Waziri Mwigulu: Makato ya Miamala ya Simu tunatunisha mfuko, ni 'Solidarity Fund'

"Mtu anayetuma 1000 hadi 2000 anakatwa Tsh.10, anayetuma 20,000 hadi 30,000 anakatwa 960, Mil. 1 hadi Mil. 3 ni 9000 na Mil 3 na kuendelea ni 10,000, kwa anaetuma 100,000 hadi 200,000 anakatwa 2500, kama unaweza kutuma 10,000 kwanini usichangie shughuli za maendeleo?”

"Mimi naunga mkono dira ya Rais ya kutaka maji yapatikane kila kijiji, sasa tunafanyaje? tukasema tuchangishane, hivi unaona tunaweza kupoteza maisha ya Mtoto sababu ya maji, kisa unalia unakatwa Tsh.5?, mbona milio ya simu tunaweka na unakatwa Tsh. 100?"

"Kuna Shule zinakusanya watoto mpaka 1500 au 1000 na Shule haina maji wanaambiwa waende Shule na kidumu cha maji, sasa tunafanyaje ili maji yapatikane? ndio maana kuna uwepo wa kukatwa Tsh. tano kila unapotuma hela kwa ajili ya huu mfuko wa mshikamano"

"Watu wanalalamika kuhusu hela za miamala, hii ni solidarity fund, tuna mambo ambayo tunakubaliana hayapaswi kuendelea mfano ubovu wa Barabara vijijini, kama Taifa tuongeze Tsh.100 katika mafuta ili kila fedha itakayoongezeka iende kuleta maendeleo"

"Kwenye chungu, ni lazima bajeti, fedha zitatoka wapi ni lazima tutoe kodi, mwaka huu tumeleta kodi ya miamala, ni vizuri sana mjue hili la kwenye miamala sio tu kodi, hili tunatunisha mfuko, ni solidarity fund, huu ni mfuko wa mshikamano wa Watanzania"

"Akaunti zilifungwa kipindi kile kwasababu ya masuala ya kikodi na Wafanyabiashara wanarudishiwa fedha zao kwasababu akaunti imelipa kodi au hesabu zake zilipigwa vibaya kwahiyo kuna fedha ambayo haikuwa kodi inarudishwa"

"Kenya, Uganda, Malawi, Rwanda, Msumbiji mafuta yako bei juu kuliko sisi, ulishaona hizo Nchi waje kununua mafuta Tanzania?, nitoe rai Watanzania wawe Wazalendo kwasababu kwenye Nchi zote zinazotuzunguka Tanzania ndio Nchi inayouza mafuta bei ya chini"

Chanzo: CLOUDS 360
Mpaka Sasa , binafsi nalipa kodi sizopungua kumi, ila awa viongozi wetu wanalipa kodi, maana kwao kila kitu ni bure
 
Tz nchi ya hovyo sana. rasilimali nyingi sana lakini wanashindwa kuzitumia kupata kodi. waziri analinganisha TZ na rwanda kweli. hizo pesa si ndio zinatumika kujenga mahekalu ya marais wastaafu na kuhongana mabenzi. alafu mtu anasimama anasema hataki kodi za dhuluma. Hii dhuluma kwa wananchi wanyonge
 
Serkali ya kishetan iko madarakan chini ya muwakikishi delira na jopo lake la machawa wa bunge la ndugai....hovyo kabisa hii nch
 
"Mtu anayetuma 1000 hadi 2000 anakatwa Tsh.10, anayetuma 20,000 hadi 30,000 anakatwa 960, Mil. 1 hadi Mil. 3 ni 9000 na Mil 3 na kuendelea ni 10,000, kwa anaetuma 100,000 hadi 200,000 anakatwa 2500, kama unaweza kutuma 10,000 kwanini usichangie shughuli za maendeleo?”...

Ukitaka kuongeza mapato ya kodi kutokana na petroli, usiongeze kodi ya petroli...punguza kodi ya kununua magari !

Hivyo divyo watu wenye akili wanafanya. Boeing anauza ndege nyingi kwa hasara (au at cost price), kwa sababu anajua utanunua spea kwake na utafanya service kwake na utakarabati hio ndege kwake. Tigo anauza simu "at cost price" kwa sababu anajua atakubana kwenye hela ya vocha! Umewahi kujiuliza kwa nini printer ziko cheap lakini wino wake uko expensive...jibu hilo hapo.

Serekali yetu ina watu wavivu wasiojiongeza kubuni sera za kijanja.

Kwa haraka mabadiliko yanabidi kufanyika mfano;
- Kodi kwenye magari ya chini ya $1,000 itolewe( TBA should create tests to avoid TZ becoming a dumping ground ).
- kodi kwenye smartphone za chini ya 150,000Tzs itolewe...which has already been done (sort of) so AWESOME !
- Kodi itolewe kwenye Pay As You Go solar equipment (Zola, Devergy etc...)
- Kodi itolewe kwenye Mitungi ya gesi ya magari
- Kodi itolewe kwenye Majiko ya gesi ya chini ya Sh150,000
- N.k

...na hio kodi itumike vizuri, nimechoka kuona ma VX yamepaki masaa mawili matatu wakati engine imewaka na AC ipo full...
 
Kuna watu walikua wanajilinganisha na MO au DANGOTE sasa ngojea nisubiri nione kama MO na DANGOTE watasema kitu.

Solidarity Solidarity Solidarity ngojea niiingie studio nifanye HIT 1 niipe jina Solidarity😂

Tunisha Mfuko Mwananchi, vijiji vinahtaji barabarara/maji/umeme/nk na Zitaenda tu.

Na msipoziona hizo barabara nisisikie mnalalamika Sherehekeeeni kama mlivyokua mkisherekea Alivyotuacha JPM..

Viva Mama Viva mchaka mchaka chiiinjaaa....

#nabado
 
kwa hiyo unapenda vya buree eeehh!!!
unataka usadiwe na mataifa ya ulaya eeeh!!!
kumbuka pia misaada tunayo ipata kutoka nchi za ulaya ni KODI ZA WANANCHI WA MAREKANI, UGERUMANI, DENMARK, NEWZELAND, FRANCE, CHINA, UINGEREZA N.K, wananchi wazalendo wa nchi hizo wanatozwa kodi ambazo zingine ndio tunapewa ss misaada na wakati mwengine tunakopeshwa.
acheni kuwa walemavu wa akili lipeni kodi ili itusaidie maendeleo yetu.
Taifa imara itajengwa na sisi watanzania wenyewe kwa kulipa kodi sio kutegemea misaada au mikopo.
 
"Mtu anayetuma 1000 hadi 2000 anakatwa Tsh.10, anayetuma 20,000 hadi 30,000 anakatwa 960, Mil. 1 hadi Mil. 3 ni 9000 na Mil 3 na kuendelea ni 10,000, kwa anaetuma 100,000 hadi 200,000 anakatwa 2500, kama unaweza kutuma 10,000 kwanini usichangie shughuli za maendeleo?”

"Mimi naunga mkono dira ya Rais ya kutaka maji yapatikane kila kijiji, sasa tunafanyaje? tukasema tuchangishane, hivi unaona tunaweza kupoteza maisha ya Mtoto sababu ya maji, kisa unalia unakatwa Tsh.5?, mbona milio ya simu tunaweka na unakatwa Tsh. 100?"

"Kuna Shule zinakusanya watoto mpaka 1500 au 1000 na Shule haina maji wanaambiwa waende Shule na kidumu cha maji, sasa tunafanyaje ili maji yapatikane? ndio maana kuna uwepo wa kukatwa Tsh. tano kila unapotuma hela kwa ajili ya huu mfuko wa mshikamano"

"Watu wanalalamika kuhusu hela za miamala, hii ni solidarity fund, tuna mambo ambayo tunakubaliana hayapaswi kuendelea mfano ubovu wa Barabara vijijini, kama Taifa tuongeze Tsh.100 katika mafuta ili kila fedha itakayoongezeka iende kuleta maendeleo"

"Kwenye chungu, ni lazima bajeti, fedha zitatoka wapi ni lazima tutoe kodi, mwaka huu tumeleta kodi ya miamala, ni vizuri sana mjue hili la kwenye miamala sio tu kodi, hili tunatunisha mfuko, ni solidarity fund, huu ni mfuko wa mshikamano wa Watanzania"

"Akaunti zilifungwa kipindi kile kwasababu ya masuala ya kikodi na Wafanyabiashara wanarudishiwa fedha zao kwasababu akaunti imelipa kodi au hesabu zake zilipigwa vibaya kwahiyo kuna fedha ambayo haikuwa kodi inarudishwa"

"Kenya, Uganda, Malawi, Rwanda, Msumbiji mafuta yako bei juu kuliko sisi, ulishaona hizo Nchi waje kununua mafuta Tanzania?, nitoe rai Watanzania wawe Wazalendo kwasababu kwenye Nchi zote zinazotuzunguka Tanzania ndio Nchi inayouza mafuta bei ya chini"

Chanzo: CLOUDS 360
mwambieni MWIGULU akitaka kufanikiwa ashirikiane na wadau wanaotoa mawazo yao na wayafanyie kazi. mfano #KATIBAMPYA hii si kwa faida ya mtu binafsi au kikundi cha wajanjaa fulani... hapana ni kwa ajili ya WATANZANIA WOTE AKIWEMO NA YEYE. sasa waendelee kujifanya hamnazo hawasiki wanachoambiwa .
TUSILAUMIANE
 
WANANCHI WA MAREKANI NA NCHI ZA ULAYA ZINAWASIKIA WATANZANIA kuwa hawataki kulipa KODI ETI WANATAKA WASAIDIWE!!!!
AISEE!
NGOJA WANACHI WENZETU WATUSIKIE! SIJUI WATATUONAJE, KWELI TUMEKOMAA AU TULIDEKEZWA MPAKA UKUBWANI?!
 
Liongo hilo limwigulu mkeka ni huuView attachment 1854876
Screenshot_20210715-103850-1.jpg
 
Namuunga Mkono Dr. Mwigulu, anasema ukweli mtupu, kwa mie niliesafiri nchi nyingi za jirani na mbali Mafuta karibu nchi zote majirani sisi tuko cheaper, sasa kuongeza tshs 100 kwenye mafuta sioni tatizo kabisa. Tunahitaji barabara nzuri vijijini jamani
 
Mtu kama ww anza kupiga esabu zako kwa mwezi unatumia shilingi ngapi kwa matumizi yasiyo ya lazima?. Siyo kila mmoja analalamika ni wachache na wanafiki mnampongeza mama na huku mnataka miujiza. Bila kuchangia chocho ila kwa michepuko sasa
 
Kuna siku nilisikia huyu mama anasema alisoma uchumi, mpaka unashangaa pamoja na taaluma yake hiyo ameshindwa kutambua kuwa kuongeza kodi ya dhuruma kwenye miamala ya simu ni kuuwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Serikali na wachumi uchwara wanakaa wanaweka jumla yakodi tatu kwenye muamala mmoja wa simu hizi si dharau za waziwazi nakutuona mazuzu ,wanapandisha kwa makusudi bei ya mafuta kitu ambacho ni kichocheo namba moja cha ushughuli za kiuchumi nchini.

Jambo la kuchekesha zaidi nikaona hapa hakuna kiongozi nikupunguza kodi kwenye vitu ambavyo havina tija kwenye uchumi wa nchii, yaani mtu anapunguza kodi kwenye betting/gambling ,pombe halafu anapandisha tozo kwenye gharama ya mafuta.

Yaani mama katika vipaumbele vyako vyote kwenye shughuli za kiuchumi nikuchochea kamali na unywaji pombe, vingine vyoote umepiga chini. Watu wanasema mwigulu anakufanyia hujuma sio kweli vitu vidogo kama hivyo havihitaji mpaka usome macro economics yaani umepwaya kweli kweli.

Oky kodi mmeshaanza kuchukua jee zitasaidia vipi wananchii kama sio kuibia masikini, Mama ebu rejea bajeti ya ofisi ya waziri mkuu ya mwaka 21/22 asilimia 80 ya bajeti yote ni matumizi binafsi asilima 20 ndio inapelekwa kwenye shughuli za maendelea.
Matumizi binafsi wanalipana posho mara mbili mbili, vikao visivyo na tija, wanakula bata huku wakiaacha raia kwenye janga la umasikini.

Uongozi mbovu,, muundo wa serikali mbovu, bunge bovu, katiba mbovu

Sent using Jamii Forums mobile app
View attachment 1855593
 
Back
Top Bottom