Waziri apiga marufuku vimini au tight maofisini!

GHASIA ASILETE GHASIA HAPA, kama nikusimamia sheria mbona anakuwa selective, kwani sheria ya rushwa haipo, sheria ya kulipabeli za maji haipo au hazijui. mavazi ya heshima ni yapi? mfano yeye kuficha uso kwenye hijabu ajui kwa wengine anakuwa tayari amekiuka maadili, maana yeye kama ofisa wa umma (yaani watu wote) kule tu kuwa amevaa mavazi ambayo moja kwa moja yanatambulisha dini yake anakuwa ameisha onyesha alama kwamba anaweza asiwatendee watu wengine haki (anakuwa hayuko neutral). anataka nguo isiyovuka magoti hiyo si ni min-hijabu.
mimi namuomba ashughulikie maadili ya rushwa,uzembe, uchelewaji, lugha chafu nk aachane na mavazi.
 
Mimi naafiki suala la kuwa na utaratibu wa mavazi unaoeleweka mahala popote kazini. Sioni kama tuna haki ya kubishana au kuwakosoa wenye ofisi ZAO kwa kuweka au kusimamia sheria na kanuni ZAO za kazi, ikiwepo utaratibu wa uvaaji, kuheshimu muda wa kazi, utendeji bora nk nk. Hata hayo mengine yamekuwa yakipigiwa kelele na mawaziri na watendaji wengine wakuu mahala pa kazi. Sijaona mtu akiwatukana kuwa wanaleta masharti ya dini zao au maadili yao na kwamba watu wafanye kazi kwa mpangilio wautakao wao! Kwanini mnamshupalia mama waziri ati analeta mambo ya dini au anakuwa headmistress nk?
Hekima inaniongoza kusema kuwa tumwache waziri afanye kazi yake. Kama unafanya kazi ofisi za serikali na huwezi kufuata sheria zao, FUNGASHA VIRAGO, KAAJIRIWE KWENYE CASINO AU NIGHT CLUB!
Hongera mama Hawa Ghasia!!!
 
Nakumbuka wakati wa kampeni huyu mama alizomewa na wapiga kura wa jimbo lake. Kumbe walimjua si kitu si lolote. Mavazi enzi hizi!! Hivi hujui unavyovaa hilo hijabu unawakera pia wengine? Je, kikwete angekuwa anatinga kanzu na kibarakashia kila siku unadhani ingekuwa na tafsri ipi? Usilete mambo ya msikitini kwenye utumishi wa uma. Huna credibility ya kulisimamia hilo, kwani wewe unaonyesha uko biased..unavaa vazi la kidini ofisini..una udini..au ndo mlolongo wa mambo kama ya kutaka mahakama ya kadhi? Vaa hijabu yako an acha wengine wavae yawafaao..wewe kama unavaa kwa shinikizo, ni tatizo lako binafsi. Buni cha maana, si kuleta kero.

Haya mawazo duni ndo unakuta vitoto vya shule navyo hijabu! kwani kulikuwa na vimini nako huko? Hiyo sheria ya mwaka 1961 siyo sheria sasa, ni SHARIA..maana imepitwa na wakati.
 
MUHASHIMIWA ANASEMA ..anapiaga marufuku nguo zinazoachioria ushabiki ..hapo ina maana huwezi kuvaa nguo za chama chako[rangi au nembo],nguo za klabu yako,pia nguo inayoashiria dini ..kwa maana hiyo basi yeye pia anatakiwa abadili uvaaji wake maana unaonesha kuwa yupo biased ..ingetosha pia kama akivaa bazee la kiadrika na kilemba kikubwa [or something like that]kama lengo ni kujisitiri na isingeashiria imani yake!!!
 
Kwanza sheria yenyewe ni ya mwaka 1961, sijui hapo analeta vitu gani, atataka na wanaume waanza kuvaa suruali za zamani na raizoni, na kuwataka wanawake wasitengeneze nywele wawe wanawake afro.
 
Kwanza sheria yenyewe ni ya mwaka 1961, sijui hapo analeta vitu gani, atataka na wanaume waanza kuvaa suruali za zamani na raizoni, na kuwataka wanawake wasitengeneze nywele wawe wanawake afro.
Tena naomba kuongeza, sheria ya 1961, pia ilisema ya kuwa watanzania wasivae nguo zilizotengenezwa kwa vitambaa vya nje, bali kanga vitenge na batiki! Haya Ms Ghasia, kazi kwako!
 
Mambo ya tamaduni za kuiga hayooooo....

Bora kila mmoja wetu maofisini avae kama Wamasai basi. Hilo nitaliunga mkono.


SteveD.
 
I think our priorities are upside down! The minister should focus in address the civil servant morale and motivation, work ethics, accountability etc.
Kwa kutovaa vimini vinasaidiaje kuboresha utumishi wa umma nchini?
 
Haya jamani, bado mko pale pale? Mwajua kuna ofisi kibao za kuajiriwa? Mtu halazimiki kuajiriwa katika ofisi ya serikali kama sheria hiyo (iwe imepitwa na wakati au imeupita wakati!) inamkera! Ofisi ziko kibao, kuanzia naiti kilabu hadi makasino! Waende wakaajiriwe huko wapenda vimini, shida iko wapi??? Na kama mtumishi wa serikali anaona sheria (au SHARIA) ile ni kinyume na haki zake kama binadamu huru, aiburuze serikali mahakamani, bila shaka kero hii itapigwa dharuba ya kisheria (hata kama si ya KISHARIA!)
 
Haya jamani, bado mko pale pale? Mwajua kuna ofisi kibao za kuajiriwa? Mtu halazimiki kuajiriwa katika ofisi ya serikali kama sheria hiyo (iwe imepitwa na wakati au imeupita wakati!) inamkera! Ofisi ziko kibao, kuanzia naiti kilabu hadi makasino! Waende wakaajiriwe huko wapenda vimini, shida iko wapi??? Na kama mtumishi wa serikali anaona sheria (au SHARIA) ile ni kinyume na haki zake kama binadamu huru, aiburuze serikali mahakamani, bila shaka kero hii itapigwa dharuba ya kisheria (hata kama si ya KISHARIA!)

Tatizo hapa Mkuu, ni priorities na matumizi ya jukwaa la siasa kutoa maagizo ya kiutendaji. Kama tamko hili lililengwa kwa watumishi wa umma basi kuna namna ya kuwataarifu na sio huku kutangaza hadharani. Ni kama vile kiongozi kutoa tamko hadharani kuwa wanaochelewa kazini watakiona! Au aseme anapiga marufuku unywaji wa pombe katika sehemu za kazi! Hivi ni vitu vya kiutendaji wa kila siku na kama kuna maagizo yanayoviongoza ( standing orders n.k)inabidi yatumiwe. Tunachotegemea kutoka uongozi wa juu ni matamko kuhusu policy issues na mambo yenye impact kitaifa. Matatizo yako mengi mno yanayohitaji maagizo na maelekezo kutokaviongozi wetu. Hili kwa bahati mbaya, si mojawapo. Kama ulivyoisha elezwa HAKUNA anaevaa MINI katika ofisi ya serikali.
 
Hapa Waziri, sina uhakika kama anajua wajibu wake kama waziri na kama wizara. Hayo alitakiwa kuwasisitizia tawala za mikoa watekeleze hizo sheria, na solution wanyotakiwa ili kuepukana na mambo ya mavazi ni kuanziaha uniform kwa wafanyakazi, ili kuepusha migongano.

Hivi mtu akivunja hiyo sheria, adhabu yake nini?
 
Hee bibi, usituharibie ndoa zetu kabisaa, wenzio waume zetu wanafurahia tunapovaa hivyo vimini na ndo wanaotununulia, sasa kama we mumeo anapenda kukuona ndani ya hijab masaa yote, poa, mbona hatujakwambia hilo vazi si la kiofisi wakati ukweli ndio huo? Tunajua unao uhuru wa kuvaa kama sisi, kwa nini unataka kutupatia sheria mama, kawambie wanao.
 
Kweli GHASIA akiwa kiongozi wa Tanzania - badala ya kufikiria jinsi ya kuwafariji wafanyakazi wa Tanzania wanavyofanya kazi katika mazingira magumu - foleni ndefu - ina maana kuamka asubuhi sana na kulala usiku sana; kubanana kwenye mabasi - usafiri mbovu wa jiji la Dar es Salaam; ukosekanaje wa umeme - hata kunyosha nguo inakuwa taabu - anawaza jinsi ya kuwaongezea KERO kwa kuleta mambo ya mavazi - kwanza kama serikali hainunui hayo mavazi - yanamhusu nini? mshahara wenyewe kiduchu anadhania unatosha kununua mavitambaa makubwa ya kushona manguo marefu, mapana etc.???? Hivi anajua maana ya GLOBOLIZATION???? Hii ni East Africa kwa sasa hivi - kuna wafanya kazi wa Serikalini; mashirika; makampuni mbali mbali; ma-ubalozi etc. sasa sijui anaongelea Wafanya kazi wapi??? Au hajui kuwa kuna DRESSING CODE kwenye kila taasisi??? Mfano Banks, Hotels, Sheria - mahakama etc. - sasa anataka kuingilia hata CODE AND CONDUCT za makampuni mbali mbali??? Hivi anategemea AIR/GROUND Hostess kwenye shirika la ndege avae long skirt - atamove vipi??? Na hao wafanya kazi wa Serikalini - awaache kabisa - kwanza amewafanya wengi wamekuwa wachovu - kwa kutokuwapa exposure - kama yeye asivyo na exposure - analeta mambo ya mwaka 1961 - Badala ya kufikiria kuwajaza MAPESA anafikiria kuwa sheria za mavazi - ANAUDHI SANA HUYU HAWA GHASIA - kama hana interest ya kuwa SMART - abakie hivyo hivyo -
 
asee natumbuaga macho nikiwa
angahizo za hicho chuo.wangebidi
waanzie hapo chuoni
ili akili zijenge mazoea hayo ya nguo ndef
otherwise wakitoka chuo wataendelea tuuu kutandika vimini alaaa



mtoto wa mkulima kile chuo bado kipo ila ni balaa jinsi wanavyovaa. Labda waanze ni hicho chuo chao.
Ila ni ushauri mzuri wa kazi, siku hizi watu wanavyovaa kazini kama wanaenda disco, dressing code ni muhimu sana sehemu za kazi. Na kwa kuwa serikalini hamna dressing code wadada wanavaa vipedo na tops kazini!!!

admin hii thred iunganishwe na aliyopost mwanakijiji inaongelea issue moja.
 
hii ni nzuri lakin katika utekelezaji kuna weza tokea matatizo kama sera na sheria itakosa msmamiz wa kueleweka na aliye fair na reasonable. mfano kuhusu vimini iwekwe wazi kabisa kimini ni aina gani ya vazi na sketi ili iwe kimini inatakiwa iishie wap au ifike wap? maana isije ikawa kila ofisi wakaweka tafri yao na kila bosi akaamua ajuavyo.
 
Bado sijaona tatizo la Vimini, mbona ni mambo ya kawaida tu jamani? Labda kama kuna mtu anishawishi ni kwa kiasi gani vimini vimesababisha matatizo kama:- Mgao wa umeme, hali ngumu ya maisha, ukame, njaa, malaria, kipindupindu, uvivu wa kufikiri miongoni mwa viongozi wetu, Ukimwi, utapiamlo, ukosefu wa kazi, mass failures kwenye mitihani nk.
 
Anawaonea wivu wafanyakazi wanaopendeza ndani ya suti zao na staili zao za nywele. asilete sheria za mwaka 47 kwenye karne hii ya utandawazi. yeye atueleze kwanini wafanyakazi hapandishwa vyeo kwa upendeleo kwa vile kuna wanaopanda kila baada ya miaka miwili na kurekebishiwa mishahara. apite kila taasisi ya serikali kukagua waliopanda vyeo miaka kumi iliyopita kuona kama wanastahili.hiyo ndio kazi anayopaswa kufanya nasiyo eti mdada leo kavaa nini. shauri lake anayependa kuonyesha tumbo na matiti yake hadharani tena ofisini.yeye mbona anavaa Hijabu ofisini kwani ofisi msikiti?
 
Back
Top Bottom