Waziri Mkuu - Naomba Urudi Tena Bukoba!

Ericus Kimasha

JF-Expert Member
Oct 27, 2006
488
470
Mh. Kasim Majaliwa,

Pole na majukumu na asante kwa ujio wako Bukoba kujulia hali, kufariji na kuaga miili ya wahanga wa tetemeko la ardhi.

Nimelazimika kukuandikia hapa baada ya jitihada zote za kukufikishia ujumbe wa haraka kushindikana. Kupitia hapa nina imani kuwa Ndg. Lizaboni na timu yake watakufikishia tu nakala ya barua yangu. Na nimejifunza jambo ambalo lilikupendeza basi kitengo cha maafa kilicho chini ya mamlaka yako kianzishe njia ya mawasiliano (hotline) isiyo na mlolongo pale muhanga anapotaka kufikisha taarifa za haraka katika kitengo.

Naomba kuleta katika ufahamu wako kuwa ziara uliyofanya Bukoba haijaleta tafsiri nyingine zaidi ya kuamini kuwa ulifika kwa lengo la kuzika maiti na si kusaidia wahanga. Baadhi wanaamini hivyo kwa kuwa, kwa baadhi ya marehemu hakukuwa na uharaka wa kimila, kidini wala kitamaduni uliokuwa unalazimu mazishi yafanyike kwa haraka kiasi kile. Wengi walidhani kuwa ujio wako ulikuwa wa kuangalia jinsi gani misaada ya kibinadamu ingewafikia haraka wahanga. Ni masikitiko yangu kukufahamisha kuwa mpaka usiku wa kuamkia leo hakukuwa na hema wala shuka ambalo lilikuwa limitolewa kwa msaada wa kitengo cha maafa kilicho chini ya ofisi yako!

Baada ya kuwa katika mtanziko wa kuonekana janga hili halijapewa kipaumbele kinachostahili, watu katika makundi mbalimbali ya kijamii walikuwa wameanza jitihada za kuchangia maafa haya. Shughuli za uhamasishaji zilikuwa katika hatua nzuri mpaka pale taaarifa ya Serikali ilipotolewa Bungeni kuwa misaada yoye ipitie kwa Mkuu wa Mkoa. Sehemu ya uamuzi huu yaweza kuwa na nia njema. Lakini tunajiuliza kama imechukua Wizara yako siku nne kushindwa kutumia bajeti iliyo chini ya kitengo cha maafa kusaidia wahanga, itachukua siku ngapi misaada itakayopitishwa kwa Mkuu wa Mkoa kuwafikia walenga? Na Je, itakuwa misaada ya kusaidia wahanga au kuzika wafu?

Binafsi nimejaribu kufuatilia kulegalega kwa Serikali na Uongozi wa Mkoa katika kufikisha misaada kwa walengwa kumetokana na nini? Nimebaini yafuatayo:

Wakati wananchi tukilichukulia tetemeko la ardhi kama janga kwa maisha ya watu, watendaji na viongozi wa kisiasa Mkoani Kagera wanalishughulikia kisiasa. Badala Baraza la Madiwani wakae pamoja na viongozi wa Mkoa katika kupanga na kushughulikia suala hili, wao wamegawanyika pande mbili. Upande mmoja una Baraza la Madiwani, Meya na Mbunge wao. Na upande wa pili uko na viongozi wa chama Tawala na wa Kitaifa, Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya. Ukinzani wa makundi haya kutaka kujionyesha kundi lipi limeguswa zaidi unaathiri shughuli za uratibu na ukusanyaji wa misaada.

Kwa historia ya majanga makuu yaliyokwishaipata Bukoba, na kwa yanayoendelea katika uzorotaji wa Serikali kuonyesha jitihada za kuleta misaada ya kibinadamu, inachagiza hisia za watu kuamini kuwa Bukoba ni nje ya nchi kwa Tanzania.

Naamini ujumbe huu umefika. Na kama kwa jambo lihusulo Bukoba na maisha ya watu wake dola italitafsiri kama taarifa ya uchochezi, naomba Jeshi la Polisi lisipate taabu kunitafuta. Liniandikie kupitia ekimasha at Gmail.com kituo cha polisi au magereza ninayotakiwa kulipoti. Nitafika wakati na saa hiyohiyo.
 
Nimekuelewa vizuri mkuu. Namba moja aliahirisha ziara ya nje. Mpaka sasa hajafika kule?! Huenda wanangoja kauli na maelekezo yake
 
Umeandika vema sana mkuu. Umeshauri vema. Kwa hali ya kisiasa ilivyo nchini, hakika hali kama hii ya sasa hapo Bukoba lazima itokee. Kunategemewa hali ya kususiana, kuhujumiana nk. Sasa ni muda wa uongozi wa kitaifa kuwa kitu kimoja na kutumia zaidi busara katika ku-handle hiyo hali. POLENI SANA WANA-KAGERA. MUNGU WA MBINGUNI ATAFUNUA NJIA!
 
Atakujaje bila hela?wakipata misaada ndo watakuja,leo wemeitisha harambee
besti si tunaambiwa serekali hii inabana matumizi na kulundika hela kwenye hazina ama ni kwaajili ya madawati? Na zile hela zilizobanwa wakati hule wa sherehe ya uhuru. Basi inaonekana dhahir wazi kabisa hamna hela hazina. Hata takwim ya mapato TRA inayotoa kila mwez siyo ya kuaminika inaukakas.

Na labda pengine Kwasabab bukoba ni UKAWA na kama ni hivyo Mungu hatawasamehe viongoz wetu
 
Ni vizr misaada yote ipitie kwa mkono wa serikali siyo holela!
 
Nimelielewa sana bandiko lako mkuu!!Nimejifunza kitu kuhusu hii serikali katika baadhi ya mambo
Pathetic!!
 
Ni suala la aibu sana kwa serikali yetu, hakuna mhamko kabisa kuanzia serikali kuu, vyombo vya usalama na mpaka vyombo vya habari.
Sijasikia kauli yoyote ya Rais Magufuli, labda nipo nyuma ya muda.

Kitengo cha maafa ambacho kipo chini ya Ofisi ya waziri mkuu na kinapata fungu, sijaona msaada wake kabisa. Wanafunzi Ihungo na Nyakato wamelala nje badala ya kwenye Mahema.

Juzi wakati wanaaga miili uwanja wa Kaitaba, televisheni ya Taifa ambayo inatumia kodi zetu walikuwa busy wakionesha taarabu na tamthiliya...Shenzi kabisa. Dr. Ryoba inabidi awajibike kwa huu ujinga wao.

Jeshi la wananchi Tanzania kwao ni muhimu kufagia na kupanda miti kuliko uokoaji wa wahanga.

Nchi ya Kenya ndio imekuwa ya Kwanza kutoa misaada, serikali imelala usingizi wa pono.

Nimebaki njiapanda, mitaa yetu ya Kilimahewa nyumba nyingi zimeharibika hazifai kabisa, sisi tumepata nyufa kubwa tu. Serikali inabidi ifanye tathmini kwa umakini zaidi ili kuja na jibu sahihi kuhusu uharibifu.
 
Ilitumika kwenye kampeni.
Ni aibu. Barabara za magari zinaweza kupata bajeti ya ghafla kwa mtu mmoja tu kuamka na kubatilisha sherehe ya kitaifa na zikapatikana bilioni 4. Janga la tetemeko la ardhi ambalo limechukua uhai wa watu, limeacha majeruhi na kuharibu makazi tunakwenda kutembeza bakuli na kuchukua karibu wiki hatujafikisha msaada wowote kwa wahanga!

Tujitafakari sana; tunaishi kutafuta maendeleo ya vitu (e.g barabara) au watu?

Nitafurahi kusoma report ya ukaguzi wa CAG kwa Waziri Mkuu-Kitengo cha Maafa maana hali halisi inayoonyesha Kitengo hiki ni sawa na 'kisima kikavu'

cc: Lizaboni
 
Back
Top Bottom