Waziri Ataka Zanzibar iwe Dola Huru, Irudishiwe kiti chaker UN

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1]
mansoor-yussuf-himid1.jpg
Waziri asiye na Wizara Maalum Mh Mansour Yussuf Himid

Written by Ashakh (Kiongozi) // 18/07/2012 // Habari // No comments[/h]
Waziri asiye na Wizara Maalumu katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mansour Yussuf Himid ametaka Zanzibar iwe Dola huru iliyokamilika na iwe na kiti chake Umoja wa Mataifa (UN) na kutambuliwa na taasisi za kimataifa.
Waziri huyo ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM na Katibu wa Idara ya Fedha ya Chama hicho Zanzibar, pia amepinga msimamo wa chama hicho tawala kuwa na Muungano wa Serikali mbili na kuudhihaki kuwa hauna manufaa wala tija kwa Wazanzibari.
Mansour alisema hayo jana wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria katika kikao cha bajeti cha wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2012/13.
“Wananchi wetu wawe huru katika kutoa maoni ya mchakato wa Katiba…kama watu hawataki Muungano waseme, ikiwamo wanaotaka Muungano wa mkataba akina sisi … mfumo huu wa Serikali mbili kwangu mimi sebuu,” alisema Mansour akimaanisha anaukataa moja kwa moja.
Alisisitiza kuwa Muungano wa Serikali mbili kwa sasa hauna nafasi tena na hauwezi kuisaidia Zanzibar kwenda mbele na kupiga hatua kubwa ya kiuchumi kutokana na Zanzibar kukosa sifa ya kuwa Dola yenye kumiliki uchumi wake.
Alitoa mfano wa maeneo huru ya uchumi ambayo yalitangazwa na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk Salmin Amour mwaka 1992 Fumba yakiwa na eneo la hekta 900 za msitu zilizotengwa, lakini yameshindwa kuendelezwa na kubaki msitu wanaoishi wanyama aina ya komba na ngedere.
“Tusidanganyane hakuna mwekezaji anayeweza kuja kuwekeza katika maeneo huru ya uchumi yaliyo Fumba kwa sababu Zanzibar haina uwezo wa kuhimili uchumi wake na ndiyo maana maeneo hayo yamekuwa msitu wa kuishi komba na ngedere,” alisema Mansour. Hakuna wa kumtisha.
Alisema zama za kutishana zimepitwa na wakati na kufafanua kuwa kutofautiana katika mawazo isiwe chanzo cha kutukanana na kudharauliana na kusingiziana kiasi watu wengine kuonekana wahalifu wakifananishwa na wafuasi wa vyama vya kisiasa vilivyopita ikiwamo Hizbu na Jumuiya ya Mihadhara ya Kidini ya Uamsho.
Alitoa mfano wa viongozi walioongoza kwa vitisho na nguvu za kijeshi, kwamba kwa sasa hawapo tena madarakani kutokana na wananchi kuwapinga na kuwakataa moja kwa moja wakiwamo marais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak na wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.

Chanzo: Habari Leo
 
kama kweli wewe HUTISHWI basi ninakuomba haya maneno ukayasema mbele ya NEC ya CCM Dodoma.

Mnabwabwaka tu mkiwa Zenji mkija bara mnaufyata. BTW Rais wako Dr. Shein ameshasema ataurinda Muungano kwa gharama yeyote. Sasa kama unapingana na Rais wako si jiondoe kwenye baraza la mapinduzi.
 
Ni kweli mheshimiwa tumechoka kuwa chini ya hawa wabara, hatuwezi kujiamulia mambo yetu weneyewe mpaka tukaombe Dodoma, hapa hatukubali katuu!!
 
Huyu waziri anahusika na wizi.......

Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayochunguza ubadhirifu wa mali za Serikali ya Zanzibar imeitaka serikali kurejesha kiwanja alichopewa kinyume na sheria, mke wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume.Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi kiwanja hicho namba 186 chenye mita za mraba 750 kipo katika mtaa wa Kinazini, mkabla na Jemgo la historia la Dk. David Livingstone, mjini Unguja.Ripoti imeeleza kwamba kiwanja hicho kilikuwa kikimilikiwa na Wizara ya Kilimo na Maliasili kabla ya kupewa Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) kujenga makao makuu yake. Uchunguzi wa kamati umebaini kuwa ZRB baada ya kupewa uwanja huo walishindwa kuuendeleza baada ya kupata uwanja mwingine katika eneo la Mazizini na kujenga makao makuu yake na uwanja ulirejeshwa Wizara ya Ardhi.

Ripoti imesema Wizara ya Kilimo ilitoa kiwanja hicho kwa ZRB kupitia barua ya Agosti 28, 2002 yenye kumbukumbu WKMMU/29/5/41/72 kwenda Wizara ya Ardhi ya kuwapa ZRB. Uamuzi wa Wizara ya Kilimo na Maliasili ulikubaliwa na Wizara ya Ardhi na kukabidhi uwanja kwa ZRB Septemba 9, 2002 kupitia barua yenye kumbukumbu namba MUNA/34/14/378/ VOl.1 na kutoa shahada ya haki ya matumizi ya ardhi ya Aprili 4, 2003.
Hata hivyo, ripoti imesema baada ya ZRB kupata sehemu nyingine ya kuendelea na ujenzi waliamua kukirejesha kiwanja hicho serikalini ambapo aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Makazi,Maji na Nishati, Mansour Yussuf Himid, aliamua kiwanja hicho kumpatia mama yake Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, mwaka 2010.

Akihojiwa na kamati hiyo Desemba 7, mwaka jana, Waziri Mansour, ambaye sasa ni Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum alikiri kiwanja hicho kumpa mama Fatma Karume baada ya kumuomba ili aweze kukitumia kwa shughuli zake za biashara ambazo hazijaelezwa.
Ripoti imeeleza kwamba baada ya mama Fatma kupewa uwanja huo ndani ya mwezi mmoja aliuuza kwa Kampuni ya F & K Enterprises Limited, ambapo anamiliki na hisa.Uchunguzi umebaini kuwa baada ya mama Fatma na wenzake kupitia kampuni hiyo kukabidhiwa uwanja huo waliuuza kwa Sh. milioni 150 kwa mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar, Ali Shahib Khamis, na Waziri kumpatia hati miliki namba L.O.NO Z-53/S.178/2010/186 na R.O.NO Z-150/2010 ikiwa ni shahada ya matumizi ya ardhi iliyotolewa kwa mujibu wa sheria namba 12 ya ya ardhi ya mwaka 1992.

Akihojiwa na kamati juu ya kuuza ardhi hiyo ndani ya mwezi mmoja tangu kupewa mama Fatma, Mansour alisema hii ilitokana na kampuni yao kushindwa kufikia malengo waliojiwekea na hivyo kumua kukiuza kiwanja.Kamati imesema haikuridhishwa na utaratibu wa kisheria uliotumika kutoa kiwanja cha serikali baada ya mama Fatma Karume na wenzake kushindwa kuwasilisha nyaraka za kuthibitisha maombi yao kwa wizara kabla ya kutolewa kiwanja hicho."Mpaka tunatoa taarifa hii hakuna ushahidi wowote ambao mama Fatma aliuwasilisha pamoja na kuahidi angefanya hivyo kama alivyotakiwa kufanyaharaka iwezekanovyo," ripoti imesisistiza. Ripoti imeeleza kwamba kamati ilichukua hatua mbali mbali za kufuatilia suala hilo ikiwa pamoja na kuwahoji watendaji wakuu wa wizara, lakini imeshindwa kupata ushahidi wa maombi ya barua ya mama Fatma Karume au kampuni hiyo."Kamati kwa kauli moja inathibitisha kwamba hakuna ushahidi wa kuombwa kiwanja hicho na hivyo, ina wasiwasi waziri ametumia vibaya madarakan yake, ameamua kukimilikisha kiwanja cha serikali kwa mtu bila ya maombi yoyote kinyume na taratibu na sheria," ripoti inasema.

Hata hivyo, kamati imesema baada ya Waziri Mansour kuhojiwa juu ya kukosekana kwa maombi ya wahusika, alisema yalikuwepo maombi ya kampuni ya F&K Enterpreses LTD katika faili maalum na alishangazwa na taarifa za kutoweka kwa nyaraka hizo.

SOURCE: NIPASHE

Yote kwa yote lakini kukosea haimuzui kutoa maoni yake kuhusu muungano, mbona kabla hajasema hukuleta hizi kashfa? au unatunyamazisha ili content ya ujumbe wake iwe ni kujadili comment zako? tunataka Zanzibar iliyo huru hata kama nani kaiba nini!!! kwanza bara kwa ufusadi usiseme afadhali huku Zanzibar.
 
Sasa weye mbona unataka kunizuia mimi nisitowe mawazo yangu juu yake? Taarifa hii nilirejea tena juzi wakati Mama mkubwa kabisa alipotaka kutudanganya kuwa haangaliwi na serikali.
 
Sisi ambao tumekuwa tunalilia Tanganyika lakini bila kuwa na uthubutu za kuidai (tungeitwa na kushitakiwa kama wahaini) hatuna budi tuwaunge mkono hawa akina AL UAMSHO. Jitihada wanazofanya zikifanikiwa ni mavuno kwetu - we'll have our beloved Tanganyika back! Ninakuunga mkono kwa asilimia mia Mhe Waziri.
 
mansoor-yussuf-himid1.jpg
Waziri asiye na Wizara Maalum Mh Mansour Yussuf Himid

Written by Ashakh (Kiongozi) // 18/07/2012 // Habari // No comments

Waziri asiye na Wizara Maalumu katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mansour Yussuf Himid ametaka Zanzibar iwe Dola huru iliyokamilika na iwe na kiti chake Umoja wa Mataifa (UN) na kutambuliwa na taasisi za kimataifa.
Waziri huyo ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM na Katibu wa Idara ya Fedha ya Chama hicho Zanzibar, pia amepinga msimamo wa chama hicho tawala kuwa na Muungano wa Serikali mbili na kuudhihaki kuwa hauna manufaa wala tija kwa Wazanzibari.
Mansour alisema hayo jana wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria katika kikao cha bajeti cha wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2012/13.
"Wananchi wetu wawe huru katika kutoa maoni ya mchakato wa Katiba…kama watu hawataki Muungano waseme, ikiwamo wanaotaka Muungano wa mkataba akina sisi … mfumo huu wa Serikali mbili kwangu mimi sebuu," alisema Mansour akimaanisha anaukataa moja kwa moja.
Alisisitiza kuwa Muungano wa Serikali mbili kwa sasa hauna nafasi tena na hauwezi kuisaidia Zanzibar kwenda mbele na kupiga hatua kubwa ya kiuchumi kutokana na Zanzibar kukosa sifa ya kuwa Dola yenye kumiliki uchumi wake.
Alitoa mfano wa maeneo huru ya uchumi ambayo yalitangazwa na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk Salmin Amour mwaka 1992 Fumba yakiwa na eneo la hekta 900 za msitu zilizotengwa, lakini yameshindwa kuendelezwa na kubaki msitu wanaoishi wanyama aina ya komba na ngedere.
"Tusidanganyane hakuna mwekezaji anayeweza kuja kuwekeza katika maeneo huru ya uchumi yaliyo Fumba kwa sababu Zanzibar haina uwezo wa kuhimili uchumi wake na ndiyo maana maeneo hayo yamekuwa msitu wa kuishi komba na ngedere," alisema Mansour. Hakuna wa kumtisha.
Alisema zama za kutishana zimepitwa na wakati na kufafanua kuwa kutofautiana katika mawazo isiwe chanzo cha kutukanana na kudharauliana na kusingiziana kiasi watu wengine kuonekana wahalifu wakifananishwa na wafuasi wa vyama vya kisiasa vilivyopita ikiwamo Hizbu na Jumuiya ya Mihadhara ya Kidini ya Uamsho.
Alitoa mfano wa viongozi walioongoza kwa vitisho na nguvu za kijeshi, kwamba kwa sasa hawapo tena madarakani kutokana na wananchi kuwapinga na kuwakataa moja kwa moja wakiwamo marais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak na wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.

Chanzo: Habari Leo

Tatizo la ndugu zangu wazanzibar ni kutofikiri kwa kina. Wapiga kelele wengi wa Zanzibar hasa waasisi wa hoja za kuashiria kuvunja muungano wengi wao ni mafisadi ambao wanaona njia pekee ya kufisidi hicho kisiwa ni Zanzibar kuwa dola huru.

Kwa mtu kama Jussa haiwezekani ikawa hajui madhara kuvunja muungano kwa upande wa Zanzibar yet ndio yuko mstari wa mbele kulilia muungano uvunjike. Hawa wote ni mafisadi tu, Maalimu Seif alipiga kelele wakati wa kampeni mpaka akawaahidi wazanzibar kuwa atawaletea pasipoti za Zanzibar, leo yuko wap?? Amepata alichotaka katulia tuli kama hayupo, anakula bata. Ile amepata tu umakamu wa rais akaenda nje ya nchi kwa wiki 7 mfululizo, kitu ambacho hata Vasco da Gama mwenyewe, JK, hajawahi kufanya.

Hawa wakina Mansour ni walewale tu, hawana jipya. So, wabara tudai taifa moja-nchi moja, hawataki wale kona. Wataletewa tende za bure na waarabu
 
Unajua hawa viongozi wengine wanachekesha sana..
Sasa unataka Zanzibar iwe huru kwa nini usifanye wewe referendum hadi unasubiri maoni ya kuundwa kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano.. Kwa nini viongozi wa Zanzibar wanashindwa au wanaogopa kuingia gharama za kukusanya maoni ya Wazanzibar kuhusiana na mustakabali wa nchi yao? maana kama hawataki huu muungano, wanaitaka Zanzibar huru basi bila shaka maamuzi ya maana ni kukataa kushiriki ktk kuchangia maoni ya katiba mpya ya Jamhuri..
 
Huyu jamaa kwa kweli ni ajabu, sasa yeye ni waziri na mjumbe wa nec, bado anamlalamikia nani? badala ya wananchi kumlalamikia yeye kama kiongozi wao wa kutekeleza hicho anachohubiri lakini na yeye bado analalamika, ana mlalamikia nani?

Hivi rais na baraza lake wakitamka kuanzia leo zanzibar ni nchi kamili, hivi nani atawapelekea majeshi kuwakamata mawaziri,rais na wana baraza? na kama kweli wakitamka hivyo na wakapelekewa jeshi basi kila mtu na hata umoja wa mataifa utatambua kumbe ni kweli zanzibar ni koloni la tanganyika.
 
Unajua hawa viongozi wengine wanachekesha sana..
Sasa unataka Zanzibar iwe huru kwa nini usifanye wewe referendum hadi unasubiri maoni ya kuundwa kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano.. Kwa nini viongozi wa Zanzibar wanashindwa au wanaogopa kuingia gharama za kukusanya maoni ya Wazanzibar kuhusiana na mustakabali wa nchi yao? maana kama hawataki huu muungano, wanaitaka Zanzibar huru basi bila shaka maamuzi ya maana ni kukataa kushiriki ktk kuchangia maoni ya katiba mpya ya Jamhuri..
afadhal uneongea tena kwann muendelee kutoa maoni kwenye katiba ya tZ na nyinyi hamutaki muungano???waznZ tuna akili gani mbona hatueleweki
 
Unajua hawa viongozi wengine wanachekesha sana..
Sasa unataka Zanzibar iwe huru kwa nini usifanye wewe referendum hadi unasubiri maoni ya kuundwa kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano.. Kwa nini viongozi wa Zanzibar wanashindwa au wanaogopa kuingia gharama za kukusanya maoni ya Wazanzibar kuhusiana na mustakabali wa nchi yao? maana kama hawataki huu muungano, wanaitaka Zanzibar huru basi bila shaka maamuzi ya maana ni kukataa kushiriki ktk kuchangia maoni ya katiba mpya ya Jamhuri..

Mkandara,

..asante kwa kuliona hilo.

..Mansor anadai maoni ya wa-Zanzibar "wote" yasikilizwe. sasa hapo ulitegemea kwamba mfumo mzuri wa kusikiliza maoni ya wa-Zanzibar wote ni kuitisha kura ya maoni.

..sasa hebu soma hiki kipande nilichoambatanisha ambapo Mansour Yussuf Himid anaonyesha kuogopa na kupinga kupigwa kwa kura ya maoni kuamua future ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

..kwa kweli sielewi wanachokitaka wa-Zanzibari ni kitu gani. Kwa mfano wanasema wanataka "muungano wa mkataba", bila kufafanua na kueleza mkataba huo utahusisha masuala yepi. Pia hata muungano huu tulionao sasa hivi Mwalimu Nyerere na Sheikh Abeid Karume walisaini mkataba.

Mansour Himid said:
Tuangalie ugumu wa kura ya maoni katika mifano ifuatayo: kwanza, katika daftari la wapiga kura, wanaostahili kupiga kura ya maoni ni watu wasiozidi laki sita kwa Zanzibar yote. Takwimu kutoka Bara zinaonyesha kwamba Dar es Salaam peke yake kuna Wazanzibari 350,000. Je, Tanzania nzima?

Dhana kubwa inayowahofisha viongozi wa serikali juu ya kura ya maoni ni kwamba jee ikiwa 30% ya Wazanzibari wanaoishi Zanzibar wataukubali muungano wa sasa au wa serikali moja wakiungwa mkono na Wazanzibari laki tatu na nusu kutoka Bara, kweli kutakuwa na Zanzibar huru? Au kukiwa na matokeo ya kati na kati bila ya majibu sahihi itakuwaje?

Tukumbuke kwamba asilimia karibu 40 ya Wazanzibari waliyapinga Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya 2010. Sasa ikiwa watajumuika na Wazanzibari waishio Bara itakuwaje?

..habari nzima kuhusu mahojiano ya Mansour Himid yapo ktk link hii hapa:

Muungano wa mkataba ndio dira yetu | Zanzibar Daima

NB:

..kitu cha ajabu ni kwamba wabunge wa kutoka Zanzibar walioko ktk bunge la muungano hawatoi matamshi kama haya yanayotolewa na Mansour Himid na Ismail Jussa. Kuna kipindi Ismail Jussa alikuwa ni mbunge ktk bunge la muungano na hakusikika akitoa tamko lolote lile kupinga muungano.
 
Mkandara,

..asante kwa kuliona hilo.

..Mansor anadai maoni ya wa-Zanzibar "wote" yasikilizwe. sasa hapo ulitegemea kwamba mfumo mzuri wa kusikiliza maoni ya wa-Zanzibar wote ni kuitisha kura ya maoni.

..sasa hebu soma hiki kipande nilichoambatanisha ambapo Mansour Yussuf Himid anaonyesha kuogopa na kupinga kupigwa kwa kura ya maoni kuamua future ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

..kwa kweli sielewi wanachokitaka wa-Zanzibari ni kitu gani. Kwa mfano wanasema wanataka "muungano wa mkataba", bila kufafanua na kueleza mkataba huo utahusisha masuala yepi. Pia hata muungano huu tulionao sasa hivi Mwalimu Nyerere na Sheikh Abeid Karume walisaini mkataba.

..habari nzima kuhusu mahojiano ya Mansour Himid yapo ktk link hii hapa:

Muungano wa mkataba ndio dira yetu | Zanzibar Daima

NB:

..kitu cha ajabu ni kwamba wabunge wa kutoka Zanzibar walioko ktk bunge la muungano hawatoi matamshi kama haya yanayotolewa na Mansour Himid na Ismail Jussa. Kuna kipindi Ismail Jussa alikuwa ni mbunge ktk bunge la muungano na hakusikika akitoa tamko lolote lile kupinga muungano.
Yale yale alosema Nyerere kwamba kuna Wazanzibar na Wazanzibara hii inahitimisha kwamba kumbe hata wao wamegawanyika..Je, ina maana hawa Wazanzibara sii Wazanzibar na nchi hiyo sii yao?
 
Mansouri anabwabwata kama walivyo wale kama yeye wa kupenda wanaume wenzake, yeye mawaziri wenzake ndio wake zake. Sasa hewa ndio imewazidi wanataka nafasi ya kupumulia? Mbona kauli mbiu yenyewe ni ya kishog?
 
Tatizo la ndugu zangu wazanzibar ni kutofikiri kwa kina. Wapiga kelele wengi wa Zanzibar hasa waasisi wa hoja za kuashiria kuvunja muungano wengi wao ni mafisadi ambao wanaona njia pekee ya kufisidi hicho kisiwa ni Zanzibar kuwa dola huru.

Kwa mtu kama Jussa haiwezekani ikawa hajui madhara kuvunja muungano kwa upande wa Zanzibar yet ndio yuko mstari wa mbele kulilia muungano uvunjike. Hawa wote ni mafisadi tu, Maalimu Seif alipiga kelele wakati wa kampeni mpaka akawaahidi wazanzibar kuwa atawaletea pasipoti za Zanzibar, leo yuko wap?? Amepata alichotaka katulia tuli kama hayupo, anakula bata. Ile amepata tu umakamu wa rais akaenda nje ya nchi kwa wiki 7 mfululizo, kitu ambacho hata Vasco da Gama mwenyewe, JK, hajawahi kufanya.

Hawa wakina Mansour ni walewale tu, hawana jipya. So, wabara tudai taifa moja-nchi moja, hawataki wale kona. Wataletewa tende za bure na waarabu
we acha maneno mengi hivi wewe una faida gani na muungano tueleze ndo upingane na huyu jamaa anayetaka Zanzbr huru,mi si mzanzibarilakini sioni faida ya muungano waloungamuungano walikufa na muungano wao ,ZANZBR ni nchi yenye Rais wake na kila kitu bendera yake bendera ni alama ya ya nchi huru sasa uataka tu kuwakaba wa Zanzibar waachwe huru
 
mansoor-yussuf-himid1.jpg
Waziri asiye na Wizara Maalum Mh Mansour Yussuf Himid

Written by Ashakh (Kiongozi) // 18/07/2012 // Habari // No comments

Waziri asiye na Wizara Maalumu katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mansour Yussuf Himid ametaka Zanzibar iwe Dola huru iliyokamilika na iwe na kiti chake Umoja wa Mataifa (UN) na kutambuliwa na taasisi za kimataifa.
Waziri huyo ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM na Katibu wa Idara ya Fedha ya Chama hicho Zanzibar, pia amepinga msimamo wa chama hicho tawala kuwa na Muungano wa Serikali mbili na kuudhihaki kuwa hauna manufaa wala tija kwa Wazanzibari.
Mansour alisema hayo jana wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria katika kikao cha bajeti cha wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2012/13.
"Wananchi wetu wawe huru katika kutoa maoni ya mchakato wa Katiba…kama watu hawataki Muungano waseme, ikiwamo wanaotaka Muungano wa mkataba akina sisi … mfumo huu wa Serikali mbili kwangu mimi sebuu," alisema Mansour akimaanisha anaukataa moja kwa moja.
Alisisitiza kuwa Muungano wa Serikali mbili kwa sasa hauna nafasi tena na hauwezi kuisaidia Zanzibar kwenda mbele na kupiga hatua kubwa ya kiuchumi kutokana na Zanzibar kukosa sifa ya kuwa Dola yenye kumiliki uchumi wake.
Alitoa mfano wa maeneo huru ya uchumi ambayo yalitangazwa na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk Salmin Amour mwaka 1992 Fumba yakiwa na eneo la hekta 900 za msitu zilizotengwa, lakini yameshindwa kuendelezwa na kubaki msitu wanaoishi wanyama aina ya komba na ngedere.
"Tusidanganyane hakuna mwekezaji anayeweza kuja kuwekeza katika maeneo huru ya uchumi yaliyo Fumba kwa sababu Zanzibar haina uwezo wa kuhimili uchumi wake na ndiyo maana maeneo hayo yamekuwa msitu wa kuishi komba na ngedere," alisema Mansour. Hakuna wa kumtisha.
Alisema zama za kutishana zimepitwa na wakati na kufafanua kuwa kutofautiana katika mawazo isiwe chanzo cha kutukanana na kudharauliana na kusingiziana kiasi watu wengine kuonekana wahalifu wakifananishwa na wafuasi wa vyama vya kisiasa vilivyopita ikiwamo Hizbu na Jumuiya ya Mihadhara ya Kidini ya Uamsho.
Alitoa mfano wa viongozi walioongoza kwa vitisho na nguvu za kijeshi, kwamba kwa sasa hawapo tena madarakani kutokana na wananchi kuwapinga na kuwakataa moja kwa moja wakiwamo marais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak na wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.

Chanzo: Habari Leo

Scotland, Wales and N. Ireland hawana kiti UN wanatumia kiti cha UNITED KINGDOM; sasa kama wanataka kiti chao

Ina Maana tutakivunja kile cha TANZANIA na kuwa na cha TANGANYIKA na ZANZIBAR; sasa hapo HATUNA MUUNGANO

Si ndio Maana ya Wanavyosema? Sasa kuhusu Wananchi Wanaokaa Sehemu mbili tuwajadili pia sababu ni kuvunja

Muungano kiaina yake... Na Bara kwa kweli hatuoni ni Tatizo sababu kuendeleza hivyo inatuletea UGOMVI; UDINI,

na KUGOMBANIA MALI haswa KATI YA TANGA na PEMBA
 
Back
Top Bottom