Waziri Ummy Mwalimu: Marufuku KULAZIMISHA Wajawazito kwenda Kliniki na Wenza wao

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Waziri kupitia mtandao wa kijamii wa X, amepiga marufuku wahudumu wa afya kuwalazimisha wajawazito kwenda kliniki wakiwa na wenza wao.

Ameandika
"Nimepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wajawazito kuhusu kulazimishwa kwenda Kliniki na Wenza wao. Hali inayofanya wengine "wakodi" wenza.

Kwanini walazimishe? Huu ni udhalilishaji mwingine kwa wanawake.

Sisi watoa huduma za Afya Tutoe elimu na hamasa kwanini mwenza aende na sio kulazimisha."

Screenshots_2023-11-30-18-56-57.png
 
Nao wamezidi kutafuta rushwa
Yaani kila mahali wizi
Na sheria nyingi zinatungwa na wafanyakazi na sio serikali
Kwa sababu wao ndio wanasababisha watu watunge sheria zao
Elimu inatakiwa na mabango kila mahali haya barabarani weka tu watu wajue haki zao
 
Huo utaratibu huwa siuelewi una malengo gani. Mimba iko kwa mwanamke, anaemhudumia ni nesi au daktari.

Haya, mimi mwanaume naenda kufanyaje yaani!!!
 
Sasa magonjwa si wanatakiwa wapimwe wote mke na mume??
AU atatibiwa mama kwa niaba ya bwana???
Uzinzi mbaya sana
Unampaje mimba/ujauzito mwanamke usieweza kutembea nae hata kwa ajili ya maendeleo yenu na familia/mtoto???
 
Back
Top Bottom