Habari wana JF,
Leo kumesikika habari kwamba waziri wa nishati na madini mh. Simbachawene ametoa agizo la kuchukuliwa hatua kali kwa wakuu wa idara ya ufundi wa Ilala na Temeke DSM. Mheshimiwa waziri, hali uliyokumbana nayo huko ndivyo ilivyo kwa nchi nzima. Kuhusu kitengo cha dharura nadhani TANESCO hawaelewi maana ya neno 'emergency' ukitaka kuamini hili wewe mwenyewe mh. jaribu kuchukua simu yako uwapigie uone kama utajibiwa. Unapiga simu ya 'emergency' mara tano bila kupokelewa! Hata kama watapokea ukiwajulisha tatizo wanachukua wiki nzima kufika (si kushughulikia tatizo leneyewe). Baada ya hapo hesabu wiki nyingine kulishughulikia. Yaani TANESCO inakera kupita kiasi. Wafanyakazi wake wamegeuka Miungu watu ukiingia ofisini kwao hawana hata muda wa kukusikiliza. Ni mengi sana tunayashuhudia sisi wananchi wa kawaida.