Waziri Masauni tupunguzie Traffic Polisi barabarani

Ukipunguza unafiki na uzandiki utasaidia kupunguza ulemavu na vifo vitokanavyo na ajali na hutoona hakuna ulazima wa trafiki

We ni kilaza mmoja ambaye hujatembea hata nchi moja iliyoendelea.

Ajali za barabarani lawama zinatupwa kwa madereva tu, ukweli hausemwi barabara zetu ni mbaya, mbovu na nyembamba.

Uwepo wa trafiki hauna maana kabisa Serikali inajificha kwenye shamba la karanga.

Kuna nchi ukienda utakaa mwezi mzima na hutaona trafiki wala kusikia honi ya gari wala pikipiki.

Acheni rushwa tunajua mnapewa malengo ya kukusanya na kupelekea mabosi zenu gawio kila jioni, na mnaambiwa kila siku hakikisha umepiga faini gari zisizopungua 10.
 

Mnataka traffic wapungue barabarani ili muendeshe magari vichwa vyenu vikiwa nje ya gari?
Tunataka tufanye BIASHARA na tushindane na nchi Jirani huku tupunguze gharama za uendeshaji. Huu mradi wenu wa kukusanya fine bila kufanya kazi ni mwizi kuibia raia na makampuni na tunapinga rushwa. Hatutaki watoto wakue wakute rushwa ni halal sie tumefundishwa rushwa ni adui wa haki
 

Mnataka traffic wapungue barabarani ili muendeshe magari vichwa vyenu vikiwa nje ya gari?
Wanaondesha magari vibaya ni madereva wenu wa serikali na majeshi yenu wao hata afisa akiwa anaenda nyumba ndogo ni misafara na kutanua. Miundo mbinu yenu ni wizi mwendazake kajenga barabara njia 8 na bado Polisi wenu wanadangia humo humo
 
Miaka ya 2010 World Bank walitoa ripoti ya kufanya biashara nchini Tanzania na kwa viwango vya wakati ule tulishika nafasi kama ya 121 kama sijakosea. Raisi wa wakati ule Mh. Jakaya hakuridhishwa na hiyo ranking na kuchukua hatua at least tufikie 2 digits yaani tuwe chini ya 100. Majirani zetu kama Kenya na Rwanda walituacha mbali mno katika mazingira mazuri ya kufanya biashara.

Mh. Raisi aliunde task force kuhakikisha hatua zinachukuliwa haraka kuhakikisha mazingira ya Biashara yanakuwa bora Zaidi. Nakumbuka TPSF walishika hatamu katika kuratibu baadhi ya Task force uhsusan zile zilizokuwa zinawagusa wafanya biashara. Maarufu ni ile ya Trade Across Border ambayo iliangazia corridor ya kusini kwa maana barabara ya Dar – Tunduma na ile ya Kati Dar – Lusumo. Kiukweli kwa wakati ule hatua zilichukuliwa na One stop Border zilianzishwa, Mizani ya kisasa ikajengwa na Mzani wa Kibaha ukahamishwa Vigwaza na Zaidi kuondosha barriers Zaidi ya 52 kuelekea Lusumo.

Kwa masikitiko makubwa kabisa Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ndio walikuwa waratibu wa task force hii na kibaya Zaidi Waziri Mh. Masauni ndio aliyekuwa Mwenyekiti wa Task Force na alikuwa Naibu Waziri wakati ule sijui kwa makusudi au kwa bahati mbaya ameachia askari polisi kuongeza vituo barabarani tena Zaidi ya mara 10 ya vilivyokuwepo wakati ule. Inawezekana kabisa askari wake hawajui lolote kuhusu mazingira na kero za kufanya biashara nchini lakini yeye Mh. Waziri arejee makablasha yake na afanye Tathmini usumbufu unaoletwa na Jeshi la Polisi barabarani.

Usumbufu wao ni ule ule unaolalamikiwa miaka yote, kwanza kupotezea watu muda wa kusafiri na kufikisha mizigo kwa wateja, Pili kushawishi na kupokea rushwa, kubambikia madereva makosa na Zaidi ni kuipaka matope nchi yetu kwa kutoonyesha weledi kazini na Rushwa. Haina maana askari wasiwepo barabarani la hasha waweke vituo vya ukaguzi vichache na vinavyoratibiwa vizuri kama wenzetu wanavyofanya. Ili muda wa maroli na mabasi kukaa barabari upungue. Chukueni mfano Morogoro Road – ukimaliza kibamba tu unaanzia Gogoni wapo, kiluvya madukani wapo, kibaha maili moja wapo, Tanita, Miomboni, Visiga, Msufini, Ruvu, Vigwaza, Chalinze na Mwidu hii ni mkoa wa Pwani tu.

Kila palipo na kituo cha polisi basi lazima wakae na barabarani kuzui magari, na hapa hatujaweka wale wa Torch, wa kukusanya maokoto na waungwana wachache wanaokaa kwenye Zebra. Hivi hakuna namna tunaweza tuka mechanise au modernize kazi za hawa jamaa wakatuacha barabarani tusafiri kwa amani. Pamoja na wingi wote huu wa askari barabarani bado wazee wa busta (pikipiki zinazobeba mkaa zinapita mbele yao) wao ni kila Fuso, Truck lazima wasimaishe na kuuliza kama unacheti ukisema hauna wakupige cheti.

Mh. Waziri wa mambo ya Ndani tunakustua tazama tena jeshi la Polisi hasa wanaosimama barabarani, na ukumbuke Rushwa ni adui wa haki tunajua Takukuru hawanaga meno na wala hawaoni lakini sie wananchi, wafanyabiashara, madereva na wakulima tunaumia sana na mapungufu ya watendaji wa Jeshi la Polisi. Tunamkumbuka Hayati mwendazake sababu wakati wake huu uzembe hakuwa na nafasi sasa umerudi kwa kasi mno sijui wamewazoea nyie viongozi wao au wanawamudu??.

Mh. Waziri ikukupendeza kadurufu tena kuhusu Doing Business Road Map 2010 na Tasks Force alizounda Mh. Jakaya Kikwete na wenyewe mjitathmini na kama wakati ule tulikuwa 121 hivi leo tumeshika namba ngapi. Tunajua Bwana Simbeye hayuko TPSF leo lakini Kaacha makablasha yoyote huko watangulizi wake waanzie watizame na wapate pa kuanzia Vipi kuhusu TCCIA, na wadau wengine au wamemuachia Mungu au na hili tumtafute Bashite.
Njaa kali hao majamaa
 
Idadi ya traffic polisi inatakiwa kuongezeka ili wananchi waache ukondoo
Duh! Waongezeeni maarifa Hawa mlio nao kwanza wajitambue na waache rushwa. Wapeni technolojia makondoo ni Hao traffic wanasimamisha gari moja na wanauliza maswali hayo hayo katika vitu zaidi ya 20 ndani ya km 200. Hii nchi ni ya kwetu sote na tunajua hamtaki mawazo tofauti na yenu lakini lazima tuweke record Sawa kwamba tuliwakumbusha na mnachofanya tunakiona
 
Duh! Waongezeeni maarifa Hawa mlio nao kwanza wajitambue na waache rushwa. Wapeni technolojia makondoo ni Hao traffic wanasimamisha gari moja na wanauliza maswali hayo hayo katika vitu zaidi ya 20 ndani ya km 200. Hii nchi ni ya kwetu sote na tunajua hamtaki mawazo tofauti na yenu lakini lazima tuweke record Sawa kwamba tuliwakumbusha na mnachofanya tunakiona
Mkuu unanionea mimi. Siko huko
 
Maili Moja trafic,kiluvya traffic,kwa Komba traffic,Luguruni traffic,Temboni traffic,bucha traffic,, UBUNGO maji traffic kudadadeki
 
Back
Top Bottom