Waziri Bashe na Wabunge wote wa Mkoa wa Kagera hiki kilio cha Wakulima wa Vanilla kiko mikononi mwenu

No overtaking

Member
Dec 14, 2013
40
78
Hapa sina cha kuongeza Video inajieleza yenyewe. Nimetaja Kagera tu sababu ndiyo sehemu video ilipochukuliwa tangu mwezi wa tano na mpaka sasa hakuna lolote lililofanyika.

Kila mara inasemwa kwamba wakulima katika Mkoa wa Kagera wana nafasi kubwa sana ya kuuza mazao yao nchini Uganda ambapo wanapata bei nzuri sana kuliko hapa kwetu lakini wanapigwa pini.

Waziri Bashe hili linakuhusu. Serikali iliweka wazi kwamba Mkoa huo utafanyika kuwa sehemu ya kimkakati katika uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Hivi hii ya kufungua msimu wa kununua Vanilla mwezi wa Saba wakati Vanilla inakauka shambani ndiyo hamasa??? Ni mkulima gani wa Kagera au sehemu yoyote nchini atahamasika kuweka nguvu zake katika uzalishaji usiompa faida?


 
Back
Top Bottom