Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,893
- 16,317
Ndugu zangu katika JamiiForums, bila shaka wote mu wazima wa afya,
Kwa kuzingatia ukweli kuwa sekta binafsi hapa Tanzania ndio imeajiri wafanyakazi wengi kuliko hata taasisi za serikali, hivyo kwa namna yoyote ile utendaji kazi wao una athiri (negatively or positively) kwa kiasi kubwa sana uchumi na ustawi wa taifa letu tukufu.
Baada ya Waziri wa Kazi kuamuru kufanyika kwa zoezi la ukaguzi wa vyeti kwa watumisi wote wa mashirika ya umma, atakuwa na mpango gani kwa watumishi wa sekta/makampuni binafsi walioajiriwa kwa ujanja ujanja na baadhi kwa kutoa rushwa za ngono ama kutumia vyeti visivyo halali?
Ninafahamu fika ya kuwa Waziri wa Kazi (serikali) has limited scope juu ya namna ya uendeshwaji wa mashirika na kampuni binafsi, lakini wafanyakazi wenye uwezo mdogo waliopo na kujaa huko katika kampuni binafsi wanaumiza uchumi wa nchi yetu kupitia utoaji wa huduma mbovu na zisizokidhi viwango.
Watanzania kamwe hawataweza kushindana na watu kutoka nchi zingine katika Jumuiya ya Afrika mashariki kama tatizo la ubabaishaji katika utoaji wa huduma katika sekta binafsi halitadhibitiwa mapema.
Note: Hapa tunazungumzia watu wanaotumia vyeti vya watu wengine ama bandia kupata kazi, pamoja na watu kupata kazi ambazo hawana sifa wala taaluma husika, jambo linalopelekea utoaji wa huduma mbovu zinazoathiri uchumi na ustawi wa taifa letu.