Waziri Mkuu Pinda kuhutubia bunge la katiba kabla ya upigaji kura rasimu

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Dakika chache zilizopita wajumbe wa bunge la katiba wametoka ukumbini kupewa maelekezo juu ya upigaji kura za rasimu ya katiba. Wameambiwa yafuatayo:

1. Waziri mkuu Pinda kesho saa tatu asubuhi atawahutubia wabunge kabla ya rasimu iliyorekebishwa kuwasilishwa tena. Agenda anayo mfukoni lakini inadaiwa agenda kuu ni mahakama ya kadhi ambapo Chenge amegoma kuiweka katika rasimu. Pinda atatumia hotuba yakr kuwapoza waislamu na kuwasihi wasigomee kupiga kura pamoja na kwamba mahakama ya kadhi haimo katika katiba.

2. Upigaji kura utaanza saa tisa jioni kesho na kumalizika keshokutwa jumanne. Kila mtu atatajwa na kupigia kura sura kumi kesho na zile zinazobaki zitapigiwa kura jnne.

3. Jumatano ni siku ya kufanya maridhiano kwa ibara zote zitakazokosa theluthi mbili. Maridhiano yatafanyika kwa waliopinga kupewa nafasi kutoa hoja zao na kamati ya uandishi na uongozi kutoa ufafanuzi na kisha kura kupigwa tena. Zitapigwa mara tatu na kama theluthi mbili ikikosekana itahesabika kuwa ibara hiyo imekataliwa.

4. Hii ni mengineyo: upo ugumu wa kupata theluthi mbili toka zanzibar kutokana na mgawanyiko mkubwa uliopo. Hotiba ya PM huenda ikasaidia ku-address hili pia. Kuhusu mahakama ya kadhi hali ni tete zaidi ya kawaida. Ndio sababu PM amepewa muda kesho asubuhi kujaribu kuweka ushawishi wa mwisho.

5: Kuna taarifa kuwa hatimae swala la migomo ya wafanyakazi limeingizwa katika katiba baada ya wafanyakazi nao kupanga kususa kupigia kura rasimu nzima kesho.

Nikipata mapya toka hapa dodoma usiku huu nitawawekeeni hapahapa. Kuna vikao kadhaa vya kuweka misimamo vinaendelea usiku huu sehemu kadhaa.
 
Yale yale ya kujifanya kuzindua Bunge wanatangaza msimamo wa chama chao. upigaji kura na hotuba wapi na wapi !!!?
 
jme very good question. Jana waziri kabaka alipewa nafasi kujibu swala la migomo ya wafanyakazi lakini katika bunge la katiba hakuna waziri yoyoye anayetambulika. Wanafanya kulazimisha mambo
 
Last edited by a moderator:
Pinda na ccm yake wamefika mwisho. Usanii wa kikwete kumuanzisha warioba kuhutubi bunge ili yeye amalizie ndio unaendelea. Kwa sara za watz nakuakikishia nchi itapata matatizo makubwa saana lakini mwisho mungu atatupeleka nchi ya kanaani
 
Anahutubia bunge wakati wazanzibar wamo kwenye bunge na yeye hana mamlaka yoyote kwa nchi ya zanzibar.
 
Kwaiyo Pinda ameona ni vyema kuwaunga mkono wakiristo kutokuwepo Mahakama ya Kadhi lakini waislamu waje wapigwe domo ili yaishe?

Hii nchi ina unafiki wa hali ya juu kabisa kwani hiyo Mahkama ya kadhi wakiristo wao inawasaidia nini wakati waislamu wenyewe kwa wenyewe ndio taratibu zao? au ndio mfumo kiristo umepamba moto? Waislamu tusikubali kama hakuna Mahkama ya Kadhi tokeni nje hamna kura
 
Si kama laki tatu za kila siku wamebakza siyo zaidi ya milioni mbili. Naomba waislamu wakomae na kadhi alafu wakristo nao waigomee ili katiba ya 6 ibume
 
Back
Top Bottom