Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema katika uchaguzi ujao ukiwemo wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu Jeshi la Polisi litalinda Demokrasia ili kuhakikisha unakuwa uchaguzi wa Huru na Haki huku Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Camillus Wambura akisema wako tayari kuhakikisha uchaguzi unapita salama.
Demokrasia haihitaji polisi kabisa, ni watu wapige kura kwa uhuru, na zihesabiwe kwa uwazi na Uhuru, matokeo ya kweli na halali yatangazwe. Ulinzi wa nini? Ulinzi ndio wizi!
Katiba ya nchi iliyopo pamoja na Sheria za nchi zilizopo zina-promote uimla (dictatorship).
Kazi Kuu kabisa ya Jeshi la Polisi ni Kusimamia Sheria pamoja na kulinda Katiba ya nchi.
Je, Jeshi la Polisi linatarajia kulinda demokrasia gani wakati Katiba na Sheria zilizopo hazitambui uwepo wa hicho kitu kinachoitwa demokrasia?? Je, ni demokrasia gani basi ambayo Jeshi la Polisi linaahidi kwamba watailinda??
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.