Waziri wa zamani asema January Makamba ameisababishia nchi hasara ya Shilingi trilioni 1.268

PROSEKYUTA

Member
Aug 23, 2011
34
40
Kwenye mchango wake kwenye hotuba ya bajeti ya Waziri wa Nishati, January Makamba, ya 2023/24 iliyopitishwa na Bunge jana, Waziri wa zamani, Luhaga Mpina, amehoji madudu yafuatayo yaliyofanyika kwenye wizara ya Nishati chini ya Makamba:

MKATABA WENYE UTATA WA TEHAMA WA SHILINGI BILIONI 70 BAINA YA TANESCO NA KAMPUNI YA TECH MAHINDRA YA NCHINI INDIA

Hotuba ya Waziri haijaeleza utekelezaji wa ujenzi wa Mfumo wa TEHAMA ambao unatekelezwa na Kampuni ya Tech Mahindra ya India. TANESCO na Tech Mahindra ziliingia mkataba wa Tsh. Bilioni 70 mwaka wa fedha 2021/2022 kujenga mfumo wa TEHAMA. Hatujaelezwa mradi huu umefikia wapi na umeisaidiaje Tanesco kuboresha mifumo yake ya TEHAMA?

Je,.TANESCO ilipata kibali cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kama
hakuna uwezo wa ndani ya nchi wa kujenga mfumo huo? Aliuliza Mpina.

Fedha nyingi zimetengwa na kutumika katika mradi huu halafu Bunge halipewi taarifa yoyote, aliongeza.

USIMAMIZI MBOVU WA MKATABA WA BWAWA LA JULIUS NYERERE (JNHPP)

(i) Makato ya CSR bilioni 270 hadi sasa Wizara haijazidai kutoka kwa mkandarasi kama mkataba unavyotaka. Waziri katika hotuba yake ameeleza kwa kuanzia Serikali itajenga chuo kikubwa cha kisasa cha ufundi wa umeme na mafuta na gesi mkoani Lindi. Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024 bila kutaja gharama za mradi huo na bila kuweka bangokitita la miradi yote ya kijamii itakayonufaika na CSR
ya Mradi wa JNHPP.

Hii inathibitisha kuwa wizara haina dhamira ya dhati ya kudai fedha hizo kutoka kwa Mkandarasi na kama ilivyoelezwa na CAG kwenye ripoti yake ya mwaka 2021/2022.

(ii) Kushindwa kudai tozo ya fidia ya ucheleweshaji (5%) ya bei ya mkataba kiasi cha Tsh. Bilioni 327.93 kwa mwaka na kwa miaka miwili ni sawa na Tsh. Bilioni 655.

Hotuba ya Waziri haijaeleza hatua zozote zinazochukuliwa na Serikali kudai fedha hizo licha pia ya CAG kulalamikia eneo hili.

Kitendo cha Waziri wa Nishati, kushindwa kueleza hatua zilizochukuliwa kukusanya fedha hizi kwa mujibu wa mkataba kunathibitisha kwamba hakuna nia njema na kuleta sintofahamu kubwa kwa wananchi.

Leo hii Waziri wa Nishati awaeleze watanzania fedha zao ziko wapi?

Pia Wizara na TANESCO wameshindwa kuidai Kampuni ya IPTL madai halali baada ya Serikali kushinda kesi mahakamani tangu Machi 2021 bila sababu za msingi Tsh. Bilioni 342.

Waziri aueleze umma wa watanzania fedha zao Bilioni 342 ziko wapi?

Wizara ya Nishati na TANESCO wameshindwa kukusanya madai haya ya kisheria zaidi ya Tsh bilioni 926 katika Bwawa la Mwalimu Nyerere na IPTL Tsh Bilioni 342 jumla ya madai yote ni Tsh Trilioni 1.268.
 
Wataumbuka tu kama wanavyoumbuka treni ya mwendo kasi walisema mwezi wa pili wakasema mwrzi tano wakaema mwdzi sita sasa wamesema mwezi saba hiyo 2023 ahadi ya 2022 hapo sijataja hapo
 
Back
Top Bottom