Waziri Dkt. Ndumbaro atembelea kambi ya Singida Fountain Gate, Cairo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro @damasndumbaro_official ametembelea Kambi ya Timu ya Singida Fountain Gate iliyopo Cairo Misri ikijiandaa na mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Timu ya Future utakaochezwa Oktoba 1, 2023 Cairo nchini Misri.

Dkt. Ndumbaro ametembelea Kambi hiyo Septemba 28, 2023 baada ya kumaliza Mkutano Maalum wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika uliofanyika nchini humo Septemba 27, 2023.

Akizungumza na wachezaji hao amewaasa wacheze mpira wakiwa kwa kufuata maelekezo ya benchi la ufundi na kanuni za mpira ili kupata matokeo yatawapeleka hatua ya makundi.

"Tunawashukuru sana kwa kutuletea heshima nchi yetu na ninyi wenyewe, tusimwangushe Rais Samia Suluhu Hasani, sasa ni zamu ya Tanzania kwenye michezo, sasa ni zamu Singida Fountain Gate" amesema Waziri Dkt. Ndumabaro.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Misri Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema furaha moja huongeza nyingine na amewatakia wachezaji hao ushindi mwema.

Naye Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Wallace Karia amesema Tanzania imekuwa na mwendelezo mzuri ambapo timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars imefika hatua nzuri ya kufuzu WAFCON na kupata fursa ya kuwa mwenyeji wa AFCON 2027 kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.

Aidha, Rais wa Singida Fountain Gate Bw. Japhet Makau ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wa maandalizi ya Safari na mapokezi mazuri kutoka ubalozini Misri na kusisitiza kuwa Timu ipo salama na inaendelea na mazoezi kuelekea mchezo huo.

F7HDeMxWwAA9XUZ.jpg
F7HDelbWAAA_Fn8.jpg
F7HDez9XEAAuCc4.jpg
F7HDfEmWUAA-ozN.jpg
 
Back
Top Bottom