Website za Serikali hazina taarifa za sasa huku tunakimbilia kwenye Tehama

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Napata sana shida kwa Taasisi,Idara na mamlaka nyingi za Serikali unapofungua website zao ili upate taarifa ambayo inaweza kukusaidia katika shughuli zako za kazi na kukuta aidha hata website hawana au kama wanayo basi hakuna taarifa za sasa zote ni za miaka 2 hadi 4 nyuma kiasi cha kushindwa kupata taarifa unazozihitaji kwa shughuli zako mahususi.

Ni Taasisi chache sana ambazo wamejitahidi kuweka taarifa zao kwa wakati na kila wakati kiasi ambacho unachokihitaji lazima utakipata na usipokipata basi ni rahisi kupata kwasababu mawasiliano yao yako live au mubashara....mfano TRA,BOT,POLISI na BAADHI YA WIZARA nk kwa uchache wanajitahidi.

Lakini wengine ni shida sana mfano hizi municipal zetu ndiyo shida kabisa hakuna kitu wameweka humo ofisi za ma DC na RC unapita vitu vichache.

Nakumbuka utawala wa Rais Dr Kikwete alijitahidi sana kuhakikisha serikali inakuwa na taarifa za kutosha katika website ili kurahisisha mawasiliano na pia kusaidia wanainchi kufahamu kinachoendelea na hata ikiwezekana kupata baadhi ya documents ambazo uki download tu unapata documents au form fulani kuliko kuanza kuitafuata katika ofisi husika hizo hard copy.

Kiukweli kama tunataka mambo ya TEHAMA na hayo mambo ya basi kuna haja ya wahusika kuangalia upaya namna ya kuboresha taarifa zao ktk website ili ziwe na manufaa kwa wanainchi wao.
 
Hawa watu wanahisi bado tupo miaka ya 80's
..maana utakuta hata server za website za jkt au necta zinazidiwa na blog ya millardayo
 
mpaka mwaka 2016 website ya jeshi la wananchi ilikuwa inasema amiri jeshi mkuu ni jk
 
Back
Top Bottom