DOKEZO Waziri wa Maji imulike MORUWASA, wananchi wananyanyasika

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Jan 2, 2023
231
558
Manispaa ya Morogoro (Morogoro mjini) ni mji wa zamani kidogo hivyo hata baadhi ya miundombinu iliyowekwa zamani imeshachoka ikiwemo miundombinu ya maji hasa hasa hizi meter (dira za kusoma matumizi ya maji)

Meter nyingi ni chakavu kiasi kwamba kuona unit za matumizi ni vigumu sana jambo linalopelekea hisia ya ukadiriaji wa unit kuwa kubwa

Pili mbali na ukadiriaji wa matumizi ni kwamba kawaidi uchakavu au uzèe wa kitu hupunguza ufanisi wa meter hizo

Pamoja na uchakavu na uzee wa meter hizo ikitokea ikaharibika wao moja kwa moja wanadai fidia ambayo ni Tsh.100,000/= kwa dhana kwamba watumiaji ndio walioharibu

Pamoja na uonevu huo kituko ni kwamba hata baada ya kulipa fidia haufungiwi meter mpya badala yake wanakuletea iliyokwishatumika ambayo imeng'olewa kwa mtu mwingine kwasababu mbalimbali

Sasa hapa unajiuliza, hizi faini ambazo almost ni sawa na gharama ya meter mpya zinaenda wapi? Na kwanini tulipe fidia kwa kitu kilichoharibika sababu ya kutumika kwa muda mrefu? Meter nyingi zilifungwa miaka ya mwishoni mwa 1990's

Je, gharama tunazolipa kila mwezi moja ya kazi yake si pamoja na kufanya matengenezo ikiwemo kuondoa miundombinu iliyochoka? Kwao hili hawana

Haya yote wanafanya kwasababu wanajua hakuna mbadala wa shirika lingine la maji

Nadhani mamlaka za maji wangepewa watu binafsi ufanisi ungeongezeka. Serikali wabaki kuwa moderators kwasababu wafanyakazi wengi wa mamlaka hizi ambazo ni monopoly hawajali wateja na kwa MORUWASA imekithiri

Bill za maji ziko juu kwasababu meter nyingi ni mbovu hivyo wasoma meter wanakadiria tu

Kitengo cha huduma kwa wateja kipo kwa ajili ya ku print bill tu badala ya kusaidia wateja wao wenye shida mbalimbali na wanafanya hivyo kwasababu wanajua kinachofanyika
 
Hawa Morowasa ni wangese sana. Ila matasisi ya Imma ni vituko, tuwape DP world yote tu.
 
Moro hakuna maji hizo bill zinatoka Wapi
Kama Hujui MORUWASA Nao Wababaifu Wao Maji Wakati Mwingine Hayatoki Wanakadiria. Wafanyakazi Hasa Wasoma Meter Wajeuri
Anakaa Home Kwake Anatuma Unit
 
Back
Top Bottom