Waziri Angela Kairuki: Uhakiki wa vyeti haujafanywa kwa Viongozi walio katika nafasi za kisiasa!

Sifa ni kujua kusoma na kuandika,lakini vipi kuhusu kosa la jinai la kufodge vyeti???Maana kama wasingeingia kwenye siasa wangevitumia kupata ajira!
Hivi tunajua maana ya "Forgery" au "Fake" item? (Kugushi cheti) Je? Kuwa na majina mawili tofauti ni forgery? Nijuavyo Kugushi ni kuigiza Saini, maandishi au muundo wa bidhaa ya mtu mwingine kwa lengo la kuhadaa na kuhalalisha matumizi yake. Jina ni utambulisho wa mtu ambao mwenyewe au kwa niaba yake, mtu mwingine anaamua kulitumia katika kujitambulisha kwa wengine.
 
Nayakumbuka maneno ya rais wangu pale Bandarini. Alivyo wa chachafya wenye vyeti feki. Aliwaambia; Toa cheti halali cha darasa la 7 tu wala usihofu. Kioneshe wazi nasi tukupime kwa kazi yako.
Iweje leo mnahalalisha wanasiasa ati hawatasumbuliwa na vyeti vyao?? Mbona mnasema hata darasa la kwanza tu au ngumbaru bora tu ajue kusoma na kuandika?? Kweli nimeamini, ndo maana wanapigia kelele kiswahili hadi chuo.
Msihalalishe maiti. Simamieni maneno ya rais. Onyesha cheti chako halali hata ka ni darasa la 7. Tukupime kwa kazi yako nzuri.
Bashite, onesha sasa vyeti halisi, mkuu kishakupa neema. Ningelikuwa ni mimi, ningeonesha kile cha darasa la 7 na kuwa sina kingine. Mwanasiasa au mteule wa rais haguswi woga wa nini?? Usiache neema hii ikupite. Ukiendelea kushupaza shingo, unamharibia aliye kuteua.
 
Kwa nini huombi vyeti vya mbowe lowasa na sumaye na tundu lisu na mchungaji msigwa Vihakikiwe? Kuanzia vya kuzaliwa?
Mkuu hao unaowataja ni vichwaa balaa yaani walipata ABABABAB tena kam msigwa sijui kwanini asiwe ndiye mshauri mkuu wa serikali.


Ana elimu yakutosha
Ana upako wakutosha

Serikali lazima iwe safii
 
Hivi tunajua maana ya "Forgery" au "Fake" item? (Kugushi cheti) Je? Kuwa na majina mawili tofauti ni forgery? Nijuavyo Kugushi ni kuigiza Saini, maandishi au muundo wa bidhaa ya mtu mwingine kwa lengo la kuhadaa na kuhalalisha matumizi yake. Jina ni utambulisho wa mtu ambao mwenyewe au kwa niaba yake, mtu mwingine anaamua kulitumia katika kujitambulisha kwa wengine.
Basi kuanzia leo naomba niitwe Ibrahim Lipumba,msisahau kunipa na uprofesa!
 
Inawezekana vipi asiyethamini vyeti ndiye afanye uhakiki wa vyeti? Je si wakati sasa wanasiasa kujitenga na mambo ya kitaalamu Maana wao ni kujua na kusoma tu?
Kusoma na kuandika.......... This is Tanzania!!

I'm loving it!!
 
Huyu rais kuna baadhi ya mambo anafanya inabidi kama binadamu uliye kamili ufikiri mara mbili.
 
Mkuu wa nchi amewatoa kafara watumishi 9932 ili kumlinda Daudi Bashite.

Mbele ya Bashite hao wote 9932 ni watakatifu.
 
Hivi cheti cha sekondari katika kutafuta ajira kina uzito mkubwa kuliko cheti cha diploma au degree na Ma PhD feki? Inakuwaje nguvu kubwa inawekwa ktk vyeti vya sekondary wanaacha ngazi nyingine? Anayefoji cha ngazi ya juu ndiye anapata madaraka makubwa na mshahara mkubwa na deal kubwa na hawa ndio wanatia taifa hasara.
 
Oyoooooo bashite yuleeeee anaendelea kupeta wanaomwombe mabaya wanaendelea kunyong'onyea piga kazi bashite katiba inakuruhusu
 
Binafsi nimeiona faida kubwa ya vyeti feki vya Bashite ktk Taifa hili kulikoni angefaulu.
Faida ni hii, baba kupambana kumuokoa mwanae ktk sakata la vyeti feki au niseme kuliepusha chaguo lake lisimtie aibu, amejikuta akiwasamehe watumishi hewa zaidi ya elfu tisa na kujitutumua tu kuwa waondoke kazini kuanzia leo kwa usalama wao.
Kama sio umbulula wa bashite basi hawa wangepambana na mkono wa sheria na kuishia lupango baada ya kichapo cha wazawa wa ccp waliopata sifa ya undata kwa kigezo sifa cha urefu, kujua kusoma na kuandika basi.
 
Back
Top Bottom