotea.
JF ni sehemu bora ya kujifunza ukikutana na nyuzi makini, ambazo kwa binafsi yangu zimekua za kumulika kwa tochi. Nisehemu ya burudani na kupotezea mawazo hususani kwenye comments na kubwa zaidi si sehemu sahihi ya kuomba ushauri hususani ukiwa kwenye kipindi kigumu, asilimia kubwa ya wadau wanao comment hawajafahamu nguvu ya kile wanacho andika.
Binafsi nakipenda hiki kijiwe, lakini kama wasemavyo wadau ukiwa na akili za kushikiwa JF inaweza ikakupoteza kabisa.
Karibuni kwa maoni.