Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,707
- 40,766
Na. M. M. Mwanakijiji
Mojawapo ya vitu ambavyo huwa vinafanywa 'vizuri' na watawala wa watawaliwa unapoelekea mwaka wa uchaguzi ni jinsi gani huwa wanajipanga kujipendezesha kwa wakubwa wa dunia. Unajua pale nchi inapojisema tu kuwa ni ya "kidemokrasia" basi wakubwa wanaanza kuangalia vitu vinavyofanyika hasa linapokuja suala la uchaguzi. Uchaguzi unachukuliwa kama kipimo hasa cha ni jinsi gani nchi imekomaa kidemokrasia.
Inapotokea tu kuwa kuna figisufigisu fulani basi wakubwa wa dunia - US, UK, EU, UN na taasisi mbalimbali huwa na haraka ya kutuamulia kama uchaguzi ulikuwa huru na waki (free and fair). Lakini wao hawaanzii siku ya uchaguzi tu bali wanaangalia hata miezi michache nyuma. Na taasisi za ndani na za nje zote zinaanza kutoa "mafunzo" (training) kwa waangalizi wa ndani na wa nje. Waangalizi wa ndani ni wale wa taasisi za kiserikali na za nje ya serikali ambazo huwa zinafuatilia uchaguzi kuanzia maandalizi hadi utangwazaji wa matokeo ya uchaguzi na hata uapishaji wa uongozi mpya.
Zinapokuwepo taasisi za kidini na zisizo za kidini za ndani. Lakini linapokuja lile la waangalizi wa nje wao wanaweza kushirikiana na taasisi hizi za ndani au wakawa na watu wao wenyewe mara nyingi hawa huanza kuingia nchini kama miezi mitatu kabla ya siku ya uchaguzi mkuu. Wakiongozwa na utaratibu uliowekwa na tume ya uchaguzi basi taasisi hizi hupewa uhuru wa kutembelea sehemu mbalimbali kuona maandalizi ya uchaguzi yanavyokwenda na wanalindwa na sheria na taratibu mbalimbali. Taasisi hizi huwekewa masharti ambayo wanatakiwa wayafuate.
Lakini kubwa linalotuhusu leo - ni jinsi gani - wakubwa wa dunia wanaweza kuizawadia nchi kwa kuandaa uchaguzi mzuri. Hivyo watawala wa watawaliwa hujitahidi saini kupambisha maandalizi ya uchaguzi ili jicho la wakubwa lianze kuangalia kwa mapenzi. Hili linatuleta kwenye mada ya leo.
Tunavyoelekea uchaguzi mkuu mwakani tutaanza kusikia na kuona jinsi watendaji wa serikali wa ngazi mbalimbali wakianza kuonesha na kuahidi jinsi gani uchaguzi wa mwakani utakuwa na tofauti kubwa na ule wa 2020. Unaweza kuamini kabisa - ukiwasikiliza sana - kuwa hiki chama kinachoenda kuandaa uchaguzi ujao sicho kilichoandaa uchaguzi uliopita na kuwa sasa wamepata akili ya kuendesha uchaguzi mzuri, usio kuwa na rabsha wala washawasha.
Kwa vile wakubwa wataanza kuvutiwa basi muda si mrefu tutaanza kusikia wakubwa wakitoa misaada ya kuandaa uchaguzi mkuu. Kuna fedha nyingi - mabilioni- ya maandalizi ambavyo yataelekezwa kwa vyama vya siasa na wanufaika wakubwa wakiwa ni chama cha watawala wa watawaliwa. Ikumbukwe kuwa katika fedha hizo kuna ulaji mkubwa unaofanyika kuanzia kwenye maandalizi ya makabrasha ya mafunzo, mafunzo yenyewe, uchaguzi wa nani atakuwa mwangalizi (ndugu, jamaa, na marafiki) na taasisi zao za NGO zikijiandiksha tume ya uchaguzi kuwa watakuwa ni sehemu ya waangalizi wa ndani au wa kimataifa.
Itaendelea...