Waziri Mkuu Majaliwa: Suala la mshahara ni siri ya mtu. Siyo lazima litangazwe hadharani

Ukweli utasemwa siku zote hata kama watu hamuupendi.
Siwezi kamwe kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa.Lipi nimesema hapo ambalo sio logic.Tatizo la Watanzania ni kwamba tunapenda kupindisha pindisha sana mambo na unafiki.Mimi sio mnafiki,I call a spade a spade.
Sawa Mr .. Sijui spade
 
hv sirikali hii inavyopenda kiki ipandishe mshahara isitangaze? ule wa buku jero tu ulitangazwa miez takriban sita. Hahaa poor me.....
 
Mbona wakifanya tukio dogo wanakimbilia kwenye media?
Why hii issue ya mishahara wanataka kufanya siri?
Hawa wameishiwa na hawana fedha sasa wamebaki kulalamika!
 
kirerenya Swali kwa waziri mkuu linahusu nyongeza ya mwaka ya mshahara (annual increment) hii IMO kwenye mkataba wa ajira; Waziri mkuu anajibu tofauti kuwa nyongeza ya meidai ya kila mwaka haitawekwa hadharani ni siri ya mfanyakazi!
 
Duh! Nchi ya maajabu kabisa hii!
Ni sahihi kusema kuwa mshahara ni siri ya mwenye kulipwa lakini bado kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria za ajira kwani masharti yanayotajwa na sheria hiyo yametupwa katika awamu hii.

Katika moja ya hotuba zake mkulu kakataza malimbikizo ya madeni ya mishahara kwa watumishi na aliagiza kuwa mtumishi akipata barua ya promotion alipwe kabisa kwa mwezi husika. Ni nini kimesababisha wale waliopandishwa tarehe moja April hawajalipwa hiyo mishahara mipya hadi leo?

Na watumishi walioorodheshwa na hazina na madai yao kuonyeshwa kwenye tofuti ya hazina ni kwanini hawajalipwa hadi leo? Au zile bilioni 200 zilizotolewa mkulu nazo zimekwenda kisikojulikana? Mh. Majaliwa analijua hili kuwa hakuna mtumishi yeyote aliyepanda daraja mwezi April hawajalipwa hadi leo? Au naye ni walewale?
 
kirerenya Huyu dingi inaonyesha hashirikishwi mambo mengi sana ya serikali japokuwa yeye ndo PM....pole sana ndugu Kassim.
 
kirerenya wamechanganyikiwa, nyongeza ya mishahara siri, mapato ya madini siri. vipi mapato ya TRA wataendelea kutangaza. tulijua tu ilikuwa nguvu ya soda. wameishiwa pumuzi
 
Hakuna siri kwenye mishahara, ukiongezwa hata kwa siri jioni nchi nzima ishajua,
 
Hili suala ni two ways traffic, unapomwambia mtu aongeze tija lazima umpe vitendea kazi vyote vya kufanyia kazi ili uwe na uhalali wa kudai tija. Wafanyakazi wengi wa serikali ni waalimu na watumishi wa wizara ya afya...... nenda kwenye maeneo yao ya kazi ujionee hali halisi halafu uniambie hiyo tija itaongezwaje?
Tija na ubora wa kazi kama hakina vitendea kazi hamna kitu (work done=0) , hivi unafikiri india wanatuzidi nini zaidi kwenye matibabu? Ni vitendea kazi tu!
 
Aliyoongea Waziri Mkuu ni sawia kabisa.Swala la kuongezwa mshahara ni siri ya mtu.Ni kweli pia kwamba nyongeza za mishahara zikitangazwa hadharani,bei zinapanda mno mpaka kufikia hata kiwango cha ku-nullify hiyo nyongeza yenyewe.Haya tumeyaona huko nyuma.

Hata hivyo watumishi nao wasiishie kudai increments tu na kupandishwa madaraja,waongeze tija,jambo ambalo limekuwa kero sana kwa serikali.Hii itaipa hata serikali incentive,morale na enthusiasm ya kuongeza mishahara na kupandisha madaraja.[/QUOTE
Tija bila vitendea kazi? Srikali ingekua serious kununua vitendea kazi kama inavyonunua versions za Landcruiser VX tungekua mbali sana hasa sekta ya afya!
 
Hayo madeni mnayolipa kwa watumishi mbona mnatangaza au hizo hela hazihitaji siri na hayo manoti mnayo toa hadharani mkiwa juu ya magari yenyewe hayana athari kwa jamii. Yaani awamu hii SIFA yashinda SIRI. mkishindwa kufanya jambo mnasingizia jamii itawaelewaje mkilimudu jambo mnaisahau hiyo jamii ma kwamba kuna siri.
 
Asiye na Chama, nimesema naelewa mazingira ambayo wafanyikazi wanafanyia kazi,ikiwa ni pamoja na upungufu wa vitendea kazi.Lakini ni kweli kwamba mazingira ya kazi ndio tatizo tu,au kuna matatizo pia ya uzembe,lack of initiative,juhudi,weledi,
uaminifu nk.kwa upande wa wafanyakazi ambayo wangeweza kuya address ili kuongeza tija?Jibu ni ndio.Kama ni hivyo,basi watumishi waya address, ili serikali ipata enthusiasm ya kuongeza mishahara na kupandisha madaraja.
 
Najua mazingira yote ya wafanyikazi wa Tanzania na kwamba kweli sio mazuri sana kihivyo.Lakini hivi unaweza kuniaminisha kwamba elimu duni wanayopata watoto wetu haiwezi
ku-improve katika mazingira yaliyopo kama waalimu watajituma zaidi?Je,wagonjwa wetu hawawezi kupata better care and treatment katika mazingira yaliyopo?Je,wakulima wetu hawawezi kupata ushauri bora zaidi kutoka kwa VEOs katika mazingira yaliyopo kama VEOs watajituma zaidi na barabara zetu haziwezi kuwa bora zaidi kama road engineers wetu watakuwa waaminifu na makini zaidi nk.nk.? No,nathani there is room for improvement, ila hakuna nia ya dhati,uwezo au ubunifu wa kutosha wa kufanya hivyo.Tupo Tanzania wote, we know this is true,but there is no initiative and will to do not that!Yes, hii kitu ni two way traffic,lakini reason must prevail,mwajiriwa ndiye wa kuchukua the first step.Tusisahau kwamba mwajiri ndiye kashika mpini.
Na moyo wa wafanyakazi unakufa zaidi pale ambapo wanasiasa wanaopiga blaa blaa ndio wenye maisha mazuri, wanaabudiwa na wanawapiga mkwara wafanyakazi na kufanya mahali pa kupatia kiki za kijinga!
 
Back
Top Bottom