Waziri Biteko anakosa mshauri wa kisiasa. Hana muda na Wizara ya Nishati, muda mwingi anatumia kujitangaza mikoani na ameanza kupoteza mvuto jukwaani

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,118
Waziri Biteko ni kama ameshindwa kuelewa waliomteua wanataka nini kwake.

Je, wanataka umeme au wanataka azunguke kufanya siasa za uchaguzi? Amekimbizana na majukwaa mfululizo toka alipoteuliwa hadi sasa

Vision yake kwenye wizara imemezwa na malengo ya kisiasa yaliyo mbele yake kuliko malengo ya kitaaluma yanayohitajika Wizara ya Nishati kwa sasa.

Hii yote ni kukosekana kwa critical thinkers na political analysist kwenye cycle binafsi ya wanasiasa wa Tanzania. Wao ndio wanaweza, wanapanga na kutekeleza.

Duniani kazi ya kuwaza na kupanga mikakati wanafanya wengine na mwanasiasa anabaki na utekelezaji wa kilichochakatwa.

Dotto rudi ofisini kama wiki tatu hivi mfululizo usome majalada utabaini jukumu walilokupa linaweza kuwa liability kwako siku za mbeleni
 
Ninakubaliana nawe kwenye mada yako; lakini nimeona nilinyanyue hili hapa ambalo pengine hujalitafakari vizuri.
Hao 'Critical Thinkers' na 'Analysts' unaozungumzia wewe, kwani huwaoni hata humu akina Faiza Fox; akina Lucas, Choice..., n.k.
Hao chawa walioenea kila sehemu huoni kazi zao.

Kama huoni hivyo wewe, basi ujue wenzio hao ndio wanaokidhi mahitaji yao. Standard zako, siyo zao.
 
Huo mvuto anaopoteza aliwahi kuwa nao lini ? Huyu hajawahi kuwa na mvuto popote
Na kwa kweli hata sijui madhumuni ya kumteua katika huo "unaibu"; tena mtu anayepewa wizara yenye matatizo makubwa sana; hapo lengo la uteuzi kwa kweli linatatiza.

Lakini haishangazi, ukikumbuka historia ya teuzi zinazofanywa na utawala huu zisizokuwa na lengo maalum.
 
Waziri Biteko ni kama ameshindwa kuelewa waliomteua wanataka nini kwake.

Je, wanataka umeme au wanataka azunguke kufanya siasa za uchaguzi? Amekimbizana na majukwaa mfululizo toka alipoteuliwa hadi sasa

Vision yake kwenye wizara imemezwa na malengo ya kisiasa yaliyo mbele yake kuliko malengo ya kitaaluma yanayohitajika Wizara ya Nishati kwa sasa.

Hii yote ni kukosekana kwa critical thinkers na political analysist kwenye cycle binafsi ya wanasiasa wa Tanzania. Wao ndio wanaweza, wanapanga na kutekeleza.

Duniani kazi ya kuwaza na kupanga mikakati wanafanya wengine na mwanasiasa anabaki na utekelezaji wa kilichochakatwa.

Dotto rudi ofisini kama wiki tatu hivi mfululizo usome majalada utabaini jukumu walilokupa linaweza kuwa liability kwako siku za mbeleni
Umeongea pointi sana
 
Vyeo viwili kwa wakati mmoja kwa Biteko ndio changamoto. Ana mambo ya kiserikali na mambo ya wizara.

Mara nyingi anatumwa kwenda kufanya hiyo kazi na waziri Mkuu ama rais mwenyewe.

Matatizo ya wizara ya nishati yanajulikana na suluhisho lake linajulikana, Biteko hata awepo ofisini hakuna atakachobadilisha.

Kwa sasa wizara, TANESCO na nchi kwa ujumla matumaini yao ni Bwawa la Mwalimu Nyerere kuwashwa mwaka kesho ili umeme uwake, hakuna mbadala mwingine wowote ulioko hapa karibu wa kutatua changamoto ya umeme, hakuna.

Walioharibu ni kina Makamba na maharage, wamekaa pale miaka 2 mizima hakuna cha maana walichokifanya, wakashindwa hata kuanzisha mradi mmoja wa umeme wa solar ama upepo ambao ungeweza kukamilika ndani ya miezi 18 hadi 24. Wao wakakalia wizi, media coverage na publicity tu.
 
Waziri Biteko ni kama ameshindwa kuelewa waliomteua wanataka nini kwake.

Je, wanataka umeme au wanataka azunguke kufanya siasa za uchaguzi? Amekimbizana na majukwaa mfululizo toka alipoteuliwa hadi sasa

Vision yake kwenye wizara imemezwa na malengo ya kisiasa yaliyo mbele yake kuliko malengo ya kitaaluma yanayohitajika Wizara ya Nishati kwa sasa.

Hii yote ni kukosekana kwa critical thinkers na political analysist kwenye cycle binafsi ya wanasiasa wa Tanzania. Wao ndio wanaweza, wanapanga na kutekeleza.

Duniani kazi ya kuwaza na kupanga mikakati wanafanya wengine na mwanasiasa anabaki na utekelezaji wa kilichochakatwa.

Dotto rudi ofisini kama wiki tatu hivi mfululizo usome majalada utabaini jukumu walilokupa linaweza kuwa liability kwako siku za mbeleni
Umeme kishawapa Tanesco miezi 6. Unataka akae hapohapo anangojea mpaka lini?

Kumbuka huyo ni Naibu Waziri Mkuu pia.
 
Waziri Biteko ni kama ameshindwa kuelewa waliomteua wanataka nini kwake.

Je, wanataka umeme au wanataka azunguke kufanya siasa za uchaguzi? Amekimbizana na majukwaa mfululizo toka alipoteuliwa hadi sasa

Vision yake kwenye wizara imemezwa na malengo ya kisiasa yaliyo mbele yake kuliko malengo ya kitaaluma yanayohitajika Wizara ya Nishati kwa sasa.

Hii yote ni kukosekana kwa critical thinkers na political analysist kwenye cycle binafsi ya wanasiasa wa Tanzania. Wao ndio wanaweza, wanapanga na kutekeleza.

Duniani kazi ya kuwaza na kupanga mikakati wanafanya wengine na mwanasiasa anabaki na utekelezaji wa kilichochakatwa.

Dotto rudi ofisini kama wiki tatu hivi mfululizo usome majalada utabaini jukumu walilokupa linaweza kuwa liability kwako siku za mbeleni
Ukiwa Kiongozi na ukitaka kufurahisha watu dizaini ya mtoa mada utapata shida sana.

Ndio maana Samia hanaga huo ujinga na wapambe ndio wanafanya.Tabia za kutaka kufurahisha binadamu na kulazimisha wakukubali alikuwanazo Mwendazake ndio maana propaganda na maigizo yalikuwa mengi sana.

Samia ndio role model wangu sio kwenye siasa hata mtaani,Sina mda wa kulazimisha wanipende sijui kufurahisha binadamu.

So wanaotaka kumpendeza binadamu Wana shida sana na in most cases watawahi kufa sababu ya stress za kujitafutia na kutojikubali na kukubali Hali halisi.

Mwisho mtoa mada usilazimishe unachokitaka wewe Kwa Biteko ndio iwe na yeye anakitaka ila kama nae analazimisha kuiubalika basi atapata tabu sana.
 
Kwa hiyo hakuna haja ya kuwa na Waziri?

Biteko anahangaika na cheo bandia badala ya kushughulikia tatizo la umeme.
Acha wivu Mzee.Kwa nafasi yake waliyompa analazimika sio tuu kuisemea Nishati Bali kushughulika na masuala General ya Serikali kama anavyofanya PM na Yuko sahihi.

Naibu Waziri wa Nishati technically ndio ana play role kubwa ya Waziri wa Nishati kulingana na status ya boss wake.

Foreign secretary wa England ni Deputy Prime Minister pia so nae anakuwa na general role ukiacha kazi ya kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Na ndio maana juzi amemuwakikisha Rais Nje ya Nchi na akapata heshima za kiplitokali safi kabisa huko Uganda Kwa sababu ya kwamba ni Mwakilishi wa Rais lakini ni Deputy PM.

Angekuwa Waziri wa kawaida asingepata zile heshima hata kama katumwa na Rais ,Iko hivyo yaani.
 
Waziri Biteko ni kama ameshindwa kuelewa waliomteua wanataka nini kwake.

Je, wanataka umeme au wanataka azunguke kufanya siasa za uchaguzi? Amekimbizana na majukwaa mfululizo toka alipoteuliwa hadi sasa

Vision yake kwenye wizara imemezwa na malengo ya kisiasa yaliyo mbele yake kuliko malengo ya kitaaluma yanayohitajika Wizara ya Nishati kwa sasa.

Hii yote ni kukosekana kwa critical thinkers na political analysist kwenye cycle binafsi ya wanasiasa wa Tanzania. Wao ndio wanaweza, wanapanga na kutekeleza.

Duniani kazi ya kuwaza na kupanga mikakati wanafanya wengine na mwanasiasa anabaki na utekelezaji wa kilichochakatwa.

Dotto rudi ofisini kama wiki tatu hivi mfululizo usome majalada utabaini jukumu walilokupa linaweza kuwa liability kwako siku za mbeleni
Wahuni siyo watu wazuri,juzi kwani hujamsikia JK akimsifu Biteko kuwa uteuzi wake ni sahihi kabisa.Hao ndiyo ukute walimshauri Bi.Mchele baada ya kuona mtu wao January katolewa basi wakasema umpe Dotto na cheo cha Naibu Waziri Mkuu.Hapo sasa ndiyo Wahuni wanacheza na gepu,anaandaliwa ziara za kisiasa kama zote na anasahau jukumu la Uwaziri wa Nishati.
Ni kama Samia tu anavyoandaliwa shughuli,akitoka huku anaenda huku ili Wahuni wafanye yao!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Ninakubaliana nawe kwenye mada yako; lakini nimeona nilinyanyue hili hapa ambalo pengine hujalitafakari vizuri.
Hao 'Critical Thinkers' na 'Analysts' unaozungumzia wewe, kwani huwaoni hata humu akina Faiza Fox; akina Lucas, Choice..., n.k.
Hao chawa walioenea kila sehemu huoni kazi zao.

Kama huoni hivyo wewe, basi ujue wenzio hao ndio wanaokidhi mahitaji yao. Standard zako, siyo zao.
Wewe jamaa!

Back
Top Bottom