Waziri awatolea uvivu wafanyakazi KIA

Mallaba

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
2,554
47
Mussa Juma, Arusha

SERIKALI imeutaka uongozi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro International Airpot (Kia) kurekebisha mfumo wake wa utendaji kazi ili kuvutia , abiria na ndege kutumia uwanja huo.

Waziri wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Deodorasi Kamala, alitoa wito huo wakati akizungumza na uongozi wa Uwanja huo kujadili changamoto mbalimbali zikiwemo zinazochangia wasafiri wengi kukwepa kutumia uwanja huo .

Dk Kamala alisema, kwa muda mrefu sasa kumekuwa na malalamiko juu ya urasimu na huduma zinazotolewa katika uwanja huo jambo linalosababisha wasafiri wengi wanaoingia na kutoka nchini kukwepa kutumia uwanja huo na kukimbilia viwanja vingine.

Alisema baada ya kupata malalamiko hayo, alifuatilia na kubaini ukweli wa baadhi ya mambo yanayofanywa katika uwanja huo na hivyo kuwakwaza abiria na mashirika ya ndege.

Waziri Kamara alisema, miongoni mwa mambo yanayolalamikiwa ni pamoja na usumbufu usio wa lazima kwa abiria na wasafirishaji na viwango vikubwa vya adhabu wanavyotozwa kama vile kutokuwa na chanjo ya homa ya manjano ambapo wamekuwa wakitozwa faini ya dola za kimarekani kati ya 30 na 50 jambo ambalo halifanyiki katika viwanja vingine .
“ Unakuta nchi haina taarifa ya kuwa na ugonjwa huo, lakini mnalazimisha chanjo, japo kuwa suala hili la kisheria, lakini katika utekelezaji wake zinahitajika busara na pia uzalendo ukiwemo wa kumfanya mgeni aone umuhimu wa kurudi Tanzania alisema Kamala .

Alisema, jingine linalalamikiwa ni pamoja na baadhi ya watendaji kushirikiana na baadhi ya kampuni ya utalii katika kuhujumu mapato ya nchi kwa kutoa Visa kwa njia za panya jambo ambalo ni kinyume cha sheria na pia linatoa picha mbaya kwa wageni .

“Tunajua kuwa kuna hako kamchezo katika uwanja huu, ninaomba muache, wageni wenyewe wanatuambia na tofauti na mnavyofikiri wenzetu wenye uzalendo wa nchi zao wakiona hivi vitu vya mkato mkato ...kamchezo hako waache kabla hatua hazijachukuliwa” alisema Dk Kamala.

Aidha alimwagiza Mkurugenzi mtendaji wa Uwanja huo kuchunguza na kukomesha tabia hiyo kwani pamoja na kuhujumu uchumi wa nchi inazorotesha jitihada za Watanzania za kuingia katika ushindani wa soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aliwataka watumishi wote wa Uwanja huo kutambua kuwa kiwanja cha ndege hicho ni Kioo cha nchi hivyo ni jukumu la kila mfanyakazi kufanyakazi kwa uadilifu na kutoa huduma bora.

Kwa upande wao baadhi ya watumishi wa uwanja huo akiwemo Mkurugenzi Mkuu, Van De Kreeke na Meneja mwendeshaji ,Japhet Urio pamoja na kukiri kuwepo kwa baadhi ya changamoto walisema asilimia kubwa ya mambo yanayolalamikiwa yako nje ya uwezo wao .



Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ni ya viwanja vinavyotoza gharama kubwa kwa ndege zinazotua hali ambayo imesababisha ndege chache kutua tofauti na viwanja vya ndege vingine.


source:mwananchi


Hongera Dk Deodorasi Kamala lakini mbona hii ni mero ya mda mrefu sana?mlikuwa wapi kila siku?
Ni kweli uwanja wa KIA upo na umekuwa ni kama hasara kwa nchi yetu,sijui upo kwa ajili ya manufaa ya akina nani, maana sio siri ni uwanja unaoogopeka kwa kila mtu si nje wal andani ya nchi,
baadhi ya amtatatizo yanayohitaji kubadilishwa ni:
1.Kupunguza landing and taking-off fees so that can attract more flights
2.cancel or reduce unnecessary fees kama hizo za homa ya manjano,mtu anatoka nchi yake amabayo haina then unamwambia eti alipie ,je hizo pesa zinakwenda wapi? si ndo ufisadi huu maradufu
3.Be attractive and carring for visitors and tourist,
4.Be competitiveness with other International Airports so that can attract more flights
5.leo tunaona ndege nyingi zinauogopa sana huu uwanja kwanini?
6 .Kenya wameamua kujenga uwanja mwingine tena mpakani na moshi,je sio kwamba KIA ndo itakufa kabisa,
 
Tuna rasilimali nyingi sana mpaka tunashindwa jinsi ya kuzitumia, mwisho tunajimaskinisha kwa ujinga wetu huu
 
.wakati waziri anasema alichunguza na kubaini mapungufu yanayolalamikiwa, lakini mwishoni anaagiza, uongozi wa uwanja wafanye uchunguzi tena. kwanini asichukue hatua? Inanishangaza hapo ati, haamini aliyoyaona?

:mmph:
 
Hapo ndio ujue jinsi ganai viongozi wetu wasivyojua kuwajibika,hawajua majukumu yao nini bali kila siku utawasikia wakisema mchakato mchakato wala huwa haiishi,Waziri umeshaona tatizo liko wapi baada ya kutoa himimisho hapohapo bado eti unaomba wafanye uchunguzi,yaani ni uchunguzi ndani ya uchunguzi..kazi kwelikweli:A S-rose:


.wakati waziri anasema alichunguza na kubaini mapungufu yanayolalamikiwa, lakini mwishoni anaagiza, uongozi wa uwanja wafanye uchunguzi tena. kwanini asichukue hatua? Inanishangaza hapo ati, haamini aliyoyaona?

:mmph:
 
Anajifanya kusema baada ya kujua hana ubunge, hana uwaziri halafu hana phd so anajifanya leo kaona, hana lolote la kufanya ni ziara ya kuaga tu anakusanya allowance za mwisho. kama alikuwa yuko serious angesema wakati huo
 
Back
Top Bottom