Waziri Lukuvi Atenguliwe na Kupandishwa Kizimbani Kwa Robbery?. Mahakama Zimekuweje?!. Sasa Pesa Ndio Kila Kitu!.

Bro mayala correct me if am wrong.
Army robbery ninavyojua mi ni wizi wa kutumia silaha hapa unasema kwamba kosa la kumpiga mtu kabali ni army robbery.
Je stealing by force inakuwa wapi??!!
Mi sielewi ila nauliza tuuu wajameni
Kumbuka hata karamu ya kuandikia inaweza geuka ikawa weapon ,,
 
Mda mwingine pascal mayala uwa anaongozwa na hisia binafsi kuliko uhalisia kama mahakama inavoitaji kuthibitishia pasipo shaka na watuhumuji kuwa kosa lilifanyika na sio hisia tukienda kihisia nani atapona mayala?uwaga napenda kusema makala zake apa jukwani coz uwaga anajitahidi kujenga hoja kutetea anachokiamini ila leo sijui sherehe imembana au hana hoja kujibu wadau waliojitokeza kuonyesha upande mwingine wa hisia zake si sahihi mbele ya sheria ya ushahidi.......
Hakuna sehemu yoyote ambapo mahakama imesema Lukuvi ni mkabaji, wala alinyang'anya hilo fuko la fedha.Mahakama imesema ushaidi ni dhaifu,na mahakama haiwezi kuzingatia ushaidi dhaifu na wa hisia tu uliotolewa na serikali.Inawezekana kuwa hiyo kweli ilikuwa rushwa,bado pia inawezekana yalikuwa ni makubaliano ya watu wawili wapeane kiasi tajwa,lakini waziri akamgeuka mwenzake ili aonekane ni msafi mbele ya mfalme na umma.Kama ofisi ya umma kubwa kama ya waziri haina cctv kamera,basi hii ni nchi ya ajabu,pia kama ipo na haikunasa hilo tukio basi hilo fuko la fedha ni la ajabu likiingia ofisini kamera zinazima mithili ya ndege ya Air force one na rada zetu za ulimwengu wa tatu.Mayala karibuni tu walikupongeza kwa kuhitimu shahada ya sheria ,je ungekuwa hakimu ungetumia ushaidi wa hisia tu?,vipi kuhusu ushaidi wa cctv kamera unakubalika mahakamani au haukubaliki,na kwanini haukuwasilishwa?.
 
Wizara ya Ardhi na maendeleo ya makazi ni mojawapo ya wizara nyeti na yenye changamoto nyingi sana!
Lukuvi amethubutu kuondoa kero na kuboresha mifumo mibovu kwa manufaa ya umma!
Kwa kufanya hivyo amekuwa ni threat na kuonekana kikwazo kwa wale wenye hila na uovu!
Kanakwamba kuna Watu wapo kutaka kusikia Siku moja akipata kashfa au mabaya ili apndolewe pale maana wanamuona Kama kikwazo kwa mambo yao walozoea ya kidhulumat!
 
Sijui udhaifu wake wa ndani!
Lakini nathubutu kusema ktk mawaziri ambao wana "add value" Kwenye kutumikia wananchi basi Willium Lukuvi ni mmojawapo!
Adumu Lukuvi!
 
Labda Lukuvi alitengeneza movie baada ya kuona yule Ofisa wa TRA wa Kilimanjaro anasifiwa na Rais kwa kukataa hongo na yeye atasifiwa!

Halafu siku hizi njaa kila sehemu na watu wana hasira na Serikali, hivyo si ajabu mawakili wanawakomoa viongozi waandamizi wa serikali kufidia hasira zao.

Kwa ufupi, mambo ni mengi.
 
Sijui udhaifu wake wa ndani!
Lakini nathubutu kusema ktk mawaziri ambao wana "add value" Kwenye kutumikia wananchi basi Willium Lukuvi ni mmojawapo!
Adumu Lukuvi!
kuna mwingine alidhulumu misamaki ya watu nchi ikaingia loss kubwa likini yupo tu, na mwingine aligoma kulipa kodi ya makontena mchana kweupe na akatishia kuloga watu kwa laana, lakini bado yupo ofisini wala hajisikii vibaya.
 
M
Wanabodi
Merry Christmas.
Leo tumeanza sikukuu kwa habari kubwa hii ya mtuhumiwa wa Lukuvi kuachiwa huru. Kesi yenyewe ilikuwa simple, Lukuvi kadai mtuhumiwa ametaka kumhonga
Milioni 90. Lukuvi akazipokea na kumuitia polisi akawakabidhi ushahidi wa fuko la fedha, kesi ilipoanza kuunguruma, mtuhumiwa akasema ni Lukuvi alimkwida akamniga, akamkaba, akampora fuko lake la fedha. Mahakama imemuamini na kumuachia huru. Hivyo hili ni bandiko la swali jee Waziri Lukuvi Atumbuliwe na kushitakiwa kwa ukabaji?.


Mkuu Mwana Mwana, asante kwa taarifa hii. Japo mawakili ni watu wazuri sana katika kutetea haki, lakini pia ni watu wabaya sana katika kupindisha ukweli na kununua haki kwa wateja wao.

Mimi naamini jamaa alikwenda na fuko la fedha ofisini kwa Lukuvi na alitaka kumhonga na Lukuvi akazipokea na kuwaita Takukuru wamkamate red-handed. Jamaa akakamatwa.

Jamaa akaweka wakili smart lawyer, Imani Madega, wakili akamshauri kwa vile walikuwa wawili tuu mule ofisini, then wakaamua kutumia tricks ya "your words against mine", jamaa akamgeuzia kibao kuwa waziri Lukuvi alimkaba na kumpora fuko la fedha. Na kwa vile hakuna shuhuda mwingine yoyote, then mahakama ikatoa hukumu kwa mtindo wa "aliyekutwa na ngozi" na kwa kesi hii aliyekutwa na fuko la fedha ni waziri Lukuvi, then mfanyabiashara akashinda!.

Siilaumu mahakama kwa sababu msingi wa haki kwa sheria zetu ni presumption of innocence until proven guilty beyond reasonable doubt, and the one who allege must proove, serikali imeshindwa kuthibitisha kosa hivyo Lukuvi ni mkabaji. Hivyo Hapa siilaumu mahakama bali naishangaa!.

The common sense logic inaelekeza mtu huwezi kwenda ofisini kwa mtu na large amount of cash money kiasi hicho just like that bila kuwa na motives behind.

Haiwezekani mtu umkabe na kumpora fuko la fedha halafu mporaji uite polisi kumkamata uliyempora. Japo ameshinda katika hukumu ya kidunia, hukumu ya karma inamsubiri. Kwa wanaomfahamu huyu jamaa kwa karibu mfutuatilieni nini kitamtokea.
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako! - JamiiForums

Sasa kama hukumu hii ni ya haki, then rais Magufuli kuonyesha anaiheshimu mahakama, hana budi kutengua uwaziri wa Lukuvi ASAP na kufikishwa Mahakamani kwa ajili ya kuhukumiwa kwa kosa la armed robbery, mawazi wote are armed, ambalo halina dhamana na hukumu yake ni kifungo cha miaka 30 jela.

Japo sina uhakika na pecuniary jurisdiction ya mahakama iliyotoa hukumu hii, lakini kwa siku za hivi karibuni, mahakama zetu zimekuwa zikitoa hukumu za ajabu kwa majangili wenye fedha kwa kuwahukumu kulipa faini, lakini hukumu ya jana kiboko, kumbe waziri Lukuvi jambazi, kabaji?!.

Ila pia pesa ndio kila kitu.
P
Msiwe mnaendeshwa kwa hisia zaidi fikirieni kuwa kama mngekuwa nafasi ya hakina mngemfunga mtu ati kwa kuwa alikuwa na kiasi hicho cha pesa,vipi kama mtu alikuwa na mishe zake gjafla akaitwa huku.akiwa na hizo pesa kuna ulazima yeye kuficha wakati anaenda kwenye ofisi ya serikali je alikuwa na kosa au kizingiti kumfanya yeye atoe rushwa sasa kama hakuna ushahidi unamwekaje mtu ndani.nadhani hisia ndio zinawafanya watu kuonewa kuliko makosa yao,kesi nyingi za uhujumu uchumi na rushwa zimegubikwa na hisia kuliko facts.kama hakimu angekuwa mwoga bila shaka angeogopa serikali lakini ameona haki itendeke hata kama mbingu zitaanguka.
 
Je akipotezwa na wasiojulikana nayo itakuwa ni Karma?
Je TRA wakimfuatilia kama Kakobe nayo itakuwa ni Karma?
Je akikutwa na Nyara za Serikali kama ndugu yake Rostam Aziz nayo itakuwa ni Karma?
Ila kutoka kwenye sakafu za akilini mwangu naamini kabisa huyo jamaa alikwenda kumhonga huyo waziri. Ila mahakama nayo imezingua kwenye hiyo tafsiri ya eti alimkaba na kumnyang'anya hiyo midolali na kuita Polisi.
Kwa jinsi Mahakama ilivyoumaliza huo mchezo hapo lazima waziri aliwekewa mtego kwa 'Maagizo Kutoka Juu'. Ndiyo maana kesi imeisha kizushi kwa stering kufia kwenye maua, huyo jamaa alitumiwa tu.
Hivi Lukuvi hajawahi tofautiana na Bashite mahali kweli?
Presumption,Probability,opinion, in law never construct positivism's findings.
 
Pascal Mayalla nilijua unajua kesi nyingi zinazousiana na rushwa kumbe hujui kitu,Umesahau mwanzo kabisa ili kudhibitisha mtu umempa rushwa hao PCCB walikua wanakupa fedha zao wanaandika namba wakizikuta kwa mtuhumiwa baada ya kutengeneza mazingira ndio inadhibitishwa jamaa kapokea rushwa lakini mkipeana hela huko ukaja na police wako na Takukuru kwa hela zenu hakuna kesi hapo ila kwa waandishi habari itaonekana ni kesi kubwa maana mnatoa hukumu kabla ya kesi...
 
Kwenda na pesa ofisini sio kigezo au hoja kuntu kuwa alienda kumhonga, Wafanyabiashara hutembea na fedha nyingi na wengine hutembea na hadi mabilioni kwenye magari n.k, na ni kweli ushahidi unakuwa mgumu sana kumtia hatiani mtuhumiwa sababu hapo ofisini walikuwa wawili na wote wanaweza kusema uongo pia
Sawa lakini huyo aliye porwa mbona hakwenda kushtaki kuwa ameporwa? Au mimi siyaelewi mambo vizur?
 
Back
Top Bottom